Unafiki, Ulaghai na Woga wa CCM!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
CCM ni wanafiki, walaghai na waoga!

Hakuna ambaye anaweza kuniambia kuwa nyakati hizi na mambo yanayotokea Tanzania na ndani ya CCM kuwa kilichotokea Dodoma ndani ya CCM wiki iliyopita na kauli zote zilizofuatia si Unafiki, Ulaghai au Woga!

Naomba ni wakumbushe Wana-CCM wanapokuja na kauli zao za kujivua gamba na kwamba sasa wamejizatiti kivitendo kupigana na Uhujumu, Ufisadi, Rushwa na Uzembe, je mlikuwa wapi siku zote wakati Watanzania walipokuwa wakipiga kelele?

Je tuwaamini vipi safari hii, ilhali Mwenyekiti bado ni yule yule aliyefukia mambo mlipokutana Butiama na hata yeye kuwa hapo anatuhumiwa mengi?

KWa nini mlipokutana Butiama, mkijua tuhuma nzito za Ufisadi zikiwa zimekikabili Chama, anzia IPTL, ATCL, TRC, Rada, EPA, Richmond, Buzwagi na rip[oti ya miaka miwili ya CAG, kwa nini hamkuchukua hatua mnazodai kuzichukua leo hii?

Kwa nini hamkuwapa fursa mwaka ule waliotuhumiwa kwa orodha ya Ufisadi na ile barua ya Jeetu Patel wasijivue uongozi wa chama?

Leo hii, mnadai kuwa waliokitia chama madoa ya Ufisadi na Uzembe wanajijua, na mnawaomba, hebo mnawaomba! Kwa nini msiwataje kuwa jamani, wewe, wewe na yule mnatuhuma nyingi, tumetumia TAKUKURU, Polisi na hata makachero wa nje, na mmethibitika Vijisenti vyenu si vya halali!

Mnaoneana nini aibu? Hata kule UVCCM ambapo leo hii tunasikia shangwe kupongeza vijana kushika hatamu, nako ni majungu na shutuma tupu!

Tukubaliane moja, CCM ni waoga kushughulikia jini walilolizalisha ndani na kulitumia kwa manufaa yao. CCm ni Wazandiki na Wanafiki, wanawadanganya Watanzania kuwa wanajisahihisha.

Je mlipokaa chini na kuandika Tujisahihishe, tuwasamehe mara 70 kama Wakristo na mafundisho ya Kristo kugeuza shavu mpaka lini?

Acheni kutulaghai, nyinyi ni Wanafiki na Waoga mnaoogopana kutokana na kutumiana kwa manufaa yenu ya pamoja kama Chama kuihujumu Tanzania!
 
Mkuu utaumiza kichwa kuyasema haya majivua gamba! Sanaa tu zimewajaa, yaani juzi nilipo msikia Msekwa nikajua sanaa imefika mahali pake, eti wamejipanga kupiga vita ufisadi
 
Umesema kweli Rev. Mie pia nilishangaa hotuba za viongozi wao kujitapa wakato work done was 0. Kwamba wazunguke nchi nzima wakiwaambia ukweli wananchi? Let's wait and see.
 
madaraka matamu sana, wamekwishaona 2015 itakuwa ngumu kwao, so wanajitutumua huenda wakatengeneza mwanya mwingine wa uchakachuaji!
 
Hawa CCM siku zote wako nyuma ya wakati. Hoja za mafisadi wa tz walishasema mpaka wamechoka, we have already concluded kuwa CCM hawawezi kutatua hili tatizo. Ndo maana watu wengi wakawapa kura CDM.

Right now tunaongelea gharama za maisha, kushuka kwa elimu nk, wao ndo wanaamka na kusema hatuwataki mafisadi. Of course these things are interrelated, but in my opinion, CCM has lost all the credibility and trust of the people especially those "the educated" ones that they want to attract back to the party. It's too late, unless something extraordinary happens, the damage is beyond repair.
 
Mkuu hawa jamaa wajanja sana, sasa hivi wanapiga kelele hawawataki mafisadi lakini wakijua kwamba 2015 hawa hawa wanaowapigia kelele ndio watawafuata kwa ajili ya michango ya fedha za kofia, kanga, fulana n.k.

Kwa sasa wanachama 5 kati ya 100 ndio wanalipia ada zao za kadi sasa pesa za kujiendesha na kupiga kampeni watapata wapi zaidi ya kwa MAFISADI? Wakati wa mkutano wa uchaguzi wa UVCCM walipewa 500ml na mhindi sasa watawakataa kweli!!!? Ni zuga tu hiyo wanatufanyia...
 
HALAFU UTASIKIA WANASEMA JF WACHOCHEZI BADALA YA KUCHUKUA USHAURI NA KUUTUMIA! huuu ndo upuuzi wa viongozi wa ccm!
 
Vyombo vya habari vimelipigia kelele swala la ufisadi kwa muda mrefu sana, miaka. Ilifikia wakati CCM wakasema "kwani vyombo vya habari hamna mambo mengine ya kuandika, kila siku ufisadi ufisadi". Leo ndo wanakumbuka shuka wakati kumeshakucha. Wasubiri hukumu yao 2015 kama watafika salama.
 
Karibuni tu mwisho wao utafika. Njia ya mwongo si ndefu. Za mwizi sio 50. Giza limeendelea sana kwa lazima mwanga wa mapambazuko uonekane
 
Lini watanzania wataacha heshima ya woga?lini watanzania watasimama na kusema uonevu,unyanyasaji, n.k basi?lini watanzania watakuwa wazalendo kamili?lini haki ya wananchi itapatikana?
 
Back
Top Bottom