Unafikiri nini kilimpata baadaye Mchungaji huyu?

Kashaija

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
255
58
Mgonjwa mmoja mahututi alikuwa
hawezi kuongea na kuwekewa oxgen.
Akawa anaombewa na Mchungaji.
Akiwa anaombewa, yule mgonjwa
akachukua kalamu na karatasi,

Akaandika na akampa yule Mchungaji. Ambaye
badala ya kuisoma ile karatasi, akaitia kwenye
mfuko wa joho na kuendelea na maombi hadi
yule mgonjwa, AKAKATA ROHO.
Mchungaji hakuisoma ile karatasi akijua kua
ni wosia wa marehemu. Akasubiri baada ya
mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema;

"KUNA KITU NILIPEWA NA MAREHEMU SIKU
NILIYOKUA NAMUOMBEA"

Akampa mmoja wa wanandugu akisome.
Haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa na
yule mgonjwa:

"UMEKANYAGA WAYA WA OXYGEN,
NAKOSA HEWA".
 
Nadhani alijutia sana kwa kutambua alikuwa amesababisha kifo cha mgonjwa yule. Tukio hili halitofautiani sana na tabia zetu mbaya ya kuto-take action pale unapobipiwa kwenye simu au kusoma sms mpaka baadae. Ilim-cost jamaa moja pale alipopigiwa simu na mkwewe aliyekuwa dukani na yeye akaamua aende badala ya kupokea. Alipofika dukani akawekwa chini ya ulinzi na majambazi na kumpukutisha kila alichonacho pamoja na pesa yote iliyokuwepo dukani. Simu ile aliyopigiwa na mkewe aliyejificha mahali baada ya kuvamiwa ilikuwa ya kumtaarifu tukio lile. Kama angepokea angeweza kuokoa mali zake. Wana-JF tuwe tunasoma ujumbe au kupokea simu immediately ili kuepuka similar case kama hizi.
 
...Tatizo linakuwa kujua kati ya yule anayeku-beep kwa emmergency na yule ambaye akiku-beep ukimpigia anakuambia 'Ah, nilikuwa nakusalimia tu , mambo vipi huko?!" Na hawa ndio wengi. :mad:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom