Salamu za kuukaribisha mwaka mpya wa 2020 kutoka kwa Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad kwa Watanzania

Zitto

MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Messages
1,467
Points
2,000

Zitto

MP Kigoma Urban
Joined Mar 2, 2007
1,467 2,000
SALAMU ZA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA 2020 KUTOKA KWA MSHAURI MKUU WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KWA WATANZANIA

Nami nianze kwa kumshukuru Mola wetu Mtukufu kwa kutujaalia kuishuhudia siku ya leo ambapo tunauaga mwaka 2019 na kuukaribisha mwaka 2020. Lakini leo siyo tu tunauaga mwaka mwaka 2019 bali tunaiaga miaka minne iliyopita na sasa tunaingia mwaka 2020 ambao ni mwaka muhimu sana kwetu kama Taifa.

Wazanzibari wanapita katika kipindi kigumu sana katika historia ya nchi yao, kipindi hichi cha miaka mine cha hilaki za kila namna kimeacha makovu ya kila namna kwa Wananchi wa Wazanzibar, kama ilivyo kwa ndugu zao wa Tanzania bara, yote haya ni kwasabau CCM ndio iliyojitwika dhima ya utawala na uendeshaji wa nchi kwa pande zote za Muungano, sasa unapokuwa na Chama kilichopoteza mweleko, Viongozi wake kila uchao wanapanga kubaki madarakani kwa hila badala ya ridhaa ya Wananchi ili kushibisha matumbo yao badala ya kuwatumikia wananchi, katika hali hii hapatarajiwi maendeleo ya aina yoyote, si maendeleo ya kisiasa, si maendeleo ya kiuchumi na wala si maendeleo ya kijamii.

Katika kipindi cha miaka mine hii, Zanzibar imebaki njia panda kutokana na mkwamo wa Uchaguzi Mkuu wa 2015. Tumekuwa na Serikali iliyojitwalia madaraka kwa mabavu bila kuheshimu matakwa ya wananchi wa Zanzibar ambao kikatiba ndio wenye mamlaka ya kuamua nani awe kiongozi wao.

Tumeshuhudia Watawala wakiendesha nchi kinyume na matakwa ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 pamoja na marekebisho yake ambayo yanataka kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Pia kufanyika marekebisho ya sheria yenye dhamira ovu ya kuendeleza mifarakano, chuki na uhasama kwa kuutumia Uchaguzi. Sheria hizi ni pamoja na Sheria ya Tume ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imepandikiza mbegu za ubaguzi miongoni mwa Wazanzibari kwa kitendo cha serikali iliyopo kuwapa haki watu wa kundi moja na kuwanyima wengine. Haya yanadhihirika katika suala zima la ajira hivi leo ambapo kijana wa Kizanzibari haajiriwi kwa uwezo wake bali anaajiriwa kwa kuangaliwa amezaliwa wapi na amezaliwa na nani kwa itikadi za kisiasa. Pia hata vyeo navyo vinagawiwa kwa misingi hii hii. GSO tuliyoitarajia kufanya kazi ya kuhakikisha usalama wa nchi, leo imegeuka kuwa kikundi cha kupita mitaani kutafuta itikadi za kisiasa za wanaoomba ajira wao na za wazazi wao. Ubaguzi pia umehamia hata katika kupata nyaraka na huduma muhimu kama vile vyeti vya kuzaliwa na vitambulisho vya Mzanzibari ambavyo hutumika kwa matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na haki ya kujiandikisha katika daftari la wapiga kura, kusafiria, benki, huduma za miamala ya simu, pia kwa wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu. Kwa masikitiko makubwa, vitambulisho hivi navyo hutolewa kwa ubaguzi kutegemeana na itikadi ya mtu ya kisiasa anayodhaniwa kuwa nayo. Wananchi wananyimwa haki zao za msingi na wengine kuharibiwa hatima za maisha yao kwa kunyimwa kitambulisho hiki.

Kuna ubadhirifu mkubwa unaofanyika serikalini hivi sasa na kwa kuwa kila mmoja anahusika na ubadhirifu huo, kila mmoja anamfumbia macho mwenzake. Kwa mfano, miradi yote mikubwa inayosimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar (ZSSF) ni ulaji wa baadhi ya wakubwa. Zipo pia taarifa kuwa baadhi ya wakubwa wamejichotoea mabilioni ya fedha kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ukiacha zile walizozichota katika kipindi cha uchaguzi wa marudio 2016 pamoja na chamani kwao CCM. Pia kuna taarifa za fedha za Wawekezaji, ambazo wakubwa serikalini wamezifanya ngawira kwa kugawana miongoni mwao. Si ajabu kwa hivyo kwamba miradi kadhaa imeshindwa kuendelezwa kwa sababu za kifisadi. Kinachoshangaza wakati Rais Magufuli akiwa mkali kupiga vita ufisadi na kutaka kutuaminisha kuwa hawezi kumvulia fisadi yoyote ndani ya Serikali yake na Chama anachokiongoza, Mafisadi kutoka Zanzibar wanapata kinga kwake.

Hali ya maisha kwa wananchi wa Zanzibar imezidi kuwa mbaya. Kipato cha mwananchi mmoja mmoja kimepungua mara dufu, uchumi unashuka kila uchao hata kama watawala wanajitahidi kutulisha takwimu za kukua kwa uchumi zisizoendana na hali halisi ya maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida. Wafanyabiashara si wakubwa si wadogo, wote wapo taaban kwa kodi kubwa na nyinyi. Vijana hawana ajira wala watwala hawana mpango wowote wa kuwafikiria vijana hawa. Wafanyakazi wa umma badala ya kuongezewa mishahara ili waweze kumudu maisha yao Watawala wanapunguza mishahara na mafao mengine mbali mbali ya watumishi wa umma. Watu wote wako taaban kwa dhiki ya maisha. Katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa Fedha, SMZ imetumia fedha nyingi zadi kwenye matumizi mengineyo kuliko hata mishahara ya Wafanyakazi na sehemu kubwa ya Fedha hizo ni kutoka Mfuko wa NSSF. Shirika hilo la ZSSF lilitoa mkopo mpya kwa SMZ kiasi cha Deni la ndani la SMZ kufikia shilingi Bilioni 141 kutoka shilingi Bilioni 108 mwaka unaoishia Septemba 2018. Hii inahatarisha mafao ya wastaafu katika ya umma na sekta binafsi Zanzibar maana wote wanachangia ZSSF.

Vile vile, mauzo nje yameporomoka kutokana na uzalishaji kwenye Karafuu na Mwani kuporomoka huku uagizaji wa bidhaa kutoka nje ukiongezeka kwa takribani 46%. Hii imesabbisha kipato kwa wananchi wa kawaida ambao ni wakulima wa Mwani na Karafuu kushuka na hali ya maisha kuwa magumu. Zanzibar ambayo kiasili ni Nchi ya biashara inazidi kuporomoka kwa sababu ya kukosekana kwa biashara, Bandari kutopanuliwa kulingana na umuhimu wake katika uchumi wetu na hata miradi kama Uwanja wa Ndege ambayo ni muhimu kwa sekta ya Utalii kutomalizwa kwa wakati na gharama zake kuongezeka sana.

Bahati nzuri, pamoja na madhila yote hayo yanayowakumba Wazanzibari, imekuwa ni kama kuwachonga ukali na kuwatia ari ya kupambana kuhakikisha kuwa WANAING’OA CCM pamoja na MIZIZI yake Zanzibar, Wazanzibari wanahamu na Uchaguzi ili kumaliza kazi waliyoianza 2015, Watawala wanauogopa Uchaguzi. Tunaukaribisha mwaka 2020 kwa hamu kubwa ili kuwapa fursa nyengine muhimu Wananchi wa Zanzibar ya kutimiza ndoto zao, si nyengine ni KUING’OA CCM madarakani ili kuondoa aina zote za dhuluma, ubaguzi, uhasama wa kisaiasa na dhiki ya maisha, na kuweka Uongozi mwema utakaowaunganisha Wazanzibari wote na utakaosimamia haki na uadilifu na kuimarisha uchumi wenye kutoa tija kwa Wazanzibari wote.

Muda huu tunapozungumza hapa, zimebaki saa chache tu kabla ya kuingia mwaka 2020. ACT WAZALENDO tunautangaza mwaka 2020 kuwa ni MWAKA WA KUING’OA CCM. Sisi katika ACT WAZALENDO na mimi binafsi nitaongoza juhudi za kuhakikisha tunaunda UMOJA WA DHATI utakaovishirikisha vyama vyote makini vya siasa, asasi za kiraia, vyama vya kitaaluma na makundi yote ya kijamii, UMOJA ambao utawaongoza Watanzania kufanikisha lengo la kuing’oa CCM na kuleta MABADILIKO MEMA nchini Tanzania, Zanzibar na Bara. Nitowe wito kwa Viongozi wezangu na Vyama vyetu vya siasa, pamoja na changamoto kadhaa zilizopo miongoni mwetu na vyama vyetu bado maslahi yanayotuunganisha kwa madhumuni ya KUING’OA CCM ni makubwa zaidi kuliko tofauti zetu. Ni wakati wa kuziweka tofauti zetu pembeni ili kuwaunganisha Watanzania pamoja KUING’OA CCM 2020.

Huu utakuwa ni mwaka ambao Watanzania tunakwenda kuandika historia – historia ya kwenda kuyazika madhila haya na kujiletea MABADILIKO MEMA yatakayobadilisha maisha yetu. Mwaka 2020 ni mwaka wa VITENDO wa kuleta MABADILIKO YA KWELI na kumaliza ulaghai wa watawala wa CCM. Mwaka 2020 ni mwaka wa kuhitimisha uongo wa watawala wa CCM, watawala ambao kila ikifika miaka mitano wamekuwa mahodari wa kutoa ahadi mpya bila ya kutueleza Watanzania kwa nini ahadi zilizopita ambazo wamekuwa wakizitoa miaka nenda miaka rudi wameshindwa kuzitekeleza.

ACT WAZALENDO kama Chama makini cha siasa tumejipanga kikamilifu kutekeleza wajibu wetu katika kuyafikia mabadiliko wanayoyataka Watanzania. Watanzania watarajie kushuhudia mengi na makubwa kutoka katika Chama chao hiki ambacho siku zote kimejipambanua kuwasemea katika mambo mazito yanayowakabili. Hivi sasa tumo katika maandalizi ya Ilani za Uchaguzi za Chama zitakazotumika kusaka ridhaa ya Watanzania na Wazanzibari kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Mimi na Kiongozi wa Chama, Ndugu Zitto Kabwe tunaongoza Ziara tuliyoipa jina la “Listening Tour” ambayo lengo lake ni kuwashirikisha wananchi katika maandalizi ya Ilani zetu kwa kusikiliza maoni yao kuhusu maeneo yepi wangependa kuyaona yanazingatiwa katika Ilani hizo, kwa maana ya Ilani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ilani ya Zanzibar. Tunataka ACT Wazalendo kiwe Chama cha mfano katika kuandaa Ilani Shirikishi.

ACT WAZALENDO tumedhamiria kuijenga Tanzania inayopaa kiuchumi, yenye maisha ya raha na furaha kwa watu wake wote. Tutabuni na kutekeleza sera zitakazohakikisha uchumi imara na shirikishi, huduma bora za jamii kwa wote na maisha ya raha na furaha kwa Watanzania wote. Tunaamini maoni tunayoyakusanya yatatupa Ilani zitakazotufikisha kwenye lengo hilo.

Kwa upande wa Zanzibar, Dira yetu ni kuiweka Zanzibar mahali inapostahiki katika ulimwengu ikiwa ni mlango wa kuingilia na kutokea Afrika, kituo kikuu cha biashara na huduma za fedha katika Bahari ya Hindi, kilele cha ubora katika kiwango cha elimu na kuwa jukwaa la kukuza mafahamiano baina ya tamaduni na ustaarabu tofauti duniani. Tunataka ACT WAZALENDO ituongoze kuifikia Zanzibar inayopaa kiuchumi, yenye umoja wa dhati na maisha ya raha na furaha kwa watu wake wote.

Zanzibar kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla inaweza kuwa kichocheo cha ukuaji wa biashara na uchumi kwa eneo hili kama Singapore ilivyo kwa Malaysia na eneo la nchi za Mashariki ya Mbali, au Hong Kong ilivyo kwa China, au Dubai ilivyo kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na eneo la Ghuba kwa ujumla. Tukifikia hapo sote Zanzibar na Tanganyika tutanufaika kwa pamoja. Kizuizi kinachotuzuia kuyafikia mafanikio hayo ya pamoja ni CCM ambayo inaamini katika kuidhibiti Zanzibar na Tanganyika badala ya kujenga ushirikiano wa dhati na wa kweli wa pamoja utakaotunyanyua na kutupaisha kiuchumi pamoja. 2020 tunakwenda kukiondoa kizuizi hiki ili sote tusonge mbele kwenye ukuaji wa kasi wa biashara na uchumi na kuzijenga nchi zetu huku watu wake wakiwa na raha na furaha. Haya yatafafanuliwa vizuri katika Ilani ya Uchaguzi wakati utakapowadia.

Wazanzibari wanazitambua fursa hizi na wanajua zinaweza kufikiwa tu ikiwa wataleta mabadiliko ya kisiasa. Ndiyo maana wamechagua mabadiliko mara zote. Hata 2020 hawatorudi nyuma wala kukatishwa tamaa kwa sababu wanalijua lengo la harakati zao na mabadiliko wanayoyapigania. Nitumie fursa hii kuwakumbusha na kuwahimiza Wazanzibari wote kwenda kuchukua vitambulisho vyao vipya ambavyo watawala wa sasa wameamua kuviita kuwa ni Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi. Tunajua vitimbi vyote vinavyofanyika kuwasumbua, lengo likiwa ni kuwakatisha tamaa ili wasende kuvifuatilia. Wito wangu kwa Wazanzibari wenzangu wote hatuna nafasi ya kukata tamaa. Twendeni tukachukue vitambulisho vyetu na wakati wa kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura sote twendeni tukajiandikishe. Tumedhamiria kuutumia mwaka 2020 kukamilisha kazi tuliyoifanya mwaka 2015. Kwa Wazanzibari, mwaka wa 2020 ni MWAKA WA FUNGA KAZI.

Katika ACT- WAZALENDO tunajua tuna changamoto ya Muungano wetu wa Tanzania. Tunataka mwaka 2020 uwe mwaka wa kuanza kuchukua hatua za kuweka madarakani chama chenye dhamira ya dhati ya kuboresha Muungano. Tunaamini katika Muungano wa Haki, wenye Usawa na Heshima. Tukifikia hapo sote Zanzibar na Tanganyika tutanufaika kwa pamoja. Kizuizi kinachotuzuia kuyafikia mafanikio hayo ya pamoja ni CCM ambayo inaamini katika kuidhibiti Zanzibar na Tanganyika badala ya kujenga ushirikiano wa dhati na wa kweli wa pamoja utakaotunyanyua na kutupaisha kiuchumi pamoja. Mwaka 2020 tunakwenda kukiondoa kizuizi hiki ili sote tusonge mbele kwenye ukuaji wa kasi wa biashara na uchumi na kuzijenga nchi zetu huku watu wake wakiwa na RAHA na FURAHA.

Kwa Watawala ujumbe wangu wa mwaka 2020 ni huu: Mmeidhulumu Zanzibar na mkawadhulumu Wazanzibari kwa kuwapora chaguo lao la waliyempa ridhaa kupitia kura zao awe Rais wao kwa chaguzi tano mfululizo kuanzia 1995 hadi 2015. Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25, 2015 ndiyo uliotia fora ambapo nilimshinda mgombea wao wa CCM, Dk. Ali Mohamed Shein kwa kupata kura 207,847 sawa na asilimia 52.8 dhidi ya kura 182,011 sawa na asilimia 46.2 alizopata yeye. Miaka yote hiyo nilifanya kazi ngumu sana ya kusimamia amani ya nchi kwa kuwatuliza Wazanzibari wanaoibiwa kura zao na kuporwa ushindi wao. Mwaka 2020 Wazanzibari watahakikisha wanazilinda kura zao na kuuhami ushindi wao.

Nimalizie kwa kuweka wazi msimamo wetu kwamba mwaka 2020 unapaswa kuwa mwisho wa CCM na kile kinachoitwa ‘deep state’ kutuamulia nani wa kututawala kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar. Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ibara ya 9 ya Katiba ya Zanzibar zinaweka wazi kwamba wananchi ndiyo msingi wa mamlaka ya nchi na Serikali na vyombo vyake vyote vinapaswa kutokana na wananchi wenyewe. Mwaka 2020 tutasimamia matakwa hayo ya Katiba zetu.

Nawatakia Watanzania wote Kheri na Baraka za Mwaka Mpya wa 2020.

Ahsanteni sana.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,999
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,999 2,000
Para ya pili:
Hichi= hiki
mine= minne
=====
Narudi Kwenye mada.
Ni wakati muafaka sasa Maalim Seif( mshauri mkuu wa ACT) agombeE urais wa JMT aachane na urais wa Zanzibar. Zitto afikirie namna ya kuwa mgombea mwenza wa Maalim Seif aachane na ubunge.
Kauli mbiu ya FUNGA KAZI tupate RAHA na FURAHA inaizamisha ACT mazima. Watanzsnia wa leo yaani wa Tanzania bara na Tanzania visiwa (Zanzibar), wanajua bila kufanyakazi halali raha na furaha inasikika 'redioni' tu! Kauli mbiu za namna hii, ACT, zitawafanya kuonekana wababaishaji. Leta kauli mbiu inayokidhi matakwa ya mpiga kura.

Si lazima kufuata ushauri wangu.
 
battawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Messages
874
Points
500

battawi

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2014
874 500

Tunaingia kwenye uchaguzi kwa Tume Ipi? ZEC?
Na wakisha tuibia tunkwenda wapi?
Maalim! sisi hatujakata tamaa,lakini ..................
Tunataka Plan B
Endapo watatufanya kama 2015 what next?
Kura yangu kwa hakika siwapi CCM, lakini mbona haina thamani endapo itaamua kumchagua mpinzania?
Na kupuuzwa maamuzi ya kura yangu? Naiteteaje? Mimi mbio sina,na silaha sina,na damu sinaya kumwaga,Nifanyeje?
Tunataka Plan B ili tuwakomeshe CCm ujinga wao wa kutu fedhehesha.
Ipo Plan B?
 
sweettablet

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Messages
3,906
Points
2,000

sweettablet

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2014
3,906 2,000

Plan B ni kuacha kupoteza kura yako 2020 na kukipa kura Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kikuletee maendeleo kwa kasi ya Upepo wa Kisulisuli chini ya Rais John Pombe Joseph Magufuli!!
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Messages
2,796
Points
2,000

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2018
2,796 2,000
Sipati picha ACT-Wazalendo #2020 wanachukua nchi, pale magogoni Zitto akimsimamia "JIWE" kupanga panga mabegi na mifuko mifuko yake, halafu na kumsindikiza kwenye gari ili arudishwe kwao "CHATO".

Ningeomba "TUKIO" hilo liwekwe "LIVE" kwenye "TBC". Kama tukio la "NAPE" lilivyokua.

#R.I.P Mama Kabendera
 
battawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Messages
874
Points
500

battawi

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2014
874 500
Plan B ni kuacha kupoteza kura yako 2020 na kukipa kura Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kikuletee maendeleo kwa kasi ya Upepo wa Kisulisuli chini ya Rais John Pombe Joseph Magufuli!!
🖕MIMI NINA UMRI WA MIAKA 53,
Tangu nijifahamu CCm inatoa ahadi za Uongo.
Kila kukicha Maisha yanazidi kwend mrama.
Wameshindwa waliokuwa hawalewi pombe ataweza Pombe mwenyewe?
Nishauri vizuri.
 
sweettablet

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Messages
3,906
Points
2,000

sweettablet

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2014
3,906 2,000
🖕MIMI NINA UMRI WA MIAKA 53,
Tangu nijifahamu CCm inatoa ahadi za Uongo.
Kila kukicha Maisha yanazidi kwend mrama.
Wameshindwa waliokuwa hawalewi pombe ataweza Pombe mwenyewe?
Nishauri vizuri.
Unanizidi miaka 7. Sina ugonjwa wa aina yoyote; pressure, kisukari, gout; you name it. Nasisitiza kukushauri, chagua CCM 2020. Hutakumbwa na magonjwa nyemelezi katika uzee wako kama mimi! Karibu CCM tuufurahie uzee!!
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Messages
14,254
Points
2,000

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2016
14,254 2,000
SALAMU ZA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA 2020 KUTOKA KWA MSHAURI MKUU WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KWA WATANZANIA

Nami nianze kwa kumshukuru Mola wetu Mtukufu kwa kutujaalia kuishuhudia siku ya leo ambapo tunauaga mwaka 2019 na kuukaribisha mwaka 2020. Lakini leo siyo tu tunauaga mwaka mwaka 2019 bali tunaiaga miaka minne iliyopita na sasa tunaingia mwaka 2020 ambao ni mwaka muhimu sana kwetu kama Taifa.

Wazanzibari wanapita katika kipindi kigumu sana katika historia ya nchi yao, kipindi hichi cha miaka mine cha hilaki za kila namna kimeacha makovu ya kila namna kwa Wananchi wa Wazanzibar, kama ilivyo kwa ndugu zao wa Tanzania bara, yote haya ni kwasabau CCM ndio iliyojitwika dhima ya utawala na uendeshaji wa nchi kwa pande zote za Muungano, sasa unapokuwa na Chama kilichopoteza mweleko, Viongozi wake kila uchao wanapanga kubaki madarakani kwa hila badala ya ridhaa ya Wananchi ili kushibisha matumbo yao badala ya kuwatumikia wananchi, katika hali hii hapatarajiwi maendeleo ya aina yoyote, si maendeleo ya kisiasa, si maendeleo ya kiuchumi na wala si maendeleo ya kijamii.

Katika kipindi cha miaka mine hii, Zanzibar imebaki njia panda kutokana na mkwamo wa Uchaguzi Mkuu wa 2015. Tumekuwa na Serikali iliyojitwalia madaraka kwa mabavu bila kuheshimu matakwa ya wananchi wa Zanzibar ambao kikatiba ndio wenye mamlaka ya kuamua nani awe kiongozi wao.

Tumeshuhudia Watawala wakiendesha nchi kinyume na matakwa ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 pamoja na marekebisho yake ambayo yanataka kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Pia kufanyika marekebisho ya sheria yenye dhamira ovu ya kuendeleza mifarakano, chuki na uhasama kwa kuutumia Uchaguzi. Sheria hizi ni pamoja na Sheria ya Tume ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imepandikiza mbegu za ubaguzi miongoni mwa Wazanzibari kwa kitendo cha serikali iliyopo kuwapa haki watu wa kundi moja na kuwanyima wengine. Haya yanadhihirika katika suala zima la ajira hivi leo ambapo kijana wa Kizanzibari haajiriwi kwa uwezo wake bali anaajiriwa kwa kuangaliwa amezaliwa wapi na amezaliwa na nani kwa itikadi za kisiasa. Pia hata vyeo navyo vinagawiwa kwa misingi hii hii. GSO tuliyoitarajia kufanya kazi ya kuhakikisha usalama wa nchi, leo imegeuka kuwa kikundi cha kupita mitaani kutafuta itikadi za kisiasa za wanaoomba ajira wao na za wazazi wao. Ubaguzi pia umehamia hata katika kupata nyaraka na huduma muhimu kama vile vyeti vya kuzaliwa na vitambulisho vya Mzanzibari ambavyo hutumika kwa matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na haki ya kujiandikisha katika daftari la wapiga kura, kusafiria, benki, huduma za miamala ya simu, pia kwa wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu. Kwa masikitiko makubwa, vitambulisho hivi navyo hutolewa kwa ubaguzi kutegemeana na itikadi ya mtu ya kisiasa anayodhaniwa kuwa nayo. Wananchi wananyimwa haki zao za msingi na wengine kuharibiwa hatima za maisha yao kwa kunyimwa kitambulisho hiki.

Kuna ubadhirifu mkubwa unaofanyika serikalini hivi sasa na kwa kuwa kila mmoja anahusika na ubadhirifu huo, kila mmoja anamfumbia macho mwenzake. Kwa mfano, miradi yote mikubwa inayosimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar (ZSSF) ni ulaji wa baadhi ya wakubwa. Zipo pia taarifa kuwa baadhi ya wakubwa wamejichotoea mabilioni ya fedha kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ukiacha zile walizozichota katika kipindi cha uchaguzi wa marudio 2016 pamoja na chamani kwao CCM. Pia kuna taarifa za fedha za Wawekezaji, ambazo wakubwa serikalini wamezifanya ngawira kwa kugawana miongoni mwao. Si ajabu kwa hivyo kwamba miradi kadhaa imeshindwa kuendelezwa kwa sababu za kifisadi. Kinachoshangaza wakati Rais Magufuli akiwa mkali kupiga vita ufisadi na kutaka kutuaminisha kuwa hawezi kumvulia fisadi yoyote ndani ya Serikali yake na Chama anachokiongoza, Mafisadi kutoka Zanzibar wanapata kinga kwake.

Hali ya maisha kwa wananchi wa Zanzibar imezidi kuwa mbaya. Kipato cha mwananchi mmoja mmoja kimepungua mara dufu, uchumi unashuka kila uchao hata kama watawala wanajitahidi kutulisha takwimu za kukua kwa uchumi zisizoendana na hali halisi ya maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida. Wafanyabiashara si wakubwa si wadogo, wote wapo taaban kwa kodi kubwa na nyinyi. Vijana hawana ajira wala watwala hawana mpango wowote wa kuwafikiria vijana hawa. Wafanyakazi wa umma badala ya kuongezewa mishahara ili waweze kumudu maisha yao Watawala wanapunguza mishahara na mafao mengine mbali mbali ya watumishi wa umma. Watu wote wako taaban kwa dhiki ya maisha. Katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa Fedha, SMZ imetumia fedha nyingi zadi kwenye matumizi mengineyo kuliko hata mishahara ya Wafanyakazi na sehemu kubwa ya Fedha hizo ni kutoka Mfuko wa NSSF. Shirika hilo la ZSSF lilitoa mkopo mpya kwa SMZ kiasi cha Deni la ndani la SMZ kufikia shilingi Bilioni 141 kutoka shilingi Bilioni 108 mwaka unaoishia Septemba 2018. Hii inahatarisha mafao ya wastaafu katika ya umma na sekta binafsi Zanzibar maana wote wanachangia ZSSF.

Vile vile, mauzo nje yameporomoka kutokana na uzalishaji kwenye Karafuu na Mwani kuporomoka huku uagizaji wa bidhaa kutoka nje ukiongezeka kwa takribani 46%. Hii imesabbisha kipato kwa wananchi wa kawaida ambao ni wakulima wa Mwani na Karafuu kushuka na hali ya maisha kuwa magumu. Zanzibar ambayo kiasili ni Nchi ya biashara inazidi kuporomoka kwa sababu ya kukosekana kwa biashara, Bandari kutopanuliwa kulingana na umuhimu wake katika uchumi wetu na hata miradi kama Uwanja wa Ndege ambayo ni muhimu kwa sekta ya Utalii kutomalizwa kwa wakati na gharama zake kuongezeka sana.

Bahati nzuri, pamoja na madhila yote hayo yanayowakumba Wazanzibari, imekuwa ni kama kuwachonga ukali na kuwatia ari ya kupambana kuhakikisha kuwa WANAING’OA CCM pamoja na MIZIZI yake Zanzibar, Wazanzibari wanahamu na Uchaguzi ili kumaliza kazi waliyoianza 2015, Watawala wanauogopa Uchaguzi. Tunaukaribisha mwaka 2020 kwa hamu kubwa ili kuwapa fursa nyengine muhimu Wananchi wa Zanzibar ya kutimiza ndoto zao, si nyengine ni KUING’OA CCM madarakani ili kuondoa aina zote za dhuluma, ubaguzi, uhasama wa kisaiasa na dhiki ya maisha, na kuweka Uongozi mwema utakaowaunganisha Wazanzibari wote na utakaosimamia haki na uadilifu na kuimarisha uchumi wenye kutoa tija kwa Wazanzibari wote.

Muda huu tunapozungumza hapa, zimebaki saa chache tu kabla ya kuingia mwaka 2020. ACT WAZALENDO tunautangaza mwaka 2020 kuwa ni MWAKA WA KUING’OA CCM. Sisi katika ACT WAZALENDO na mimi binafsi nitaongoza juhudi za kuhakikisha tunaunda UMOJA WA DHATI utakaovishirikisha vyama vyote makini vya siasa, asasi za kiraia, vyama vya kitaaluma na makundi yote ya kijamii, UMOJA ambao utawaongoza Watanzania kufanikisha lengo la kuing’oa CCM na kuleta MABADILIKO MEMA nchini Tanzania, Zanzibar na Bara. Nitowe wito kwa Viongozi wezangu na Vyama vyetu vya siasa, pamoja na changamoto kadhaa zilizopo miongoni mwetu na vyama vyetu bado maslahi yanayotuunganisha kwa madhumuni ya KUING’OA CCM ni makubwa zaidi kuliko tofauti zetu. Ni wakati wa kuziweka tofauti zetu pembeni ili kuwaunganisha Watanzania pamoja KUING’OA CCM 2020.

Huu utakuwa ni mwaka ambao Watanzania tunakwenda kuandika historia – historia ya kwenda kuyazika madhila haya na kujiletea MABADILIKO MEMA yatakayobadilisha maisha yetu. Mwaka 2020 ni mwaka wa VITENDO wa kuleta MABADILIKO YA KWELI na kumaliza ulaghai wa watawala wa CCM. Mwaka 2020 ni mwaka wa kuhitimisha uongo wa watawala wa CCM, watawala ambao kila ikifika miaka mitano wamekuwa mahodari wa kutoa ahadi mpya bila ya kutueleza Watanzania kwa nini ahadi zilizopita ambazo wamekuwa wakizitoa miaka nenda miaka rudi wameshindwa kuzitekeleza.

ACT WAZALENDO kama Chama makini cha siasa tumejipanga kikamilifu kutekeleza wajibu wetu katika kuyafikia mabadiliko wanayoyataka Watanzania. Watanzania watarajie kushuhudia mengi na makubwa kutoka katika Chama chao hiki ambacho siku zote kimejipambanua kuwasemea katika mambo mazito yanayowakabili. Hivi sasa tumo katika maandalizi ya Ilani za Uchaguzi za Chama zitakazotumika kusaka ridhaa ya Watanzania na Wazanzibari kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Mimi na Kiongozi wa Chama, Ndugu Zitto Kabwe tunaongoza Ziara tuliyoipa jina la “Listening Tour” ambayo lengo lake ni kuwashirikisha wananchi katika maandalizi ya Ilani zetu kwa kusikiliza maoni yao kuhusu maeneo yepi wangependa kuyaona yanazingatiwa katika Ilani hizo, kwa maana ya Ilani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ilani ya Zanzibar. Tunataka ACT Wazalendo kiwe Chama cha mfano katika kuandaa Ilani Shirikishi.

ACT WAZALENDO tumedhamiria kuijenga Tanzania inayopaa kiuchumi, yenye maisha ya raha na furaha kwa watu wake wote. Tutabuni na kutekeleza sera zitakazohakikisha uchumi imara na shirikishi, huduma bora za jamii kwa wote na maisha ya raha na furaha kwa Watanzania wote. Tunaamini maoni tunayoyakusanya yatatupa Ilani zitakazotufikisha kwenye lengo hilo.

Kwa upande wa Zanzibar, Dira yetu ni kuiweka Zanzibar mahali inapostahiki katika ulimwengu ikiwa ni mlango wa kuingilia na kutokea Afrika, kituo kikuu cha biashara na huduma za fedha katika Bahari ya Hindi, kilele cha ubora katika kiwango cha elimu na kuwa jukwaa la kukuza mafahamiano baina ya tamaduni na ustaarabu tofauti duniani. Tunataka ACT WAZALENDO ituongoze kuifikia Zanzibar inayopaa kiuchumi, yenye umoja wa dhati na maisha ya raha na furaha kwa watu wake wote.

Zanzibar kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla inaweza kuwa kichocheo cha ukuaji wa biashara na uchumi kwa eneo hili kama Singapore ilivyo kwa Malaysia na eneo la nchi za Mashariki ya Mbali, au Hong Kong ilivyo kwa China, au Dubai ilivyo kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na eneo la Ghuba kwa ujumla. Tukifikia hapo sote Zanzibar na Tanganyika tutanufaika kwa pamoja. Kizuizi kinachotuzuia kuyafikia mafanikio hayo ya pamoja ni CCM ambayo inaamini katika kuidhibiti Zanzibar na Tanganyika badala ya kujenga ushirikiano wa dhati na wa kweli wa pamoja utakaotunyanyua na kutupaisha kiuchumi pamoja. 2020 tunakwenda kukiondoa kizuizi hiki ili sote tusonge mbele kwenye ukuaji wa kasi wa biashara na uchumi na kuzijenga nchi zetu huku watu wake wakiwa na raha na furaha. Haya yatafafanuliwa vizuri katika Ilani ya Uchaguzi wakati utakapowadia.

Wazanzibari wanazitambua fursa hizi na wanajua zinaweza kufikiwa tu ikiwa wataleta mabadiliko ya kisiasa. Ndiyo maana wamechagua mabadiliko mara zote. Hata 2020 hawatorudi nyuma wala kukatishwa tamaa kwa sababu wanalijua lengo la harakati zao na mabadiliko wanayoyapigania. Nitumie fursa hii kuwakumbusha na kuwahimiza Wazanzibari wote kwenda kuchukua vitambulisho vyao vipya ambavyo watawala wa sasa wameamua kuviita kuwa ni Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi. Tunajua vitimbi vyote vinavyofanyika kuwasumbua, lengo likiwa ni kuwakatisha tamaa ili wasende kuvifuatilia. Wito wangu kwa Wazanzibari wenzangu wote hatuna nafasi ya kukata tamaa. Twendeni tukachukue vitambulisho vyetu na wakati wa kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura sote twendeni tukajiandikishe. Tumedhamiria kuutumia mwaka 2020 kukamilisha kazi tuliyoifanya mwaka 2015. Kwa Wazanzibari, mwaka wa 2020 ni MWAKA WA FUNGA KAZI.

Katika ACT- WAZALENDO tunajua tuna changamoto ya Muungano wetu wa Tanzania. Tunataka mwaka 2020 uwe mwaka wa kuanza kuchukua hatua za kuweka madarakani chama chenye dhamira ya dhati ya kuboresha Muungano. Tunaamini katika Muungano wa Haki, wenye Usawa na Heshima. Tukifikia hapo sote Zanzibar na Tanganyika tutanufaika kwa pamoja. Kizuizi kinachotuzuia kuyafikia mafanikio hayo ya pamoja ni CCM ambayo inaamini katika kuidhibiti Zanzibar na Tanganyika badala ya kujenga ushirikiano wa dhati na wa kweli wa pamoja utakaotunyanyua na kutupaisha kiuchumi pamoja. Mwaka 2020 tunakwenda kukiondoa kizuizi hiki ili sote tusonge mbele kwenye ukuaji wa kasi wa biashara na uchumi na kuzijenga nchi zetu huku watu wake wakiwa na RAHA na FURAHA.

Kwa Watawala ujumbe wangu wa mwaka 2020 ni huu: Mmeidhulumu Zanzibar na mkawadhulumu Wazanzibari kwa kuwapora chaguo lao la waliyempa ridhaa kupitia kura zao awe Rais wao kwa chaguzi tano mfululizo kuanzia 1995 hadi 2015. Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25, 2015 ndiyo uliotia fora ambapo nilimshinda mgombea wao wa CCM, Dk. Ali Mohamed Shein kwa kupata kura 207,847 sawa na asilimia 52.8 dhidi ya kura 182,011 sawa na asilimia 46.2 alizopata yeye. Miaka yote hiyo nilifanya kazi ngumu sana ya kusimamia amani ya nchi kwa kuwatuliza Wazanzibari wanaoibiwa kura zao na kuporwa ushindi wao. Mwaka 2020 Wazanzibari watahakikisha wanazilinda kura zao na kuuhami ushindi wao.

Nimalizie kwa kuweka wazi msimamo wetu kwamba mwaka 2020 unapaswa kuwa mwisho wa CCM na kile kinachoitwa ‘deep state’ kutuamulia nani wa kututawala kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar. Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ibara ya 9 ya Katiba ya Zanzibar zinaweka wazi kwamba wananchi ndiyo msingi wa mamlaka ya nchi na Serikali na vyombo vyake vyote vinapaswa kutokana na wananchi wenyewe. Mwaka 2020 tutasimamia matakwa hayo ya Katiba zetu.

Nawatakia Watanzania wote Kheri na Baraka za Mwaka Mpya wa 2020.

Ahsanteni sana.
Zitto tatizo lako kubwa ni uongo huaminiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
battawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Messages
874
Points
500

battawi

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2014
874 500
Unanizidi miaka 7. Sina ugonjwa wa aina yoyote; pressure, kisukari, gout; you name it. Nasisitiza kukushauri, chagua CCM 2020. Hutakumbwa na magonjwa nyemelezi katika uzee wako kama mimi! Karibu CCM tuufurahie uzee!!
Sikuiona neema ningali kijana ,niitegemee leo uzeeni,Mbona hao vijana wa leo wote nawona choka mbaya ,na kila uchao baadhi yao wanakusanya degeree lakini hawana ajira.
 
Forum statistics

Threads 1,391,720
Members 528,450
Posts 34,087,414
Top