Mwanamke anakunywa pombe analewa yaani mpaka akiongea anaburuza maneno hata aeleweki, kwa kweli hata kama mzurije unajishusha kabisa.
Kunywa kidogo basi ukiona inatosha aanza kunywa maji. Yaani imefikia wakati eti mwanamke anamarafiki wa kiume wa kwenda bar kunywa pombe na huko bar anashindana na wanaume kunywa, mnaweza kusema mbona wanaume wanalewa.
Ni mwanaume na kamwe hawezi kua mwanamke. Hebu badilika basi mnajizeesha, unakutana na mdada utasema ana redeyes kumbe ni pombe ndo zimemwaribu.
Hata ngozi nayo inakakamaa, wakati mwingine mnazingizia vipodozi havijawapenda kumbe ni pombe.
Samahanini sana kama mtachukia.