Unajua historia ya bendera ya taifa lako tangu 1885? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unajua historia ya bendera ya taifa lako tangu 1885?

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Luteni, Mar 5, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hii ni bendera wakati tuko chini ya Wajerumani 1885-1919
  [​IMG]
  Flag of Deutsch-Ostafrika (1885-1919)

  [​IMG]

  Hii ni wakati tuko chini ya Mwingereza 1919-1961
  [​IMG]
  Flag of Tanganyika (1919-1961)


  [​IMG]

  Hii ni wakati tulipopata uhuru 1961-1964
  [​IMG]
  Flag of the Republic of Tanganyika 1962–64

  [​IMG]


  Hii ni bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toka 1964-..........

  [​IMG]

  Una maoni gani kuhusu bendera hizi je zinagusa au kuchangia sehemu yeyote ya maisha yako au unawezaishi bila hata kujua ama kutambua bendera yako ikoje kifupi hazisaidii
   
 2. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2010
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nashukuru sana kwa somo hili la Histroria. Nilikuwa naijua bendera ya Tanganyika lakini hiyo ya Deutsch Ostafrica na hiyo ya Tanganyika protectorate nilikuwa sizijui. Nashukuru sana kwa somo. Nimecheka kumuona Twiga kwenye bendera ya Tanganyika ilipokuwa chini ya mwingereza, kumbe tumetoka mbali na twiga mnyonge. Nadhani twiga aliwachengua wazungu.
   
 3. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nyerere alibadilisha kidogo tu hiyo bendera ya Tanganyika kwa kuiongezea rangi ya bluu na kufanya hiyo rangi ya njano na nyeusi kukaa diagonal.,najiuliza bendera ya Zanzibar kabla ya Muungano ilikuwa inafananaje, au ndiyo hiyo bluu kwenye bendera ya Jamhuri maana rangi zote zilizobakia ni za bendera ya Tanganyika.
   
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wala! Hazinigusi chochote, naona ni matambara tu yanayotungiwa maneno matamu masikioni mwa watu.
  Nawashangaa wanaochoma moto bendera ati wana hasira na serikali zenye bendera hizo.
  Damu inayogusa maisha ya mgonjwa siyo ile unayoiona kwenye chupa bali ni lile tone la damu linaloingia ndani ya mshipa wa damu. Je, umasikini wako unaondoka kwa kuiangalia bendera? Njaa hutoweka kwa aina ya rangi y abendera? Viini macho tu hivyo.
   
 5. H

  Haika JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,319
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Bendera ni signature inayotakiwa kunyesha umiliki wa sehemu, au uwakilishi wa jambo, nadhani ilianza zamani enzi za vita vya silaha za mkonomi ndi wanajeshi wahika bendera wakitangulia mbele kishujaa na vita iliisha wanasimika bendera. ina maana ENEO LINAMILIKIWA.
  Watu waliopo katika eneo wanatakiwa waifurahie bendera au waichukie bendera kwa matendo wanayofanya wale watawala.
  Wananchi tunavyochukia utawala, inabidi tufanye juu chini tuitoe hio bendera,
  manake inavyopepea ina maana kuwa hao wanaiopenda ndio wanatutawala au sio jamani?
  Au tunajitawala wenyewe???
  binafsi naona aibu kuitazama bendera, manake inaitwa ya kwetu, na inafanya vitu vya ajabuajabu
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,934
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tungebaki chi ya jerumani nafikiri mambo yangekuwa mazuri zaidi ya hawa waingereza
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,517
  Likes Received: 7,271
  Trophy Points: 280
  Asante sana kwa hiyo update yenye akili, lakini kinachonisikitisha ni kwa watanzania wengi ni kutojua milalo ya rangi, CHA AJABU HATA HAPA JF, HOUSE OF GREAT THINKERZ, INVISIBLE NA MELO WANASHINDWA KUJUA KUWA RANGI YA BLUE ALWAYS INAKUWA CHINI NA WALA SIO JUU, HEBU ANGALIA HII HEADING YETU YA NENO JAMII FORUMS HAPO JUU
   
 8. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,373
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Chimunguru, kikubwa ambacho huwa nawza tungerithi toka kwao ni discipline ya kijerumani. Unajua wabongo hatuna discipline kabisa, si ya kazi, si ya sheria, si ya chochote. Kila kitu tunajifanyia tupendavyo.

  Yaani hatuna lolote, tumejikatia tamaa na kila mtu kufanya apendavyo. Kinachoniuma, mtu akipewa dhamana tu, ndo kama ameambiwa "chukua chako mapema"
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hata mimi najiuliza ina maana Zanzibar hawakuwa na bendera kabla ya muungano ngoja nimtafute MrFrositry
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Naona kwa wakati huo kwini hakuona kitu kingine kizuri zaidi ya twiga ingekuwa leo angeweka kipande cha dhahabu
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nimeona mkuu ni kweli nimeona nembo ya JF bluu iko juu na kijani chini labda hawakuwa na maana ya bendera ya taifa nafikiri Invisible atakaposoma post yako ataelewa
   
 12. M

  Magehema JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 449
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot]Bendera ya Tanzania ina rangi nne; tunaambiwa kwamba moja kati ya rangi hizo ambayo ni njano inawakilisha madini tuliyonayo hapa Tanzania. Najiuliza kizushi, kwa kasi hii ya uchimbaji inayofanywa na wawekezaji na wachimbaji wadogodogo, hayo madini yakiisha tutatakiwa kubadili rangi bendera yetu na kuondoa ile rangi njano?[/FONT]
   
 13. D

  Danniair JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 360
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Napenda kutoa hoja, hadi leo hii ukimchukua mtoto wa Tz chini ya miaka 14 na kumpa sampuli mbali mbali za bendera ya Taifa letu, ni uhakika atakuchagulia bendera isiyo isipokuwa utamchanganya kwa ile mishazari yake. Ukipita sehemu mbali mbali zinapotungikwa bendera hii utaona maajabu. Mfano mzuri ni hivi vibendera vya kutoka china, serikali inaona vinauzwa huku vikiwa havina rangi rasmi ya samawati (blue) lakini imenyamaza tu. Nilikutana na polisi pale TAZARA akiwa na beji ya bendera yetu hapo ndipo nilichoka, kijani inaelekea kuwa njano, samawati inaelekea kuwa kijani! Hiki kwa mtazamo finyu ni kitu kidogo lakini madhara yake ni makubwa iwapo kitadharauliwa. Nawasilisha hoja
   
 14. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 803
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Kama tumeanza kwa kuunda tume ya kutafuta vazi la taifa, nadhani sasa ni wakati muafaka kuundwa kamati ya kupitia upya RANGI za BENDERA yetu ya Taifa, kwa kuwa hakukuwa na kamati maalumu ya kukusanya maoni juu ya muundo na rangi zake, je rangi zake bado zina maana ileile?..

  Nyeusi - Je bado inamuwakilisha Mtanzania na je ni Mtanzania ni mweusi tu?
  Kijani - Je bado inawakilisha uoto wa asili, je Mtanzania anafaidika kwa kiasi gani?
  blue - je bado inawakilsha bahari/maji , Je Mtanzania anafaidika nini na hili?
  Njano - Je bado inawakilisha madini yetu, je haya madini yanamfaidisha vipi Mtanzania

  Je rangi hizi ziendelee hivi hivi au kuna sababu ya kuzibadili, kabla hazijaingizwa kwenye vazi la Taifa..

  Wakati huohuo vipi kuhusu jina la nchi yetu?..
   
 15. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 32,585
  Likes Received: 12,019
  Trophy Points: 280
  Ngoja nilale kwanza nitarudi hapa kesho mapema sawa eh!
   
 16. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,690
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Sina hakika sana mantiki ya hoja zako zimelalia wapi, ila nionavyo mimi hakuna haja ya kuunda kamati ya kujadili rangi za bendera ya taifa. Ni kweli viyu vingi vinabadilika kuendana na wakati na mabadiliko ktk maisha yetu ya kila siku, ila hili la kubadilisha rangi za bendera sioni kama linawezekana vipi.

  Katiba inaweza kuandikwa upya ili kukidhi mahitaji ya wakati fulani. Hii inaewezekana kwa kuwa ndiyo dira na mwongonzo wa maisha yetu ya kila siku. Kuna mapugufu yanaonekana, yanarekebishwa then tunasonga mbele.

  Nahisi huja ya kutaka kuwa na vazi la taifa ni moja ya mbinu za kuturudisha kule tulipopotea na kuacha maadili yetu kama taifa hasa katika nyanja ya mavazi. Ni ukweli usiopingika kuwa siku hizi mtu aweza kuvaa nguo yoyote tu aipendayo bila kujali jamii inayomzunguka ina mtazamo gani juu ya vazi hilo.

  Kibinafsi mimi naunga mkono kuwepo na vazi rasmi kitaifa. Lakini pamoja na hilo, bado napinga matumizi makubwa ya rasilimali ktk mchakato wa kubuni na kufikia kupatikana kwa vazi hili. Ni ukweli usiopingika kwamba pamoja na kuwepo kwa vazi hilo la kitaifa, bado tutaendelea kuona vivazi vyetu hivi vya machukizo mitaani wamevaa kaka na dada zetu.

  Nikirudi kwenye mada yetu, kiukweli sioni tatizo la rangi za bendera yetu. Tukitaka kufuatilia dhima ya rangi zile, mimi naona ni ileile.
  Weusi ni rangi yetu Waafrika na itabaki kuwa hivyo milele. Kama tuna shaka na hili ni vema mtu mmoja mmoja akiamua aende dukani anunue rangi ajibadilishe ila rangi ya bendera yetu ibaki vile vile.

  Na ikiwa tatizo ni kwamba tume haikuundwa wakati wa kubuni rangi zile, inawezekana ni mapungufu kweli. Lakini, je hayo mapungufu yana madhara gani kwetu? Je, zile rangi zina mapungufu gani ya kimantiki hadi tuhitaji kufanya marekebisho?

  Zile rangi 3 zilizobakia mimi sioni shida. Ikiwa haziwakilishi hizo rasilimali hilo ni tatizo. Ila ikiwa haturidhiki na mgawanyo wa rasilimali hizo, hiki ni kitu tofauti. Rangi kama rangi hazina la kufanya ktk hili, kwa maana nyingine, hatupaswi kulaumu rangi ya bendera yetu. Ni lazima tutafute kitu kingine cha kutupia lawama lakini sio rangi za bendera. Mimi naamini maliasili zote zilizowakilishwa kwenye rangi za bendera zote zipo. Ingawa hakukuwa na tume maalum ya kubuni rangi za bendera yetu, lakini hata hivyo tunapaswa kumsifu huyo mwenzetu aliyeweza kubuni hiki kitu, alikuwa ni mtu makini.

  Nionanyo mimi, kama kuna mtu anayetakiwa kulaumiwa kutokana na kushindwa kunufaika ipasavyo na hizi rasilimali zetu, ni wewe na mimi. Tumeweka wasimamizi wa hizi rasilimali zetu then wameshindwa kuzisimamia vizuri na sisi tumekaa kimya. Tunapaswa kulaumiwa sisi wenyewe. Tumeshindwa kuweka watu makini wa kutuongoza vizuri, badala yake tunaanza kuhoji uhalali wa rangi za bendera ya taifa. Haya ni mapungufu.

  Kwa hilo la jina la taifa kwa sasa sina comment. Ngoja nikalitafakari kwanza huenda nikarudi baadaye.
   
 17. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sr, heshima mbele sana mkuu.

  Hili ni jambo la msingi sana, sasa inabidi tuanze na hili na ndiyo tuje kwenye mavazi na viwalo vya taifa, kuanzia maofisini, kenye michezo, mashuleni n.k..

  Hizi rangi naona zimepoteza maana yake kwa sasa, zilikuwa na mantiki ya ki ujamaa na kujitegemea lakini kwa sasa sivyo sasa ni wakati muafaka wa kuzipitia tena, kama ndugu zetu wa zenj.
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,994
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Mbona bendera ipo?

  ............................ [​IMG]
   
 19. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,848
  Likes Received: 768
  Trophy Points: 280
  Nyie msisumbuke kuunda vazi la taifa kwani tayari la taifa lipo na lina sense za kizalendo kabisa na vazi hilo ni MAGWANDA YA KAKI kama ya cdm kwani ya kizalendo zaid.
   
 20. kalikumtima jackson

  kalikumtima jackson Member

  #20
  Jun 29, 2013
  Joined: Dec 1, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ujio wa Rais wa Marekani unaweza kubaki kuwa ni kumbukumbu kubwa kwetu kama nilichokiona jana, yaani kubadilika kwa muonekano wa Bendera ya Taifa; kutakuwa kumesababishwa na ujio wa Rais Barack Obama!!

  Barabara ya Julius Nyerere inayotoka Uwanja wa Ndege atakapopita Rais huyo kumepambwa bendera zinazofanana fanana na Baendera yetu ya Taifa la Tanzania niliyoizoea.

  Naomba Watalaam wa mambo ya uraia na wazalendo wa nchi hii, mnijulishe kilichotokea mpaka bendera ikibadilishwa au ni kitu gani kinacho sababisha bendera ibadilishwe!

  Naomba mnijuze ni chombo gani chenye mamlaka ya kubadilisha bendera ya taifa na hatua zipi zinazofuatwa mpaka Bendera ikabadilishwa!

  Nilicho kiona kwenye bendera ya sasa ni kuufanya mchirizi mweusi unaokatiza kutoka ncha moja kwenda nyingine kufanywa mkubwa sana na kuifanya rangi hiyo kuwa dorminant kwenye bendera yetu, kinyume na Bendera ya zamani.

  Siku zote huwa naamini kuwa Bendera ya Taifa ni tunu na Alama yetu ambayo ina vipimo halisi na haiwezi kuwa inachezewa chezewa!

  Kama kuna mtu alipewa tenda ya kutengeneza bendera za Taifa kwa ajili ya ujio wa Obama na badala yake akatuletea bendera iliyobadilishwa bila kufuata utaratibu wa kubadilisha Bendera ya Taifa; Naomba asilipwe na achukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu.

  Maskauti wa Nchi wa sasa, mnaona kama mambo yako sawa na bendera yetu?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...