kweli kabisa, mtu yupoyupo tu, analoliongea kila siku watu hawamwelewi, pumbapumba tu, na bado anataka watu wamthamini fo who she/he is haoni kama inabidi atumie nguvu ya ziada ili apate thaminiwa na jamii?Ni kweli kujithamini au kuthamini wengine kunatokana na kujitambua wewe binafsi. Na hili kujitambua wewe binafsi inabidi ujue tamaduni za jamii inayokuzunguka iwe kazini, familia au hata Pub. Kwa kujua hilo ndio utaweza kushusha au kupandisha vigezo kutokana na maisha ya jamii hiyo.
Mara nyingi ukijishusha kwa kiasi fulani utakuwa na uwezo mzuri wa kujitambua na kujichaganya na kukubalika na jamii sehemu yeyote hile..hata pale nyumbani kwako jaribu kujishusha na kuthamini kazi za House girl au Houseboy wako..jaribu kumfanya kama mdogo wako na uone matokeo yake.... Pia tukumbuke hakuna kipimo cha thamani..sio cheo, wala hela, wala mavazi, wala mikogo..wala kutoa misaada..vyote hivyo havisaidii kupandisha thamani yako ..Thamani ni kukubalika..na kuheshimika kwa kujishusha kwako albeit ilibidi uwe juu... Hata walevi wanathamani na kuthaminiwa wakikutana kwenye jamii za walevi wenzao..ni utamaduni na vigezo vyao. Hapo utaona thamani inakuja yenyewe na wala sio wewe unayeiweka au kuilazimisha... kikubwa.. Jitambue..jishushe ili wale wanaokuzunguka ndio wakupandishe..
Kweli kabisa Tulizo, ila sie waafrica hapo bold huwa ngumu sana, wengi wetu kujishusha ili tupate faida fulani hatuwezi, natokeo yake kila mtu kichwa juu hata kwenye jambo anaona kabisa anatakiwa aje chini lakini hakuna
Kwa nini najithamini? ni hivi, dunia nzima kuna watu zaidi ya bn. ngapi? and who will give a damn about me other than myself??!..nobody!
Vyovyote ulivyo lazima mtu ujithamini, ukisubiri kuthaminiwa itakula kwako. yes, kuna muda mwingine mtu ukikutana na matatizo unaweza kujiona huna thamani lakini maisha ni pande zote na ukifahamu hili unatakiwa kutatua matatizo kwa kadiri ya uwezo wako.
Sijui aisee, najithamini na kujijali sana katika haya maisha!!..
Dah, hapo penye wekundu, mbona sie wengine ni wepesi kung'amua nimechemsha?
Kumbe kuna wenzangu hutumia muda mrefu kugundua 'wana bore?'....well well well!
...kuna wengine wanawatishia wenzao nyau hata hapa JF na u Snr/Premium Member.
Yale yale, ha ha ha...Nimekusoma kituo kwa kituo.
Ashadii, asante kwa mchango wako.
Mbu, pia ukiona watu wanakuzongazonga kwa kukukashifu sana pasipo na tija ,na kukutaja kwa sana ujue tu thamani yako iko juu mbele yao ila wao tu hawajijui kama wanakuthaminisha ki namna fulani
Shantel umeandika jambo la maana sana. Kujithaminisha mwenyewe ni jambo la busara sana. Bahati mbaya, ni wachache mno wenye uwezo wa kulitambua hilo. Tatizo linaanzia kwenye maamuzi ya mtu na mtu. Ukishajikubalisha Mwanadamu mwingine akuamulie maamuzi yako, naamini taratibu utaanza kupoteza uwezo na thamani ya maamuzi yako. Hilo litapelekea kuanza kupoteza uwezo was kujiamini (Confidence & Self esteem)
Mfano;
Ni rahisi sana kwenye mapenzi mtu akakujengea hisia hakuna mwingine kuliko wewe. Hakuna ubaya katika kulitambua hilo, ubaya ni pale nawe utaposhindwa kujithaminisha kiukweli uwe mbora kuliko mwingine.
Kimtazamo wangu, kila mmoja wetu amejaaliwa mazuri fulani ambayo yanamtofautisha na mwingine. Mtu atapokupendea kwa mazuri yako, wapaswa nawe kuyajenga na yale ulokuwa na upungufu nayo ili uweze kujikamilisha japo kwa asilimia kubwa zaidi.
Lakini vile vile, ...kuna watu ambao ni mahodari kuwakatisha tamaa wenzao. Watakuja na hadithi za, 'hujapendeza!' 'hujaelimika!' 'huna hoja!' 'hujui hili na lile' nk nk nk.... Ikiwa nawe ni mdhaifu, uka ya accomodate mawazo ya nje yakutawale maamuzi yako, jijue unajichimbia kaburi la kutaka kum- please mtu, ilhali unajipotezea Values zako.
Negative comments ni Challenges za kukupima uwezo wako, "thamani yako!"
Spot on ndugu yangu!...kujikweza kunatuharibia sana ndugu yangu. Tatizo la kujikweza hapafu watu wakaja kubaini mapungufu yako, kunawapelekea wengi kupatwa na msongo mkubwa wa mawazo, na hata wengine kujionea bora wakatishe maisha kuliko aibu watayoipata.
HB ni mtu wa namna gani?ufafanuz plse...!Likwanda HB yoyote hajiamini ana wasi wasi na hajiamini kuwa amekamilika. So kila mara ana wasi wasi kuwa kuna tatizo au hana uhakika akitoa ushauri utasikika
Mwenzangu nlikuwa namaanisha angalia saa sita usiku wakati mwenzio anategemea uwe pembeni yake mwapeana joto, mie ninapost JF si najishushia thamani kwake LOL! Nahata kama kaniomba nisiingie JF kwa kuwa na usiku sana, mwanamke mimi sijatii! Si najiandikia talaka kabisa hapa?Hongera mwaya, msalimie Liberian galmnnhh, nini tena? LOL...mbu is engaged to 'Liberian Girl.'
Duh! kaka umepiga ngumi ya jicho...mule mule pamoja na misifa yoote hiyo..nyumaya pazia ni mizigooo..tena magunia ya misumariWanasema wewe una thamani gani bila title yako?????
Mfano kuna watu ukiondoa title wanazoshikilia mfano dokta fulani,
au professa fulani.....
Au manager fulani
au mmiliki wa kitu fulani.......
Wako sooo empty ,ni kama hawawezi ku exist bila titles hizo......