Unajisikiaje unapoonekana mdogo kuliko umri wako?

hermanthegreat

JF-Expert Member
Mar 2, 2021
853
2,037
habari wanajf,

Hili Jambo la kuonekana mdogo kuliko umri wangu limekuwa Jambo ambalo naona kwangu ni Kama laana au kama baraka Tena maana nikimwambia mtu umri wangu akanitazama na Mimi haamini.

Naonekana mdogo miaka kumi nyuma kuliko umri wangu halisi na hii imekuwa na madhara haya kwangu

👉 Kushindwa kuchukuliwa sirias na watu.

👉 Kushindwa ku date na baadhi ya wanawake kwasababu wanaoona Kama wanadate kijana mdogo wa shule.,

👉 Kutokusikilizwa , na kupuuzwa.

👉 Kukosa baadhi ya nafasi za kazi au uongozi sehemu Fulani Kwani watu wanakuuona Kama wewe ni mdogo Sana

👉 Inakupasa uwe ni mtu wa kujielezea Sana hata Kama ni interview basi unataja umri wako hata Kama hujaulizwa ili kuwa ondoa hofu. , hata Kama unatongoza msichana unakuwa unatamani umuonyeshe angalau cheti chako Cha kuzaliwa aamini.

Unaeza tamani uwe hata na ndevu tu lakini wapi!

Hili Jambo naona Kama litanichelewesha kufika mbali kwani hata kukaa na watu wa Rika lako unaonekana Kama hupaswi kuwa hapo hivyo unajikuta umezungukwa na vijana wadogo, basi tu.

Hii hali inaweza kuwa ni nzuri kwa wanawake lakini kwa mwanaume inampunguzia heshima.

Kama Kuna mtu anapitia Maisha Kama haya naomba tusaidiane jinsi ya kukabiliana na hali hii.
 
habari wanajf,

Hili Jambo la kuonekana mdogo kuliko umri wangu limekuwa Jambo ambalo naona kwangu ni Kama laana au kama baraka Tena maana nikimwambia mtu umri wangu akanitazama na Mimi haamini.

Naonekana mdogo miaka kumi nyuma kuliko umri wangu halisi na hii imekuwa na madhara haya kwangu

👉Kushindwa kuchukuliwa sirias na watu.

👉Kushindwa ku date na baadhi ya wanawake kwasababu wanaoona Kama wanadate kijana mdogo wa shule.,

👉Kutokusikilizwa , na kupuuzwa.

👉Kukosa baadhi ya nafasi za kazi au uongozi sehemu Fulani Kwani watu wanakuuona Kama wewe ni mdogo Sana

👉inakupasa uwe ni mtu wa kujielezea Sana hata Kama ni interview basi unataja umri wako hata Kama hujaulizwa ili kuwa ondoa hofu. , hata Kama unatongoza msichana unakuwa unatamani umuonyeshe angalau cheti chako Cha kuzaliwa aamini.

Unaeza tamani uwe hata na ndevu tu lakini wapi!

hili Jambo naona Kama litanichelewesha kufika mbali kwani hata kukaa na watu wa Rika lako unaonekana Kama hupaswi kuwa hapo hivyo unajikuta umezungukwa na vijana wadogo , basi tu.

Hii hali inaweza kuwa ni nzuri kwa wanawake lakini kwa mwanaume inampunguzia heshima.

Kama Kuna mtu anapitia Maisha Kama haya naomba tusaidiane jinsi ya kukabiliana na hali hii.
Wewe ni mimi Kabsa aisee sem tu mim ni mrefu hcho nd kinasaidia,

ila Sura yangu na Umri wangu nkikutajia ni Mbingu na Ardhi.
 
Umenikumbusha Kuna rafik yangu alikuwaga anapenda ukubwa hatari, nakumbuka tupo darasa la pili alikuwaga anapitia saluni wakat wa kuludi shule alafu anaokota nywele walizonyolewa watu then anachukua gundi(gundi pori au minyara) na kubandika sehemu za Siri😂 alafu et anaanza kutulingishia kuwa yeye ni mtu mzima🤣 tuwe tunamwamkia,, mpka Leo jamaa nikionana Naye Huwa nacheka san.
 
Umenikumbusha kuna siku nimekutana na ndugu ambaye hatukuwahi kuonana akaniambia "za saizi". Wakubwa wacha wamshukie kama mwewe msalimie vizuri huyu mkubwa sana kwako.

Mimi ni mkubwa halafu napenda ukubwa sana. Sema mwili na sura vinanikataa. Ndio hivyo kupambana na hali tu
 
Back
Top Bottom