Unajitangazaje au unawajulisha vipi watu kuhusu biashara yako?

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,935
22,919
Vijana kazi yetu ni moja tu hapa mjini,kuinuana na kupeana mbinu za kusurvive ili kuepuka zile aibu za kurudisha mpira kwa kipa na yale maneno ya "Laiti ninge",katika maneno sipendi kusikia mtu akitamka ni pale anapoanza kusema "laiti ninge" yani ukishaweka "Ninge" ktk sentensi yako maana yake ni kwamba najutia na kuna makosa tyr umeshayafanya.

Leo bwana nataka kuandika kidogo kuhusu jinsi ya kujitangaza kwa wale wanaoanza biashara zao "mpya" lakini hii pia unaweza ifanya mtu yeyote unaefanya biashara ila biashara yako unaona imepooza au inakoelekea unaona kbsa December Haitoboi.

Katika vitu ninavyoandika humu JF jamani nataka mjue ni mbinu ambazo nimeona wengine wamefanya kisha nikazifanya namimi ktk ubora zaidi zikanipa matokeo chanya yani Plus Plus,baada ya kujiridhisha nazo ndio nazileta Humu ili ataesikia na kusoma asome atae ona haviwezekani pia sawa,sasa acha niwambie kwamba Biashara haina Uchawi wala haina Uganga wa kienyeji ila kama unaamini hivyo vitu vinafanya kazi ni sawa lkn kwangu havina nafasi.

Katika vitu vinawarudisha watu nyuma na kuwaangusha ni ukosekanikaji wateja unajua haya mabiashara tunayofanya hatuna tofauti sana na mtu anae BET mpira akampa ushindi man u mwisho wa siku ushndi anachukua Liver,biashara hata uwe na duka limejaa bidhaa mpk unazikanyaga juu Kama hauna wanunuaji ni sawa na Bure tu.

Sasa ili mnunuzi/mnunuaji aje dukani kwako au eneo lako la biashara ni lazima awe na Uelewa kuwa Mtaa A kuna duka la Nguo,Mtaa B kuna duka la Vipodozi,Mtaa C kuna mama ntilie frem ya 7,na ili mteja/mnunuzi awe na taarifa hizi ni lazima wewe unaefungua biashara au mwenye biashara yako Ujitangaze kuwa upo eneo Flani.

Unajitangazaje sasa, Unawajulishaje sasa kuwa umefungua Duka lako la kitu flani kwahiyo waje?

Kwanza ni lazima tutambue mambo mawili katika biashara yeyote ile kwamba

1.huwezi kupata pesa bila kutumia pesa kwanza

upo kwenye hiyo frem kwa sababu ulitoa kodi,uliingiza mzigo,ulifanya marekebisho ya hiyo frem au eneo lako la biashara uliweka taa nzuri za urembo,milango ya aluminium kiufupi hela ilikutoka kweli na hii yote ulifanya si kwa sababu mteja akija akikuta AC atanunua AC,si kwamba mteja akija akikuta shelf za Aluminium atanunua shelf,si kwamba mteja akikuta Flat screen inch 40 limetulia ukutani Atanunua ile Flat la hasha,

Ila ulifanya mambo yote hayo ili kupendezesha ofisi ivutie,iwe na mwonekano na ili wateja wako wakija wajiskie wameingia ofisini na kote huko ulitumia pesa ktk vitu ambavyo havizalishi maana yake n kwamba Uliteketeza pesa kwa ajili ya wateja wako (jambo zuri sana sana)

2.Wateja wanataka vya bei rahisi au Bei Chee ikiwezekana BURE KABISA.

Tupo kwenye karne yenye inahitaji pesa kwenye kila kitu na tunapoendea nahisi hadi salamu zitakua bila hela hupewi shkamooo,hii inapelekea watu kuwa makini sana na matumizi ya pesa zao,hivyo ili mtu atoe pesa kununua kitu ambacho hata asipokinunua leo Kesho atafika,atalala usingizi bila shida,nk yahitaji akili ya ziada kumshawishi huyu mtu atoe pesa yake.

Haya ni mambo mawili ambayo nilitaka kwanza yakae vichwani mwetu kisha tunaendelea sasa na insha yetu ya jinsi ya kujitangaza na kuwajulisha watu kuwa Mimi CONTROLA nmefungua saloon ya kike mje saloon kwangu.

1.OFA KWA BODA BODA WA ENEO ULILOPO

Katika vitu unatakiwa wewe mfanyabiashara utambue na uelewe n kwamba boda boda tunaopishana nao njiani wanamchango mkubwa sana ktk kukuza biashara yako,hawa ndio wanao ulizwa na wgeni na wapita njia kuwa eneo hilii saloon ya kike iko wapi? eneo hili duka la vinywaji liko wapi,eneo hili hardware iko wapi ?

na hawahawa ndio wanaotumiwa na wateja kutumwa kununua vitu kama unga,mafuta,gesi,mkaa,nk vinapowaishia huko majumbani mwao, sasa unafanyaje ili kuwakamata boda boda wote wa eneo lako ulipo ili kila boda boda atae agizwa kitu aje dukani kwako? au kila boda boda ataeulizwa duka flani amuelekeze mteja aje dukani kwako?

Ofa ambazo hutopungukiwa na kitu kama utaamua kuwapa boda boda yeyote ataekuja kununua kitu kwako
  • kuchaji simu zao (bure kabisa)
unajua boda boda ktk shida/changamoto wanapitia ni simu zao kuwaishia chaji na hawezi kurudi nyumbani et kisa akachaji simu,sasa cha kufanya wewe wachajie simu zao bure kbsa kwa shrti 1 tu aje anunue kitu chochote dukani kwako.
  • kifurushi/vocha ya jero
shida nyingine ya boda boda ni salio kifurushi cha 500 ukimpa hupungukiwi na ktu muhimu tu ujue kupga hesabu ya vitu anavyokuja kununua kama vinaingiza faida zaidi ya 1000 unapungukiwa nn ukimpa jero,ambayo humpi hela unampa huduma ambayo n kumrushia kfurush au kumpa vocha maana yake hela bado inabaki kwako(sijui kama ntaeleweka ktk hili)

Hapo unakua umewapata boda boda wote wa eneo ulilopo na ili wawe na uelewa kuhusu hizi ofa n lazima uandae vipeperushi na uvisambaze vijiwe vyote vya boda boda vya mtaa unaofanyia biashara yako,wakishatambua kuhusu hilo basi Ume win.

2.OFA KWA WATEJA WAKO SIKU/WIKI/MWEZI WA KWANZA UNAPOFUNGUA BIASHARA YAKO

Ofa inaweza kuwa ya siku/wiki/mwezi nmeweka muda tofauti kwasababu tumetofautiana vipato,kuna maboss wakutoa ofa kwa siku,wengine kwa mwezi,wengine kwa mwaka mzima ni ofa tu,hii ofa unaitoa kwa namna ipi? Tumetofautiana biashara kwahyo ofa nitakazoziweka hapa zinaweza zisiendane na biashara yako cha muhimu chukua point yangu tu.

Yawezekana unauza MITUNGI YA GESI siku ya kwanza umefungua biashara yako usiuze mtungi hata mmoja kwa faida,yani namaanisha kwamba mtungi umeletewa umeuziwa 30,000 kutoka kwenye kampuni na wewe DAY 1 uza kwa OFA watangazie kabisa MITUNGI 30,000 ofa hii n ya siku 1 au unaweza kwenda kwa siku mbili hapa point yetu si kuuza point yetu n kutangaza Biashara tuliyofungua.

Tumia nguvu zako zote,weka maspika ya matangazo,tangaza OFA OFA OFA MITUNGI YA GESI bei 30,000 YANI uza mitungi kwa bei ile ile from kiwandani hamna mtu mteja mwendawazimu atae ona hapa gesi inauzwa 30,000 aache et aende kununua pale gesi 35,000 HAYUPO. tukumbuke tunapiga hii ofa kwa siku au siku mbili mpk wewe mwenye biashara ukiridhika sasa hapa taarifa zishasambaa ushajulikana Ndipo OFA UNAIKATA ksha unarudi kwenye bei inayouzwa na wote 35,000.

Yawezekana unauza Duka la Viatu Kariakoo unajua kabisa hizi sendo bei ya jumla sh 3000,unajua kbsa hvi viatu jumla 5000 Siku ya kwanza umefungua duka fungulia maspika yako hapo nnje,mpe maiki mwehu mmoja hivi mwambie atangaze OFA YA VIATU ndani ya duka lako uza viatu kwa bei ile ile uliyonunulia k.koo usiongeze hata sh.5 tena uza kwa amani na furaha kbsa. OFA HII utaifanya kwa siku kadhaa kisha ukiridhika kuwa taarifa zimewafikia kuwa kuna duka jipya hapa UNAKATA OFA. unaendelea na bei yako uliyopanga kuuza vitu vyako.

3.KELELE ZA UFUNGUZI WA DUKA LAKO

Unapofungua duka lako hebu usifungue tu frem kisha ukajaza mzigo humo ndani ukatulia,tafuta kitu ambacho ktawafanya watu wakipita washangae shangae hapo kwako tuchukulie una duka la vipodozi na urembo utakachofanya ni kutafuta kampuni yeyote inayo deal na uuzaji wa vipodozi mfano GRACE PRODUCTS nenda ongea na meneja mauzo mpe kihela kidogo kisha muombe Siku flani Aje auze products zao nnje ya frem yako hata kwa masaa mawili tu kisha waondoke.

Nakuhakikishia watakuja tena watakuja na team mauzo yao mtaa huo watasambaa watauza vitu vyao dukani kwako matangazo yakiendelea baada ya 2hrs hao wanasepa wakija kwa mfululizo wa wiki 1 tu tyr DUKA LAKO hata mtoto mdogo aulizwe atajua lipo wapi na ni frem ya ngapi upande upi.

Ukisoma vizuri tangu mwanzo nmeanza kuandika hutoona mahali nmeandika tunapata faida kiasi gani,tunaingiza kiasi gani yani kote huko juu tumeongelea namna ya kujitambulisha/kujitngaza/kuwajulisha watu kuwa UPO wakishajua ndipo baadae unawakamata na kula pesa zao ila wakati huu tunaanza usiangalie faida Lengo lako liwe 1 tu KUITA WATEJA POPOTE WALIPO.

Ukiona biashara yako imemelea legea imepooza hebu tumia hizi mbinu fanya kama ndio umefungua leo kisha Tumia pesa kupata pesa ITA WATEJA kwa mbinu hizi amini nakwambia watakuita mchawi ila uchawi kila mtu ana wake "kichwani mwake". wakati mwingine hatupati wateja si kwasababu wateja hawapo ila n kwasababu wateja hawajui kama Hapo ulipo kuna duka la unachokiuza.

Naamini Ndugu yangu kokudo utakua umepata vi point kwa mbalii hiii ni kwa ajili yako na wengine wapenda Kufanya kwa vitendo.
 
Nimesoma tena na tena

Nakila nikisoma naiwazia Biashara yangu ya Chupi naifanyaje kwa tips hizi naona kama umetumia kiswahili kigumu sana mkuu labda hapa kwenye comments Jaribu kudadavua ili nielewe.

Nimejaribu kuishika ya kupiga kelele na hiyo Ya kuita kampuni inayouza products fulani sasa kwenye chupi itakuaje.

Nikajaribu kuwaza au nikatafute kibali cha matangazo halafu nikodi spika nifunge hapo dukani na Mc Matata kabisa tuanze kazi?

Nitarudi tena naona Maji hayajajaa Bado
 
Sio lazima iwe promo ya biashara yako ya pants mkuu,katika kila biashara tunazofanya lazima kuna biashara ndani ya biashara Mfano mzuri ni mtu mwenye Duka la vinywaji Automatical huyu mtu atauza vinywaji vyote kuanzia maji,juice,soda,bia,nk nk Japo yawezekana ofisi yake vinywaji vingi ni BIA na SODA tu.

lakini kwasababu kaona juice inauliziwa kaamua aweke,kaona maji yanauliziwa kaona aweke pia ila wakati anafungua biashara alifungua kwa lengo la kuuza BIA na SODA tu.

Hapa naongelea zile biashara zinazoingiliana kwenye biashara 1,wewe kokudo unauza underwear dukani kwako,wateja wako 81% ni kina dada,umeshajua kuwa asilimia kubwa ya wateja wako n wadada maana yake biashara yyte inayomuhusu mdada/mwanamke inafaa kuwepo hapo ofisin kwako.

Na assume mimi ndio wewe,nmefungua duka kama lako nahitaji wateja wajue ninauza nini na nimefungua frem mitaa hii,nitakachofanya ni simple tu Naingia Town nanunua hereni zile zinazouzwa set mfano kama hizi hapa chni
23130-cba104.jpg

nachanganya na hivi vidogo dogo vya namna hii hapa chini

rBVaR1seThaATe6yAAK4WzFfido729.jpg
rBVaV12rEh-AeTUpAAHkV_cUT5I471.jpg

Kisha natengeneza meza yangu nzuri sana naiweka ndani ofisini Namwaga mzigo kama wa 100,000 au wa 50,000 inategemea na mfuko wangu uko vipi hiyo siku.

Hizi hereni kwa walio dar ukiingia machimbo kule k.koo wanauza 1500 kiset kizima cha hereni hata 20,vingine 2500 vingine 5000 mpk 15,000 na kuendelea,Sasa mimi ntachanganya za bei rahisi ntaweka nyingiiiiii halafu za bei kubwa ntaziweka chache flani.

Tuchukulie mfano hizi hereni za pcha ya mwisho k set chake umekinunua 3000 k.koo ila kina vihereni vidogo vdogo 30 maana yake kila kihereni umekinunua kwa sh 100, Ukaweka mtu hapo nnje ana mike akawa anapiga kelele kwa mbwembwe kama ZOTE anatangaza "ingia ndani uvae hereni,Mwanamke unatembeaje sikio halina hereni leo kokudo kaamua kuvalisha wateja wake wote hereni,kama huna hereni ingia ndani jichagulie hereni UIPENDAYO BUREEEEE"

ukinunua kitu utapata hereni zaidi ya pair 1 bure,usiponunua pia utachaguliwa hereni bure kabisa uvae,tunawapenda wateja wetu karibu karibu karibu,usipite bila kuingia ndani hata ushangae tu kidogo,Kina kaka karibuni mchagulie ma bebeeee vituz....

Wateja+wapita njia watu wote watakua wanajiuliza huyu anaeweza kugawa hereni mtaa mzima ni nani? je ni kweli au anatutania,akiingia wakwanza ukamvalisha hereni huku ukimwambia next time aje anunue underwear,akitoka hata asiponunua TAARIFA ZAKO ZITAFIKA HUKO AENDAPO.

akiiingia mteja wapili,wa tatu wa nne, wa tano wakitoka wote masikio yana hereni MY BROTHER Taarifa/habari zako zitasambaa zaidi ya moto wa petroli.

Kumbuka hatugawi hereni kwamba tuna hela za kuchezea Point yetu ni utambulisho wa duka letu,point yetu n wajue wapi kuna duka la underwear kila mteja ataekuja hiyo siku hakikisha umemkaribsha next time kununua underwear Bro ki set cha 3000 kina hereni 30 maana yake kuna wateja 15 hao

usiangalie hela unayopoteza leo,Angalia hela utakayoipata kesho.

Bado hujapata kitu broo? basi itabidi nikutaftie TUITION na private Teacher.
 
Sio lazima iwe promo ya biashara yako ya pants mkuu,katika kila biashara tunazofanya lazima kuna biashara ndani ya biashara Mfano mzuri ni mtu mwenye Duka la vinywaji Automatical huyu mtu atauza vinywaji vyote kuanzia maji,juice,soda,bia,nk nk Japo yawezekana ofisi yake vinywaji vingi ni BIA na SODA tu.

lakini kwasababu kaona juice inauliziwa kaamua aweke,kaona maji yanauliziwa kaona aweke pia ila wakati anafungua biashara alifungua kwa lengo la kuuza BIA na SODA tu.

Hapa naongelea zile biashara zinazoingiliana kwenye biashara 1,wewe kokudo unauza underwear dukani kwako,wateja wako 81% ni kina dada,umeshajua kuwa asilimia kubwa ya wateja wako n wadada maana yake biashara yyte inayomuhusu mdada/mwanamke inafaa kuwepo hapo ofisin kwako.

Na assume mimi ndio wewe,nmefungua duka kama lako nahitaji wateja wajue ninauza nini na nimefungua frem mitaa hii,nitakachofanya ni simple tu Naingia Town nanunua hereni zile zinazouzwa set mfano kama hizi hapa chniView attachment 1510060

nachanganya na hivi vidogo dogo vya namna hii hapa chini

View attachment 1510061View attachment 1510062

Kisha natengeneza meza yangu nzuri sana naiweka ndani ofisini Namwaga mzigo kama wa 100,000 au wa 50,000 inategemea na mfuko wangu uko vipi hiyo siku.

Hizi hereni kwa walio dar ukiingia machimbo kule k.koo wanauza 1500 kiset kizima cha hereni hata 20,vingine 2500 vingine 5000 mpk 15,000 na kuendelea,Sasa mimi ntachanganya za bei rahisi ntaweka nyingiiiiii halafu za bei kubwa ntaziweka chache flani.

Tuchukulie mfano hizi hereni za pcha ya mwisho k set chake umekinunua 3000 k.koo ila kina vihereni vidogo vdogo 30 maana yake kila kihereni umekinunua kwa sh 100, Ukaweka mtu hapo nnje ana mike akawa anapiga kelele kwa mbwembwe kama ZOTE anatangaza "ingia ndani uvae hereni,Mwanamke unatembeaje sikio halina hereni leo kokudo kaamua kuvalisha wateja wake wote hereni,kama huna hereni ingia ndani jichagulie hereni UIPENDAYO BUREEEEE"

ukinunua kitu utapata hereni zaidi ya pair 1 bure,usiponunua pia utachaguliwa hereni bure kabisa uvae,tunawapenda wateja wetu karibu karibu karibu,usipite bila kuingia ndani hata ushangae tu kidogo,Kina kaka karibuni mchagulie ma bebeeee vituz....

Wateja+wapita njia watu wote watakua wanajiuliza huyu anaeweza kugawa hereni mtaa mzima ni nani? je ni kweli au anatutania,akiingia wakwanza ukamvalisha hereni huku ukimwambia next time aje anunue underwear,akitoka hata asiponunua TAARIFA ZAKO ZITAFIKA HUKO AENDAPO.

akiiingia mteja wapili,wa tatu wa nne, wa tano wakitoka wote masikio yana hereni MY BROTHER Taarifa/habari zako zitasambaa zaidi ya moto wa petroli.

Kumbuka hatugawi hereni kwamba tuna hela za kuchezea Point yetu ni utambulisho wa duka letu,point yetu n wajue wapi kuna duka la underwear kila mteja ataekuja hiyo siku hakikisha umemkaribsha next time kununua underwear Bro ki set cha 3000 kina hereni 30 maana yake kuna wateja 15 hao

usiangalie hela unayopoteza leo,Angalia hela utakayoipata kesho.

Bado hujapata kitu broo? basi itabidi nikutaftie TUITION na private Teacher.
Hahaha Duh Unaona sasa hayo madini hukuyaandika kwenye Mada thanks mkuu Nimekupata
 
Back
Top Bottom