The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,002
- 19,449
Nimejaribu kufuatilia hiki kitu kinaitwa utumbuaji majipu toka umeanza nimeona umejawa na chuki pamoja na unafiki wa hali ya juu.
Nitatoa mifano miwili kuonyesha utumbuaji huu wa majipu ni wa unafiki wa kiwango gani.
Mwaka jana rais alivunja bodi ya wakurugenzi ya TRA kwa kila alichokuja kukisema badae kuwa ilibariki ufunguaji wa Fixed Deposit Account katika mabenki ya kibiashara.
Tunajua kabisa wazo la kufungua Fixed Deposit Account lazima lilitoka katika menejimenti ya TRA na bodi ikalibariki, mkuu wa menejiment ya TRA ni kamishina ambae pia ni katibu wa bodi ya wakurugenzi, mara nyingi kama sio zote katibu wa bodi hupeleka mapendekezo ya menejimenti ya taasisi yake kwenye bodi ili yapewe baraka.
Cha kushangaza, bodi ikavunjwa kwa msingi kua iliruhusu ufunguaji wa Fixed Deposit Account huku muasisi wa hilo wazo kamishina na menejimenti yake wakiachwa wale bata mjini.
Juzi mkurugenzi wa TANESCO amefukuzwa kazi kwa kigezo kua yeye ndie alieanzisha/asisi wazo la kupandisha umeme bei pamoja na menejiment yake ambayo pia imevunjwa, maana yake ni kwamba bodi ilibariki tu mapendekezo ya menejimenti ya TANESCO.
Hapo ndio unafiki na chuki zinapokuja, hapa kwa TANESCO tunaona muasisi wa wazo alifukuzwa kazi na waliobariki(bodi+EWURA) wakiachwa. TRA muasisi wa wazo(kamishina) akaachwa waliobariki wazo la kamishina(bodi) wakafukuzwa kazi.
Hakuna mtiririko ulio wazi wa kutumbua majipu, utumbuaji umejaa unafiki na chuki, unajiuliza au kwa vile bodi ya TRA hakuwa ameiteua yeye na kamishana kamteua yeye, mkurugenzi wa TANESCO hakumteua yeye na bodi ya TANESCO ameiteua yeye?