Jamani tuwe tunasoma ujumbe mara tuupatapo!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani tuwe tunasoma ujumbe mara tuupatapo!!!!!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Lady N, Jul 20, 2010.

 1. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mchungaji akiwa katika pitapita zake za kuombea katika wodi za hospitali fulani, akakuta kuna Mgonjwa aliekuwa hawezi kuongea japo alikuwa na fahamu na aliwekewa oxgen.

  WAKATI AKIOMBEWA, yule mgonjwa akachukua kalamu na karatasi, Akaandika haraka haraka na akampa yule Mchungaji ambaye badala ya kuisoma ile karatasi, akaitia kwenye mfuko wa joho na kuendelea na maombi hadi yule mgonjwa, AKAKATA ROHO.

  Mchungaji hakuisoma ile karatasi akijua kua ni wosia wa marehemu. Akasubiri baada ya mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema; "KUNA KITU NILIPEWA NA MAREHEMU SIKU NILIYOKUA NAMUOMBEA" Akampa mmoja wa wanandugu akisome.

  Haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa na yule mgonjwa: "UMEKANYAGA WAYA WA OXYGEN, NAKOSA HEWA"
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  ha ha ha hatari na si salama
   
Loading...