Athari za makundi ndani ya chama cha mapinduzi hususani wakati wa uchaguzi ndani ya chama

NYARUKURURU

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
349
199
Ndugu wasomaji wa makala yangu hii, mtakumbuka trh 13 December 2016 Halmashauri kuu ya CCM Taifa ilipitisha kwa kishindo mabadiliko ya kimuundo na ya kiuongozi ndani ya CCM, ikiwemo kupunguza wajumbe wa CC kutoka 34 mpaka 24 na wajumbe wa NEC kutoka 388 mpaka 158 ni jambo jema mimi binafsi naupongeza uwamuzi huu maana ndo ulitumiwa na Baba wa Taifa letu.

Lakini leo mimi napenda kujikita zaidi katika athari za makundi ndani ya chama nyakati za chaguzi za chama cha Mapinduzi na katika hili nitatumia nukuu nyingi kutoka kitabu cha mwalimu Nyerere kiitwacho "TUJISAHIHISHE" alichokiandika May, 1962 akiwa Rais wa TANU, na Rais wa Tanganyika.

Kwa wale wavivu wa kusoma makala hii nawashauri wasikomenti kwa kusoma mistari miwili tu na kuanza kutoa matusi ni vyema kusoma mpaka mwisho ili kujielimisha na kuelimika na pole kwa wale nitakao waumiza kwakusema ukweli.

Ni ukweli usiopingika kuwa ili chama chochote cha siasa kiweze kuwa imara na kuonesha dira ni lazima kiwe na jumuiya imara zenye uwezo wa kukosoa mtu yeyote ndani ya chama anaetenda kinyume na katiba ya Chama hata Kama ni mwenyekiti wa chama hicho.

Ni lazima jumuiya za chama zitetee chama hicho kwa gharama yoyote Ile na kuhakikisha chama hicho hakiingiliwi na mtu yeyote yule hata Kama ni mataifa ya kigeni yenye nguvu.

Pia, jumuiya za Chama zinajukumu la kulinda Serikali yake, kwa Chama kinachotawala kuhakikisha hakuna nchi yeyote inayoingilia mambo ya ndani ya hiyo.

Ndugu wasomaji wangu, ninyi nyote ni mashahidi kwa muda wa Miaka mitano sasa tumekuwa na jumuiya ya akina mama bubu isiyoongea na isiyoonesha dira ni dhahiri kwasasa ukimuuliza mtu nani mwenyekiti wa UWT-CCM Taifa hakuna anae mjua labda kwa makada halisi wa CCM hii yote ni kwasababu hawajibiki ipasavyo, sio kweli kwamba wote walioko chini yake hawafanyi kazi lahasha ispokuwa yeye kiongozi wao wa juu ndo anawaangusha hawaoneshi njia ipasavyo.

Vivyo hivyo, katika jumuiya ya Umoja Wa Vijana CCM Taifa, kwa miaka mitano sasa hakuna muelekeo, imekuwa jumuiya ya kukaa ofsini tu na kusubiri mishahara, imekuwa jumuiya isiyoonesha dira kwa vijana wa CCM.

Imekuwa jumuiya isiyotetea Serikali yake, tuliona mwaka 2015 mara baada ya uchaguzi mataifa ya Magharibi yakaingilia kati mgogoro wa Zanzibar na chombo pekee cha CCM kukemea na kulaani kauli hizo ilikuwa ni UVCCM Taifa tena kwa kuendesha maandamano ya amani kutoka makao makuu yao kwenda Ubalozi wa Ulaya kuwataka wasiingilie mambo yetu ya ndani lakini walifumba macho.

Sio kwamba viongozi wote wa jumuiya hii hawawezi kazi la hasha wapo wengi wako vzr sana ispokuwa wanarudishwa nyuma na viongozi wao wa juu

Ni aibu kubwa leo jumuiya ya wazazi ina nguvu kuliko UVCCM Taifa, na hii tumshukuru Mungu maana CHADEMA nao walijichanganya wakamchagua mwenyekiti mbovu kuliko wa UVCCM ndo maana CCM leo Kuna nafuu.

Chama cha Mapinduzi ni chama bora Barani Africa, kufanya mabadiliko ya kimuundo tu hayatoshi ni vyema kuweka misingi imara ya kuhakikisha chama na jumuiya zake zinapata viongozi bora na imara bila kutumia Rushwa, na kukomesha tabia ya watu kushinda uchaguzi kwa vile ni watoto wa viongozi wakubwa wa Serikali na Chama cha Mapinduzi, mtu ashinde kwasababu anauwezo wa kuongoza na sio mtoto wa kigogo au kwa vile anapesa nyingi.

Nimeamua kuandika mambo haya kwasababu ndo yaliyotumika mwaka 2012 kupata viongozi ndani ya jumuiya za chama, viongozi wengi waliopita mwaka 2012 katika jumuiya ya Umoja wa Vijana na akina mama walitumia pesa nyingi na wengi wao waliopita ni kwasababu walimuunga mkono Mh, Lowasa akilenga kuwa Rais mwaka 2015.

Katika kitabu cha mwalimu Nyerere kiitwacho "TUJISAHIHISHE" ukurasa wa kwanza ameandika "umoja wa kundi lolote ni sawa sawa na umoja wa viungo mbali mbali vya mwili au mtambo. Viungo vya mwili havina budi vitii kanuni zinazoviwezesha kufanya kazi yake sawa sawa" mwisho wa kunukuu, Vivyo hivyo umoja wa wanachama wa CCM wanapaswa kufuata katiba na kanuni za uchaguzi, inapaswa viongozi wa CCM Taifa kuchukua tahadhari zaidi ili yaliyotokea mwaka 2012 yasitokee mwaka huu 2017.

Ni dhahiri yaliyotokea mwaka 2012 mpaka sasa Kuna viashiria, wapo watu wanajiandaa kugombea Urais mwaka 2025 na sasa wanapanga safu zao katika jumuiya hizi na ndani ya CCM kuanzia ngazi ya kata na sasa wanawagombea wao mfukoni na wanawaandaa kugombea mikoani, wilaya na Taifa. Endapo kamati kuu haitakuwa makini tena tutapata viongozi wasio na sifa kwa maslahi ya watu.

Miongoni mwa vitu vingine vinavyopaswa kafanyiwa mabadiliko ndani ya CCM ni pamoja na :

Kitendo cha mbunge kufariki Dunia na kuteua mme, mke au mtoto wake kuwa mgombea ubunge kana kwamba chama hakina makada wengine katika jimbo hilo na wakati wako wengi na wenye sifa

Kitendo cha kutopandisha mishahara ya madereva na watumishi wengine wa Chama wakati wao ndo watendaji wakuu na hii imepelekea wao kuomba na kupokea rushwa nyakati za chaguzi.

Hizi ni baadhi ya kero zinazo waudhi wanachama wa CCM na pengine kuelekea kupoteza majimbo wakati wa uchaguzi nazo yapaswa kushughulikiwa ipasavyo.

Mwisho.
Nimeamua kuandika ili ujumbe huu uwafikie wanachama wote CCM na wale wanaojiandaa kujiunga na ccm maana ndo Chama bora, japo Kuna watu wengi watanitukana baada ya kuwagusa na kutaja vyeo vyao lakini hakuna namna yawapasa wavumilie, mimi huwa sio mnafiki na nawataka nanyi msiwe wanafiki mtu akikosea sema hadharani hata Baba wa Taifa alisema kwenye kitabu chake nina nukuu "....... Dalili nyingine ya unafsi, na ambayo ni ugonjwa mbaya sana, ni fitina......... Wengine humwona mwenzao anafanya kosa. Badala ya kumwambia palepale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya sirisiri. Mateto haya Si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru..... "

Kwakuzingatia nukuu hiyo hapo juu ya mwalimu Nyerere nami Nimeamua kuwasema hawa viongozi ili wajirekebishe kwa maana bado Taifa linawaitaji katika nyadhifa mbali mbali na ukizingatia wengine bado vijana.
Imeandaliwa na,
Comrade
Mwita nyarukururu
Mpinga mafisadi
 
Back
Top Bottom