Unajisikiaje ukikutana na Rafiki zako mliosoma wote kipindi hicho, wako mbali sana kimaisha

Top gun maverick

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
1,944
2,454
Habari za Jumapili wanajukwaa,Pia poleni na majukumu ya kutafuta mkate wa kila siku.Niende kwenye mada husika hapo juu hivi huwa unajisikiaje hasa pale unapokutana na rafiki zako mliosoma wote kipindi hicho wako mbali sana kimaisha kuliko wewe?

Kwa Upande wangu hii imenikuta wakati natoka Kanisani na stress nyingi zimejaa kwenye kichwa ghafla napigiwa honi na Gari nyeusi aina ya BMW X5 nikashituka kuona linapaki pembeni na Mtu anashuka ananiita jina langu la Ukoo! Nikamkubuka ni rafiki yangu tuliyesoma wote.

Advance Level ila yeye Alibahatika baada ya kutoka mujibu wa sheria alijiunga na Taasisi nyeti, hapa nchini kwa sasa ni Afisa mkubwa.

Kwa upande wangu akaniuliza "ndugu kwa sasa unapiga mishe gani?", ikabidi niwe muwazi nikamwambia kwangu bado mambo hayajakaa sawa japo,nilijisikia Aibu kidogo yaani niliyekuwa nampita class,namfundisha kila siku,tunakesha wote kwenye madesa kashanizidi ilihali mimi bado sioni mwanga.

Nikajisemea Moyoni "basi mpaka pale zamu yangu itakapo fika niendele kuwapigia wenzangu makofi kwa tabasamu na upendo."

Nashukuru akanipa lift mpaka home maana nilikuwa sijawahi panda hizi BMW aisee kuna utofauti mkubwa sana na hizi IST. Naishia hapo wakuu Mungu atubariki sote Jumapili njema.
 
Habari za jumapili wanajukwaa,Pia poleni na majukumu ya kutafuta mkate wa kila siku.Niende kwenye mada husika hapo juu hivi huwa unajisikiaje hasa pale unapokutana na rafiki zako mliosoma wote kipindi hicho wako mbali sana kimaisha kuliko wewe?

Kwa Upande wangu hii imenikuta wakati natoka Kanisani na stress nyingi zimejaa kwenye kichwa ghafla napigiwa honi na Gari nyeusi aina ya BMW X5 nikashituka kuona linapaki pembeni na Mtu anashuka ananiita jina langu la Ukoo! Nikamkubuka ni rafiki yangu tuliyesoma wote.
Advance Level ila yeye Alibahatika baada ya kutoka mujibu wa sheria alijiunga na Taasisi nyeti, hapa nchini kwa sasa ni Afisa mkubwa.

Kwa upande wangu akaniuliza "ndugu kwa sasa unapiga mishe gani?", ikabidi niwe muwazi nikamwambia kwangu bado mambo hayajakaa sawa japo,nilijisikia Aibu kidogo yaani niliyekuwa nampita class,namfundisha kila siku,tunakesha wote kwenye madesa kashanizidi ilihali mimi bado sioni mwanga.

Nikajisemea Moyoni "basi mpaka pale zamu yangu itakapo fika niendele kuwapigia wenzangu makofi kwa tabasamu na upendo."
Nashukuru akanipa lift mpaka home maana nilikuwa sijawahi panda hizi BMW aisee kuna utofauti mkubwa sana na hizi IST. Naishia hapo wakuu Mungu atubariki sote Jumapili njema.

Mhu 9:11 SUV​

Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; LAKINI WAKATI NA BAHATI HUWAPATA WOTE.
 
Umenikumbusha nilikutana na jamaa angu flani yupo ndan ya ndinga, ni nlikuwa kwa mguu akashuka kunipa hi, bas akajidai na mbwembwe nyingi mara atoe iphone then ajidai anaongea na watu wamtumie milion ngapi, nami nikatoa simu yangu daa alivyoiona alishtuka akajua mi nami kumbe nimo, bas nilitoa walet ninunue kitu flani, alivyoona njurugu zilivyojaa ,aliaga fasta akapanda gar akakimbia.
Mafanikio ni swala la muda na bahat pia, mtu yeyote anaweza kuwa yeyote kwa muda wowote.
Ishi kwa Amani na watu wote. Ebr 12:14
 
Jiamini mdogo wangu.

Mimi nina ma collegemates wangu ambao kwa sasa ni wakurugenzi huko kwenye mashirika ya UN, na tukionana wala hatuviambiani.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom