MAKAPILE
Member
- Mar 27, 2012
- 8
- 1
Kutokana na habari za hapo asubuhi inasadikika kwamba waziri aliyejiuzulu kwa kashifa za ufisadi hatimae atajitokeza hazarani kwa kumnadi mkwe wake Sioi akiambatana na Nape ambaye anajipambanua kuwa yeye ni mpambanaji wa ufisadi; Kutokana na kauli zake za mara kwa mara akisema watawafukuza mafisadi, ikiwa ni kinyume kabisa na maneno yake kwa kuongozana na mh Lowasa.
Hivyo anaonesha dhahiri kwamba anachotenda si sahihi kabisa kwa jamii ya watanzania na ninamfananisha mh Nape kama wale wakristo ambao katika bibilia ambao wanamkiri kristo mdomoni mwao lakini miyoni mwao hayupo, watu hawa ni wanafiki sana na ni watu hatari sana kwa jamii yetu.
Pia kunamnafiki mwingine mh Ole Sendeka kwa kuwaongopea wanaarumeru na jamii zima ya Tanzania kwa kwenda kumnadi Sioi huku akijua kawekwa na MAFISADI,pia haitoshi uchaguzi wa kura za maoni uliendeshwa kwa rushwa.
Pia ningependa kusema hata waandishi wa habari hawaitendei haki jamii ya kitanzania kwa kuficha ukweli.Tungependa kuona kituo fulania cha TV au gazeti kwa kuwauliza hao wanaojiita wapambanaji Ole Sendeka na Nape maswali mbalimbali ikiwamo kwanini wanajiita wapambanaji ilihali wanakuwa wanafiki kwa kuongozana na mafisadi? Pia tuwauleza walikua wapi katika miaka 50 ya uhuru katika kutatua matatizo ya wanaarumeru ikiwamo swala la ardhi na maji?