Unajisikiaje ukikutana na Rafiki zako mliosoma wote kipindi hicho, wako mbali sana kimaisha

Acha tu maisha hayana formula ni Afande ila kiumri very young,kila mtu na bahati yake hapa duniani.
Mkuu ilo jambo lilinipa stress tukaenda na wenzangu pale ngome tukaishia kufukuzwa.
Hiko hivi tulivyoenda kwa mujibu wa sheria walifanya usahili kambi tatu, sisi hawakufikia kambi yetu.

Tulivyoenda chuo wakapigiwa simu wakaacha chuo wakarudi jeshini wengine walipelekwa navy, urusi egpty n.k wapo mbali kiukweli na wanamiliki magari mazuri tu.
Na wengi tulipiga nao PCB matokeo yalikua yanafanana. Mimi nimeajiriwa vijijini huku.
Kuna watu wana bahati sana
 
Lazima usjisikie vibaya lakini mgawaji ni Mungu na hugawa kwa kadri inavyompendeza mwenyewe!
 
Basi mwanangu ndo alikuwa na bahati hio
 
Mim ni mmoja ya watu ambao marafiki zao zaid ya 80% wamepiga atua kubwa sana kimaisha, sio marafiki niliokuwa nao yaan childhood friends, Primary, secondary na chuo. most of them ni matajiri na bado ni machalii kabisa, maisha aya sio poa
wengine adi wanamiliki magari mawili mawili na minengo ya kibabe kabisa na biashara kubwa. life's not fair aisee
 
Maneno ya mwisho yenye herufi kubwa, ukisoma Biblia ya kiingereza ni tofauti kidogo. Huo mstari unasema, "Bad luck happens to everyone"
 
Kikubwa tusikate tamaa,japo I know what you feel wazungu wanasema life is a journey not a competition.
Amini ipo siku itafika zamu yako endelea kuwaombea mema na wewe kadri unavowaombea utapata baraka zaidi.
 
Nimewahi kufanya kazi taasisi moja ya serikali ya uchumi, Bro tuliyepewa ofisi moja mimi na yeye alikuwa na hasira kinoma rafiki yake waliyesoma darasa moja chuo kikuu cha Dar es Salaam (2001-04, 2004-06) alikuwa katibu mkuu hazina akiwa na miaka 38. Akaamua arudi kufundisha chuo kikuu.
 
Huu mstari kila ninapousoma unanikumbusha kisa cha mwanariadha mkongwe wa Tanzania John Stephen Akwari kilichotokea mwaka 1968 Mpaka akapachikwa jina 'The Champion who finished last'

Nawasilisha..
 
The higher the risk the higher the return...

Mi naamini Mungu alivotuumba hapa duniani ameshagawa baraka kwa kila mtu equally...

Na the fact tumepewa akili na uwezo wa kufanya maamuzi, aisee kama unakutana na mwenzako kakuzidi maisha juu tu kwamba jamaa ni hardworker kuliko wewe..

So always tupambane na maisha wandugu, Mungu ameshatugawia baraka ya uhai, kutafuta mafanikio hiyo ni jitihada binafsi
 
Nilikutana na mwamangu tulipiga nae kitabu seko tulikaa sehem tunakula mtungi story za apa na pale mwamba ana mijengo mbweni goba madale kijitonyama na kimara ni mijengo ya grade A na anapush SUV mbbili za kibabe alafu kipind tunakula story mwamba anahis mimi pia mtamu anaomba investment advices kwangu maana yeye kaajiliwa mimi nmejiajiri anaona kama nina bright future zaid yake kipindi hicho nadaiwa kodi ya nyumba kodi ya ofis na ada ya dogo mambo ya january hayo ilibaki kidogo nilie njaa ila nikakaza kulinda brand yangu sikutoa mlio wa njaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…