Unafiki wa viongozi wa chama cha magamba huko Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafiki wa viongozi wa chama cha magamba huko Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MAKAPILE, Mar 30, 2012.

 1. MAKAPILE

  MAKAPILE Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutokana na habari za hapo asubuhi inasadikika kwamba waziri aliyejiuzulu kwa kashifa za ufisadi hatimae atajitokeza hazarani kwa kumnadi mkwe wake Sioi akiambatana na Nape ambaye anajipambanua kuwa yeye ni mpambanaji wa ufisadi; Kutokana na kauli zake za mara kwa mara akisema watawafukuza mafisadi, ikiwa ni kinyume kabisa na maneno yake kwa kuongozana na mh Lowasa.

  Hivyo anaonesha dhahiri kwamba anachotenda si sahihi kabisa kwa jamii ya watanzania na ninamfananisha mh Nape kama wale wakristo ambao katika bibilia ambao wanamkiri kristo mdomoni mwao lakini miyoni mwao hayupo, watu hawa ni wanafiki sana na ni watu hatari sana kwa jamii yetu.

  Pia kunamnafiki mwingine mh Ole Sendeka kwa kuwaongopea wanaarumeru na jamii zima ya Tanzania kwa kwenda kumnadi Sioi huku akijua kawekwa na MAFISADI,pia haitoshi uchaguzi wa kura za maoni uliendeshwa kwa rushwa.

  Pia ningependa kusema hata waandishi wa habari hawaitendei haki jamii ya kitanzania kwa kuficha ukweli.Tungependa kuona kituo fulania cha TV au gazeti kwa kuwauliza hao wanaojiita wapambanaji Ole Sendeka na Nape maswali mbalimbali ikiwamo kwanini wanajiita wapambanaji ilihali wanakuwa wanafiki kwa kuongozana na mafisadi? Pia tuwauleza walikua wapi katika miaka 50 ya uhuru katika kutatua matatizo ya wanaarumeru ikiwamo swala la ardhi na maji?
   
 2. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Nakiri sijawahi kumsikia Nape akitamka waziwazi Lowasa ni Fisadi, Lakini matamshi yake yanathibitisha kwamba anayewananga mafisadi mmojawapo ni mzee Huyu EL. Pia vilevile naye EL Mara zote amepiga makelele kwamba anatukanwa Na vijana kwamba yeye ni Fisadi akimlenga NAPE. Kwa maana Kama hii hawa ni maadui wa kiitikadi.. Haupo uwezekano wakakaa meza moja Kwa Lolote lile. Sasa Leo Kama wako meza moja .. Mie hapo naskia kizunguzungu ..
   
 3. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mmmmmmh! Hypocricy is a Red devil in tz society and must be perished by any means especially peoples power!Magamba kaeni sawa mtakomaje!!?
   
Loading...