Unafiki wa marafiki wa kibongo ndio huu..

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
8,969
16,930
Sijachanganyika sana na watu wa mataifa mengine hivyo sitaweza kuwaongelea hapa. Kwa kifupi sisi watanzania tuna urafiki wa kinafiki,tunampenda mtu au tunapendelea kuwa na urafiki na watu ambao wana kauwezo flani ka kimaisha.

Binafsi nilimaliza chuo mwaka 2014 na sikuwa nimebahatika kupata walau kibarua chochote cha kuniwezesha walau hata kununua shati la mtumba. Kwa kifupi nilikua nimefulia zaidi ya maelezo hata wale marafiki zangu wa karibu wakawa wananitenga,ukimpigia mtu hapokei wala hajibu texts zako na wakati mwingine unamuona mtu yuko online watsapp unamtext lkn anakukaushia tu,

Ni kawaida kwa hali kama hiyo na kama binadamu mwenye moyo wa nyama lazima ikuume sana kuona wenzio mliocheza nao na kunywa nao uji toka chekechea wanakuchunia ila nikajipa moyo tu kuwa siku moja na me ntaja kuwa mtu walau kama wao.

Sasa bhana na mimi siku chache zilizopita nimebahatika kupata kibarua kwenye ofisi moja hapa Dar. Siku ya kwanza kuripoti job nimeenda nimeulamba na baada ya kukabidhiwa kiti changu nikawa nimejifotoa kapicha alafu nikakaweka watsapp kama profile picture na nikaandika status kwamba [HASHTAG]#new[/HASHTAG] year,new place and new life# thanx God for everything#

Aisee ndani ya lisaa limoja nimetafutwa na watu ambao hata sikutarajia kama wanaweza kunitafuta mtu kama mimi maana nilijua hata number yangu huenda walishaifuta long time. Wengine wanajifanya eti kukulaumu mbona siku hizi huwatafuti na wkt wao ndio walikua wanakuchunia kisa wana tumshahara twa ubank teller.

Sasa huu kama sio unafiki ni nin maana kipindi niko juu ya mawe watu walikua wananichunia leo na me nimebahatika kupata kakibarua ndio watu wanataka tena urafiki na mimi.
Tujifunze kuwapenda hata wasiokua na kitu,huwezijua kesho ya mwenzio ikoje.
 
ee40c86ded4c016e00f31cd1e3fa3e84.jpg
 
sijachanganyika sana na watu wa mataifa mengine hivyo sitaweza kuwaongelea hapa.
kwa kifupi sisi watanzania tuna urafiki wa kinafiki,tunampenda mtu au tunapendelea kuwa na urafiki na watu ambao wana kauwezo flani ka kimaisha.
Binafsi nilimaliza chuo mwaka 2014 na sikuwa nimebahatika kupata walau kibarua chochote cha kuniwezesha walau hata kununua shati la mtumba.kwa kifupi nilikua nimefulia zaidi ya maelezo hata wale marafiki zangu wa karibu wakawa wananitenga,ukimpigia mtu hapokei wala hajibu texts zako na wakati mwingine unamuona mtu yuko online watsapp unamtext lkn anakukaushia tu,ofkoz kwa hali kama hiyo na kama binadamu mwenye moyo wa nyama lazima ikuume sana kuona wenzio mliocheza nao na kunywa nao uji toka chekechea wanakuchunia ila nikajipa moyo tu kuwa siku moja na me ntaja kuwa mtu walau kama wao.
sasa bana na me siku chache zilizopita nimebahatika kupata kakibarua kwenye ofisi moja hapa dar,siku ya kwanza kuripoti job nimeenda nimeulamba na baada ya kukabidhiwa kiti changu nikawa nimejifotoa kapicha alafu nikakaweka watsapp kama profile picture na nikaandika status kwamba [HASHTAG]#new[/HASHTAG] year,new place and new life# thanx God for everything# aisee ndani ya lisaa limoja nimetafutwa na watu ambao hata sikutarajia kama wanaweza kunitafuta mtu kama mimi maana nilijua hata number yangu huenda walishaifuta long time.wengine wanajifanya eti kukulaumu mbona siku hizi huwatafuti na wkt wao ndio walikua wanakuchunia kisa wana tumshahara twa ubank teller.sasa huu kama sio unafiki ni nin maana kipindi niko juu ya mawe watu walikua wananichunia leo na me nimebahatika kupata kakibarua ndio watu wanataka tena urafiki na mimi.
Tujifunze kuwapenda hata wasiokua na kitu,huwezijua kesho ya mwenzio ikoje.
Kumbuka daima usemi wa kihenga "a friend in need is a friend indeed"
 
Back
Top Bottom