Unajifunza nini ukiitizama picha hii?

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,264
9,715
Ndugu zangu Watanzania,

Ukiwa kama mwanadamu na binadamu ambaye umepata neema ya Mwenyezi Mungu ya kuwa hai mpaka siku ya leo unajifunza nini na unapata somo lipi ukiitizama picha hii? Nini kinakuja katika akili yako? Nini unapaswa kufanya kama mwanadamu kila uamkapo asubuhi?

Kwangu mimi Mwashambwa Lucas napata funzo na somo la kuwa Kifo ni Fumbo ,aijuaye kesho ya mtu ni Mungu pekee .siku za kuishi mwanadamu hapa Duniani zipo mikononi mwa Mwenyezi Mungu pekee, na siyo kwa ujanja wa mwanadamu wala mipango ya mwanadamu katika kuishi hapa Duniani.

Najifunza kuwa kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.kikubwa ukipata nafasi ya kuishi basi jitahidi kumcha Mungu, kuishi maisha ya kumpendeza Mungu, kutenda mema,kugusa maisha ya watu,kuacha alama katika maisha ya watu,kuwatendea watu wema.kujuwa kuwa Duniani sisi sote ni wapitaji tu na siyo mahali pa kudumu. Hivyo tunapaswa kama wanadamu kufahamu ya kuwa kama ilivyokuwa siku yetu ya kuzaliwa basi pia kuna saa yetu na siku yetu ya kufa na kuondoka hapa Duniani yaja mbele yetu kitambo kidogo.hivyo mjue sana Mungu ili uwe na amani hata saa yako ya kuondoka hapa Duniani itakapowadia.

Najifunza na naendelea kujifunza kuwa Mungu huvuna popote pale na wakati wowote ule pasipo mipaka wala kizuizi cha aina yoyote ile,kwa sababu sisi sote wanadamu ni sawa na tupo sawa mbele ya macho yake.

Mungu awalaze mahali pema peponi viongozi wetu hawa watatu waliotangulia mbele za haki. lakini pia aendelee kumjalia maisha marefu yenye heri na baraka Mheshimiwa Rais wetu mstaafu mzee Dr Jakaya Mrisho Kikwete maana ni muhimu sana Taifa kuwa na wazee na viongozi wastaafu katika kutoa mawazo na ushauri kwa uongozi unaokuwepo madarakani kwa wakati huo hasa katika nyakati ngumu zinazohitaji busara na uzoefu wa wazee walipitia katika uongozi . Kusudi la kuumbwa kwao walishalimaliza hapa Duniani na walipoishia ndipo ilikuwa mipango ya Mungu kwa wao kutufikisha hapo kama Taifa katika ulimwengu wa kiroho.

Hivyo kila kiongozi wetu aliye hai na aliyepewa nafasi na neema ya kuwahudumia na kuwatumikia watanzania anapaswa kujiuliza kuwa ni vipi na kwa namna gani amegusa maisha ya watanzania. Ni kipi atakumbukwa na watanzania pale atakapomaliza utumishi wake wa umma. Ni vipi na kwa namna ipi hadithi yake itasimuliwa na vinywa vya walio hai. Uwepo wake katika nafasi fulani ya uongozi ni kwa kiasi gani umeleta tabasamu ,furaha na matumaini katika mioyo ya watanzania. Maisha yake hapa Duniani yamebadilisha maisha ya watu wangapi na kuwapa matumaini. Ni vipi umewatendea watu haki. Ni vipi mikono yako imegusa maisha ya watu.

Kikubwa ni kutambua kuwa hakuna mwanadamu aliye kamilika chini ya jua.kila mtu ana udhaifu wake,makosa yake,upungufu wake kama mwanadamu. Hivyo kama wanadamu hatuna budi kusameheana, kusaidiana,Kuombeana heri na kumuomba Mungu atusamehe makosa yetu,atuongoze katika njia zetu na maamuzi yetu na kutufanya kuwa viumbe vipya katika matendo yetu yatakayo leta na kuchochea amani na upendo miongoni mwetu.

Hata mimi niliyeandika hapa nami ni mwanadamu ambaye sijakamilika kama alivyo kamilika Mungu,ndio maana kila siku kabla ya kulala namwomba Mungu anisamehe makosa yangu niliyo yatenda iwe kwa mawazo ,kwa maneno na hata matendo yangu.hivyo tusameheane na kuhurumiana.

Kipekee kabisa namuombea kwa dhati ya moyo wangu maisha marefu yenye heri ,amani na furaha Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan,Mungu aendelee kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania,amlinde , kumpigania na kumtetea wakati wote.mkono wa Mungu na uso wake uwe pamoja na Rais wetu.amtangulie mahali popote aendapo.Mungu ndiye awe mlinzi wake,dereva wake na daktari wake.Mungu akawe ndani ya Moyo wa kila mtu amhudumiaye Rais wetu.chochote kifanyikacho kwa Rais wetu kikawe na kibali na mkono wa Mungu ndani yake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
IMG-20240303-WA0057.jpg
 
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.View attachment 2925123
Screenshot_2024-02-29-07-56-10-583_com.android.chrome~2.jpg
 
We jitu liongo kweli kweli, 1980 ulikuwepo?
Lazima ufahamu jukwaa hili lina watu wazima kukuzidi wewe na mimatusi yako unayotukana ukishavuta mibangi yako.sasa huoni ulivyo mtoto kiakili .sasa unaanzaje kushangaa juzi tu hapo? Kweli wewe ni hamnazo kabisa. Hivi hujuwi jukwaa hili lina member wakongwe kabisa.embu niambie mfano profesa Anna Tibaijuka ni wa mwaka gani? Vipi prof Issa shivji? Vipi akina Dr Slaa?
 
Umenianza, nikianza usianze kulialia hapa, profesa Anna Tibaijuka, prof Issa shivji na Dr Slaa mara yao ya mwisho kuchat hapa ni lini?
 
Sijasoma mengine zaidi ya heading, ila najifunza kuwa Msoga soon nae tutamuomboleza kwa siku 7.
 
Back
Top Bottom