Unaikumbuka Juni Kumi na Tano???? Soma hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unaikumbuka Juni Kumi na Tano???? Soma hapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bibikuku, Jun 15, 2011.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Jamani leo kwa wale wazalendo wa zamani ilikuwa siku maalum ijulikanayo kama Juni Kumi na Tano, yaani siku ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na vyuo vya elimu kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa yaani JKT. Kule kulikuwa ni sehemu muhimu sana ya kukuza uzalendo kwa vijana na kujifunza maisha mapya bila kujali kuwa babako ni kigogo au tajiri! Kwa wale waliofanikiwa kupitia JKT watukumbushe ni nini kikubwa sana anachokikumbuka alipokuwa depo la JKT kama Mgulani, Ruvu, Orjoro, Buhemba, Bulombola, Masange na kwingineko??? Na hasa siku ya kwanza baada ya kuripoti camp!
   
 2. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Na wote waliopita huko ndio leo hii wanaitafuna hii nchi kwa kwemda mbele!!!!
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Nasikia kuna utaratibu wa kurudisha mujibu wa sheria. Shimbo kashupaa kuwa ndio maana hakuna maadili kwa vijana. Nadhani sio kweli maana katika idara zinazokula rushwa kwa wingi police inaongoza, na wao ndio wanapata mafunzo ya kweli katika training yao. Mafisadi wote CCM na kwingineko wote wamepitia jeshini. Hivyo acha habari ya JKT, fedha hazipo za kupoteza
   
 4. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Duhh umenikumbusha suluba niliyoipata siku ya kwanza niliporipot kambini. Ilikuwa ni tarehe kama ya leo mwaka 1987 baada ya kumaliza mtihani wa form six hapo Pugu high school. Ilikuwa ni saa tisa jioni nilipokuwa getini, yaani main gate ya kambi ya MSANGE JKT huko Tabora. Nikiwa na begi langu begani nilimkuta Afande mmoja wa kike alokuwa na cheo cha Sajenti, Afande huyu alikuwa ni bonge la mtu, alojaaliwa makalio ya nguvu na mwenye rangi ya maji ya kunde. Kutokana na Rafudhi yake niligundua kuwa alikuwa ni MNYATURU toka Singida. Basi aliponiona tu umbali wa mita kama 50 hivi toka Getini, aliniambia nianze kuruka kichurachura huku begi nikilinyanyua juu. Baada ya kufika hapo getini alinishika shingoni kwa chini ya kisogo na kuniambia kuwa ndani ya mwezi mmoja atahakikisha kuwa nundu iliyopo hapo shingoni itakuwa imeisha. Na nikamjibu kuwa afande hii utaiacha kama ilivyo, weee kusema hivyo tu alinikata mtama na nikajikuta niko chini. Akaninyanyua juu kwa kunishika kwenye mkanda wa suruali na kuwaita MP wawili waje na akawaamrisha wanitwishe gunia la mahindi toka kwenye Lori (lililokuwa limepaki karibu na stoo likitoka shambani) ili niingize ndani. Basi nilipotwishwa tu nikaanguka nalo hadi chini. Basi sikuisahau siku hiyo na sikumsahau huyo Afande, kwani ilinifanya siku namaliza mafunzo hapo nilimtafuta na kumuaga nikimwambia afande vipi, si unaona shingo yangu iko palepale????. Asante mdau kunikumbusha ya JKT, natamani kama mafunzo haya yatarudi tena kama zamani tena kwa muda wa mwaka mmoja kama sisi tulivyokaa. Nawakumbuka maafande kama Afande Chacha, Afande Mwiru, Afande Muhogo!!!!!!!!!
   
 5. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du mimi nakumbuka JKT Makutupora Kombania B' kwa afande Chacha 1987 Operationi Nidhamu siku kama ya leo Juni 15 tulipanda KAUDO na saa 2.00 usiku tukaripoti gatini du jamani wiki la kwanza tu wale mabint kuanzia Kombania A-C mapaja yalibadilika rangi na hapo ndipo ulipoonekana Uzalendo, hakuna cha Queen au Selule wote Nidhamu ilionekana na hata wakienda vyuo vyovyote usingesikia migomo.
  Yote hii ninkwa wale walioifuta JKT kwani sasa hakuna uzalendo tena watoto, viongozi wote wanavaa mavazi yenye bendera za USA nk kushabikia maandamano na migomo

  JKT IRUDISHWE
   
 6. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yaani nimecheka kupita maelezo mkuu inaonyesha jinsi gani ulivyokula suluba na huwezi kusahau kamwe hiyo siku. Unakumbuka mchezo wa kukatwa bogi lakini???? Unaikumbuka kambi ya kule Igambilo ambako kulikuwa kunalimwa mchicha karibu na chanzo cha maji cha mto Igombe?? Wakati ule ukikatwa bogi kwenda Igambilo unaona kama ahueni kuliko kubaki masange. Big up mkuu sijui nani kalifuta jeshi JKT letu tumchape bakora!!!!!!!!!!!
   
Loading...