Usichofahamu ni kwamba rafiki zako wa karibu ndio wengi hutembea na mkeo au mpenzi wako

Ligaba

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,045
2,821
Habari za mwisho wa mwaka.

Bandugu huu si uchonganishi ila ni dhamira tu ya kukufanya uishi kwa akili na watu wanaokuzunguka na hasa marafiki. Kwa utafiti niliofanya kulingana na matukio nilikutana nayo nathubutu kusema katika mahusiano yako rafiki yako wa karibu ni mtu wa kwanza unaepaswa kuishi nae kwa tahadhali.

Katika pitapita yangu nimegundua hali hii ipo kwa kiwango kikubwa. Janga ni kubwa zaidi kwa jinsia ya kike. Hivyo nitoe nasaha zangu kwa wanawake, ukiwa na marafiki watano tambua angalau kuna mmoja kama si wawili ambao wako radhi kabisa siku ambayo shemeji yao atakapojichetua na kuwatamkia basi wao hawatakuwa na kipingamizi.

Nikushauri uchukue tahadhari sana kwa upande wa wanaume ikiwa rafiki yako amekuzidi kipato kwa mbali sana, hata yule mwenye muonekano wa kiume halisi kukuzidi wewe, mwogope hata rafiki yako umpelekeae kesi nyingi za usuruhishi juu ya mahusiano yako. Natamani ushuhuda huu niutoe hapa lakini kimaadili haipendezi.

Kwa jinsi ya kike nikushauri sana epuka kuwaadithia shosti zako uhodari wa mtu wako kwao. Tambua tu wengine wamekutana na bamia kuanzia walipo barehe mpaka unampomtambulisha wapi alifuate tango, bila shaka watalifuata. Kingine epuka kuwaadithia namna mtu wako anavyokupenda na kukupa mshiko wa nguvu, mitoko ya nguvu na kila jambo zuri, tambua tu kuna watu hawajawahi kuhongwa hata laki katika maisha yao yote, sembuse uwaambie ulihongwa million na kuendelea?

Wakati fulani nilikuwa na mpenzi wangu, nae alitambulisha kwa rafiki yake. Kosa lake kubwa ni kumtangazia mwenzake vile anavyonipenda. Aisee nilijikuta nimepigwa mitego mpaka nilivunja amri ya sita na shemeji yangu. Nilipomuuliza kulikoni akasema, rafiki alimwambia kitu na yeye alitaka kuthibitisha. Hakuniacha shemeji huu mwaka wa kumi, ameolewa na gemu ananipa Mungu mwema.

Kuna kipindi nilitrack simu ya wife, nilichoshuhudia inatia hasira yaani rafiki yangu, na mfanyakazi mwenzangu yuko busy kakomalia kumtaka mke wangu, mpaka hapo nikaanza kutoa thamani ya marafiki wengi ni washenzi hujisikia furaha sana wakimvua nguo mpenzi wako au mkeo wabaki wanakudharau.

Hapa mtaani kuna wanaume mtu na rafikiye, uwezi amini mwanamke mmoja wa hawa marafiki kazaa mtoto copy na paste ya yule rafiki yake. Watu wote wanajua huyu mtoto wa fulani ila kitanda hakina hatia.

Cha msingi angalia namna ya kuishi na marafiki wasije kuleta maafa katika mahusiano yako.
 

Rafiki Ni rafiki tu usimchanganye na mahusiano yako, na usigombane na mpenzi wako au mkeo ukamleta rafiki yako kusuluhisha kesi trust me hapo Kama sio mkeo au mpenzi wako kupusuliwa itakuwa habari anazo mpiga picha.
Ni kweli kabisa wengi hawalifahamu hili
 
Ulikula rafiki wa mpenzi wako, nawewe mkeo ataliwa na rafiki yako, hapo hakuna kulia lia wewe tulia tu malipo no hapa hapa pole ila mkanye mkeo aache mazoea na rafikio
Ni ukweli unaoumiza
 
Usijali vyovyote uwavyo maisha yataendelea
Maisha kuendelea yataendelea wala usijali, unajua ukiwa single umachezea wake za watu au waume za watu sasa nawe ingia halafu unakuwa hata chembe ya kumbukumbu kama uliyafanya, yanakuja mule mule
 
Maisha kuendelea yataendelea wala usijali, unajua ukiwa single umachezea wake za watu au waume za watu sasa nawe ingia halafu unakuwa hata chembe ya kumbukumbu kama uliyafanya, yanakuja mule mule
Ni kweli mkuu ila yote hayo ndio yanayofanya Dunia izunguke
 
Back
Top Bottom