Nakumbuka ilikua ni Primary School...shule yao ilifanyiwa upgrade na kuwa Secondary School wanafunzi ikabidi wagawanywe kwenye mashule ya karibu sasa mojawapo ya group likatua shuleni kwetu yeye akiwemo ndani...Nakumbuka ilikua ni mwezi wa saba baada ya likizo ya May-June Darasa la nne nilichelewa kufika shule kama wiki moja.Ile kufika mwalimu wa darasa akachagua class representatives(monitor&Monitress) wapya, mimi na yeye tuliibuka kidedea tukifuatiwa na wasaidizi wetu wawili...Basi alikua mrembo kweli kweli na kwao walijiweza sana hata uniform na viatu vyake vilikua tofauti kabisa na wanafunzi wengine.Hatukuwahi kuongea chochote mpaka tunamaliza darasa la saba zaidi ya kukusanya daftari na kupeleka stuff room.Siku tunamaliza paper ya std VII akanifuata akasema Rural Swagga twende nikakununulie soda coz hatutaonana tena nilifurahi sanaa..na siku hiyo nikamsindikiza mpaka kwao mm nakaa MAJENGO yeye anaishi KCMC nilifurahi sana na Ndio ukawa mwisho wa kuonana kwetu mpaka mwaka juzi february 2011 nikiwa ndani ya South African Airways (Dar-Joz) flight no SA 184(nakumbuka coz ndio nilivyomsevu kwa phonebook yangu) Sit no sikumbuki Economy class... yeye pamoja na mwenzake ndio walikua wahudumu mule ndani...Nikamwita flani akajibu flani basi msitake kujua kilichotokea baadae...tumebahatika kupata mtoto mmoja wa kike na yeye ameacha ile kazi sasa anafanya kazi Dar awe karibu na Monitor wake na Mungu akijaalia mwaka huu mwezi wa 5 ni cherekochereko...I LOVE U J...najua utasoma huu uzi mama.