Unajitangazaje au unawajulisha vipi watu kuhusu biashara yako?

Sio lazima iwe promo ya biashara yako ya pants mkuu,katika kila biashara tunazofanya lazima kuna biashara ndani ya biashara Mfano mzuri ni mtu mwenye Duka la vinywaji Automatical huyu mtu atauza vinywaji vyote kuanzia maji,juice,soda,bia,nk nk Japo yawezekana ofisi yake vinywaji vingi ni BIA na SODA tu.

lakini kwasababu kaona juice inauliziwa kaamua aweke,kaona maji yanauliziwa kaona aweke pia ila wakati anafungua biashara alifungua kwa lengo la kuuza BIA na SODA tu.

Hapa naongelea zile biashara zinazoingiliana kwenye biashara 1,wewe kokudo unauza underwear dukani kwako,wateja wako 81% ni kina dada,umeshajua kuwa asilimia kubwa ya wateja wako n wadada maana yake biashara yyte inayomuhusu mdada/mwanamke inafaa kuwepo hapo ofisin kwako.

Na assume mimi ndio wewe,nmefungua duka kama lako nahitaji wateja wajue ninauza nini na nimefungua frem mitaa hii,nitakachofanya ni simple tu Naingia Town nanunua hereni zile zinazouzwa set mfano kama hizi hapa chniView attachment 1510060

nachanganya na hivi vidogo dogo vya namna hii hapa chini

View attachment 1510061View attachment 1510062


Kisha natengeneza meza yangu nzuri sana naiweka ndani ofisini Namwaga mzigo kama wa 100,000 au wa 50,000 inategemea na mfuko wangu uko vipi hiyo siku.

Hizi hereni kwa walio dar ukiingia machimbo kule k.koo wanauza 1500 kiset kizima cha hereni hata 20,vingine 2500 vingine 5000 mpk 15,000 na kuendelea,Sasa mimi ntachanganya za bei rahisi ntaweka nyingiiiiii halafu za bei kubwa ntaziweka chache flani.

Tuchukulie mfano hizi hereni za pcha ya mwisho k set chake umekinunua 3000 k.koo ila kina vihereni vidogo vdogo 30 maana yake kila kihereni umekinunua kwa sh 100, Ukaweka mtu hapo nnje ana mike akawa anapiga kelele kwa mbwembwe kama ZOTE anatangaza "ingia ndani uvae hereni,Mwanamke unatembeaje sikio halina hereni leo kokudo kaamua kuvalisha wateja wake wote hereni,kama huna hereni ingia ndani jichagulie hereni UIPENDAYO BUREEEEE"

ukinunua kitu utapata hereni zaidi ya pair 1 bure,usiponunua pia utachaguliwa hereni bure kabisa uvae,tunawapenda wateja wetu karibu karibu karibu,usipite bila kuingia ndani hata ushangae tu kidogo,Kina kaka karibuni mchagulie ma bebeeee vituz....

Wateja+wapita njia watu wote watakua wanajiuliza huyu anaeweza kugawa hereni mtaa mzima ni nani? je ni kweli au anatutania,akiingia wakwanza ukamvalisha hereni huku ukimwambia next time aje anunue underwear,akitoka hata asiponunua TAARIFA ZAKO ZITAFIKA HUKO AENDAPO.

akiiingia mteja wapili,wa tatu wa nne, wa tano wakitoka wote masikio yana hereni MY BROTHER Taarifa/habari zako zitasambaa zaidi ya moto wa petroli.

Kumbuka hatugawi hereni kwamba tuna hela za kuchezea Point yetu ni utambulisho wa duka letu,point yetu n wajue wapi kuna duka la underwear kila mteja ataekuja hiyo siku hakikisha umemkaribsha next time kununua underwear Bro ki set cha 3000 kina hereni 30 maana yake kuna wateja 15 hao

usiangalie hela unayopoteza leo,Angalia hela utakayoipata kesho.

Bado hujapata kitu broo? basi itabidi nikutaftie TUITION na private Teacher.
Wewe ni guru wa marketing mkuu....madini adimu sana.
 
Nimesoma tena na tena

Nakila nikisoma naiwazia Biashara yangu ya Chupi naifanyaje kwa tips hizi naona kama umetumia kiswahili kigumu sana mkuu labda hapa kwenye comments Jaribu kudadavua ili nielewe.

Nimejaribu kuishika ya kupiga kelele na hiyo Ya kuita kampuni inayouza products fulani sasa kwenye chupi itakuaje.

Nikajaribu kuwaza au nikatafute kibali cha matangazo halafu nikodi spika nifunge hapo dukani na Mc Matata kabisa tuanze kazi?

Nitarudi tena naona Maji hayajajaa Bado
Hakuna haja ya kuajiri mtu,,spika unarekodi,kisha unaiachia kazi,wewe unaendelea na mambo mengine,
"Chupi moja shs 1000,2000,3000",etc
 
Hakuna haja ya kuajiri mtu,,spika unarekodi,kisha unaiachia kazi,wewe unaendelea na mambo mengine,
"Chupi moja shs 1000,2000,3000",etc
Siku/Wiki ya kwanza ni vizuri ukaajiri mtu mkuu

maana ukisema u record tangazo la vigezo vyote ni lazima utagharamika

ktk kulitengeneza,maana Tangazo (audio) simple la kuchomeka flash

likaplay kwa mbwembwe zote lina cost 300k linakua na quality sound

linakua na maneno yanayosikka,yani Quality safi lenye vigezo vyote

na hili tangazo ili ulione utamu wake lazima ulichomeke kwenye spika heavy

zinazotema sauti ktk viwango,sasa hii n gharama sana mkuu ndio mana nmeshauri

aajiriwe mtu ambaae unaweza mpa mike akacheza anaongea siku nzima jioni ukampa 7000 tu

ukiajiri mtu atawaona wateja,atawakaribisha,atawaita watu walio mbali,tofauti na recorded Audio.
 
Back
Top Bottom