Unafiki au Ulimbukeni?

Ndugu zangu;
Kuna mtu alikuwa analalamika kwamba serikali imesababisha bei ya bia kupanda toka 900/-TZS mpaka 1,500/-2004 to 2010.Nikamuuliza bei ya soda ya Coke nchini Kenya,Afrika Kusini au Marekani ilkuwa kiasi gani mwaka 2004 na leo ni kiasi gani???

Hizi ni siasa,ulimbukeni au ushabiki???Mfumuko wa bei katika ulimwengu wa utandawazi serikali ya ndani pekee ndo huwajibika??Au ni sisi tunawajaza ndugu zetu maarifa na taarifa nusunusu.????

Tutazidi kuachwa kwa style hii.

In 2004 12-pack Heinnekken was 9.95 plus tax.
As of today it's 9.99 plus tax

I don't know about Coke!
 
Someni swali ndugu.!!
Mkuu tumelisoma ndio maana nimesema kwa kulinganisha na swali lako ambalo sidhani kama umezungumzia bei ya Heineken Bongo jinsi ilivyopanda kulinganisha na nchi ulizotaja.

Hata hivyo wewe mwenyewe unaweza kuangalia hiyo bei ya Heineken mwaka 2004 imepanda senti 0.4 (9.95 - 9.99) kwa chupa sita, na mara nyingi utakuta wao hicho kiasi kilichopandisha kimetokana na ongezeko la kodi na sio mfumko wa bei.

Lakini njoo kwetu Bongo, bei zinapanda kiholela tu yaani bia itoke Tsh 900 hadi kufikia Tsh 1,500 inakupa picha tofauti kabisa. Hasa ikiongozwa na kushuka kwa thamani ya Tsh ambayo mwaka 2004 ilikuwa Tsh 1000 kwa dollar moja na leo hii tunazungumzia Tsh 1,500 kwa dollar. Na bila shaka bidhaa karibu zote za kutengenezea bia zinaagizwa toka nje. Ndio haya matokeo tunayoyazungumza kila siku ya kutegemea imports..

Kwa hiyo ukitazama kwa kutumia dollar mwaka 2004 bei ya bia ilikuwa chini kidogo ya dollar moja yaani Tsh 900 na leo hii bei ya bia moja ni dollar moja. Sasa kwa Mzalendo Mtanzania ambaye anatumia hela za madafu na mshahara sawa na thamani ya Tsh iliyoshuka hali vitu vikipanda kwa thamani ya dollar ndio maana wanalalamika. Toka wakati wa Mwinyi thamani ya Tsh. Pato la mwananchi (mishahara) hupanda kwa asilimia 20 hadi 30 tu..
 
Mkuu tumelisoma ndio maana nimesema kwa kulinganisha na swali lako ambalo sidhani kama umezungumzia bei ya Heineken Bongo jinsi ilivyopanda kulinganisha na nchi ulizotaja.

Hata hivyo wewe mwenyewe unaweza kuangalia hiyo bei ya Heineken mwaka 2004 imepnada senti 0.4 kwa chupa sita na mara nyingi utakuta kwamba hicho kiasi kilichopandisha kimetokana na kodi na sio mfumko wa bei. Lakini njoo kwetu Bongo, bei zinapanda kiholela tu yaani bia itoke Tsh 900 hadi kufikia Tsh 1,500 inakupa picha tofauti kabisa. Hasa ikiongozwa na kushuka kwa thamani ya Tsh ambayo mwaka 2004 ilikuwa Tsh 1000 kwa dollar moja na leo hii tunazungumzia Tsh 1,500 kwa dollar. Na bila shaka bidhaa zote za kutengenezea bia zinaagizwa toka nje.

Kwa hiyo ukitazama kwa kutumia dollar mwaka 2004 bei ya bia ilikuwa chini kidogo ya dollar moja yaani Tsh 900 na leo hii bei ya bia moja ni dollar moja. Sasa kwa Mzalendo Mtanzania ambaye anatumia hela za madafu na mshahara sawa na thamani ya Tsh iliyoshuka hali vitu vikipanda kwa thamani ya dollar ndio maana wanalalamika. Toka wakati wa Mwinyi thamani ya Tsh. Pato la mwananchi (mishahara) hupanda kwa asilimia 20 hadi 30 tu..

Labda pia tujaribu kufikiri ni kwa nini bidhaa zote za uzalishaji tunaagiza kutoka nje.
 
Labda pia tujaribu kufikiri ni kwa nini bidhaa zote za uzalishaji tunaagiza kutoka nje.
Hakuna sababu zaidi ya ULIMBUKENI kama ulivyosema kwani wakati wa Nyerere baadhi ya vitu vilikuwa vikizalishwa hapa hapa nchini.. Sasa iweje tuliweza wakati wa Ujamaa na njaa kali kushusha bei ya bia leo tukiwa huru kiuchumi tunashindwa.

Basi tu mkuu wangu sisi ni Malimbukeni kuja kwa Utandawazi umetuingiza uvivu wa ajabu na kuwa taifa tegemezi..hata vyoo vya kukaa na glass za maji vinavyotengenezwa kwa mchanga na Udongo tunaagiza toka China. Ni wavivu wa kufikiri hatupendi taabu za kuuchosha Ubongo, ikiwa mali inapatikana kutoka China at very low price ambayo wenye nchi they can afford, why bother!
 
Hakuna sababu zaidi ya ULIMBUKENI kama ulivyosema kwani wakati wa Nyerere baadhi ya vitu vilikuwa vikizalishwa hapa hapa nchini.. Sasa iweje tuliweza wakati wa Ujamaa na njaa kali kushusha bei ya bia leo tukiwa huru kiuchumi tunashindwa.

Basi tu mkuu wangu sisi ni Malimbukeni tumeingia Utandawazi umetuingiza uvivu wa ajabu na kuwa taifa tegemezi..hata vyoo vya kukaa na glass za maji vinavyotengenezwa kwa mchanga na Udongo tunaagiza toka China. Ni wavivu wa kufikiri hatupendi taabu za kuuchosha Ubongo hali mali inapatikana kutoka China at very low price ambayo wenye nchi they can afford!

Unadhani Azimio la Zanzibar mwaka 1994 lilikuwa kosa la CCM au la Jamii nzima ya wasomi na wananchi wote wa Tanzania?
 
Unadhani Azimio la Zanzibar mwaka 1994 lilikuwa kosa la CCM au la Jamii nzima ya wasomi na wananchi wote wa Tanzania?
Azimio la Zanzibar halikuwa kosa la CCM kwani CCM wenyewe walitaka iwe hivyo ili wapate kujitajirisha wao kutokana na kulitumikia Taifa letu kwa miaka 24 ya Nyerere na Ujamaa wakabakia maskini wasio kuwa na mali ya kujilinda pindi nchi ikiingia Ubepari.

Azimio la Zanzibar halikubadilisha kitu chochote zaidi ya kuwaongezea viongozi kofia mbili, uwezo wa kufanya biashara hata kama kuna conflict of interest hawakujali tena maslahi ya nchi isipokuwa Binafsi..Na huwezi kuwalaumu jamii nzima ya wasomi kwani wao walikuwa hawana sauti kuanzishwa kwa Azimio la Zanzibar kwani (kumbuka) Azimio hilo lilitangulia kuanzishwa kwa vyama vingi..

Kwa hiyo CCM waliamua haya mbele ya mabadiliko yoyote ya Kisiasa na walijua sasa ni wakati wao wa kuchuma. Kifupi Ufisadi uliopo nchini ni matunda ya Azimio la Zanzibar ambalo kisheria tumeshindwa kuwafikisha mahakamani viongozi wengi waliokiuka miiko na maadili ya Uongozi lakini wakilindwa na Azimio la Zanzibar ambalo lilikwekwa na chama tawala.
 
Azimio la Zanzibar halikuwa kosa la CCM kwani CCM wenyewe walitaka iwe hivyo ili wapate kujitajirisha wao kutokana na kulitumikia Taifa letu kwa miaka 24 ya Nyerere na Ujamaa wakabakia maskini wasio kuwa na mali ya kujilinda pindi nchi ikiingia Ubepari.

Azimio la Zanzibar halikubadilisha kitu chochote zaidi ya kuwaongezea viongozi kofia mbili, uwezo wa kufanya biashara hata kama kuna conflict of interest hawakujali tena maslahi ya nchi isipokuwa Binafsi..Na huwezi kuwalaumu jamii nzima ya wasomi kwani wao walikuwa hawana sauti kuanzishwa kwa Azimio la Zanzibar kwani kubmbuka tu Azimio hilo lilitangulia kuanzishwa kwa vyama vingi..

Kwa hiyo CCM waliamua haya mbele ya mabadiliko yoyote ya Kisiasa na walijua sasa ni wakati wao wa kuchuma. Kifupi Ufisadi uliopo nchini ni matunda ya Azimio la Zanzibar ambalo kisheria tumeshindwa kuwafikisha mahakani viongozi wengi waliokiuka maadili ya Uongozin lakini wakilindwa na Azimio la Zanzibar ambalo lilikwekwa na chama tawala.

Kwa hiyo CCM ina kosa?Then kushindwa kuwaadhibu wahusika ni tatizo la CCM,katiba au jamii yetu?
 
Kwa hiyo CCM ina kosa?Then kushindwa kuwaadhibu wahusika ni tatizo la CCM,katiba au jamii yetu?
Bila shaka CCM ina kosa tunapozungumzia Uongozi bora. CCM wana makosa tukitumia jicho la wananchi kwa maslahi ya Taifa kwani Kuanzishwa kwa Azimio la Zanzibar kama ingekuwa nchi nyingine, CCM ingekwisha ondolewa zamani ktk chaguzi za mwanzo na nafikiri wananchi walitambua haya mwaka 1995 kiasi kwamba Mrema aliweza kushinda lakini walibadilisha matokeo na pengine Nyerere aliweza kukisetiri chama kwa kumpigia debe Mkapa. Mrema hakufanya kampeni kali kama miaka hii ya karibuni lakini aliweza kuweka upinzani mkali sana bila hata kutembelea vijiji au mikoa mingi.

Kushindwa kuwaadhibu wahusika haiwezi kuwa kosa kwa jicho la CCM kwa sababu ndicho walichotaka kufanya walipoanzisha Azimio la Zanzibar. Kila wanalofanya leo wanaliona ni haki yao kufanya hivyo yaani viongozi wetu wanayo nafasi sawa ya kujitajirisha hata kama watatumia wadhifa wao. CCM hawaoini Uharamu wa wahusika kwa sababu ni wao wanaofanya vitendo hivi makusudi kujitajirisha.. Uharamu wa vitendo hivi vinavyokiuka miiko na maadili ya uongozi vinaonekana tu kwetu sisi wananchi na pengine nchi za nje ambazo wanashangaa kuona Waziri akiwa na mradi wake ndani ya wizara anayoongoza. Waziri wa Utalii ana agency ya Utalii akiwaweka watu kumtumikia kwa niaba yake, hili halipo nchi nyingine yeyote lakini kwetu jambo kaa hili halina haramu.

Tatizo ni CCM, na pengine naweza kusema tatizo kubwa ni mwalimu Nyerere mwenyewe aliyetuachia viongozi wabovu kurithi utawala wenye nguvu kubwa ajabu...Toka balozi wa nyumba kumi, kata, wilaya, mkoa hadi mawaziri wote walikuwa wanachama wa CCM damu. Polisi, wanajeshi, CEO, makatibu wakuu na nyadhifa zote za uongozi wa juu zilikuwa chini ya wanachama wa CCM, ambao baada ya kuanzishwa vyama vingi walikataa kukivunja chama hiki kwanza ili kuunda vyama vyenye itakadi tofauti. Hivyo matokeo yake tunaongozwa na vichwa vya watu na sio Itikadi na ndio maana utaona sera zote za vyama vilivyojiandikisha vinafanana sana ktk utekelezaji wake. Tofauti kubwa zilizopo ni Vipaumbele lakini hawana tofauti ya kijamii ktk mtazamo wa maswala magumu. CCM ni kila kitu unachoweza kufikiria ndiye mrithi wa mali zote za nchi hii.

Kifupi, Hili sio tatizo la CCM isipokuwa CCM ndiye tatizo. Ni jukumu la wananchi kuelewa hivyo na hata waliomo ndani ya CCM wanatakiwa kuamka na kusema hapana hii habari ya kupuuza miiko na maadili ya uongozi ni lazima yafe. Ni jukumu letu sote Watanzania wenye nia nzuri na Taifa kwani Katiba itaweza tu kubadilishwa na sisi tunaopinga huko tunakoelekea lakini mwanzo ni kutokubaliana na hawa viongozi waliopo leo madarakani wapate kuelewa haramu wanazozifanya. Tuache ushabiki au Ulimbukeni, tufikirie zaidi hatma ya nchi yetu kwani Ubinafsi hata siku moja hauwezi kulikomboa taifa isipokuwa kuligawa na mwisho wake kuangamia kwa kukosa dira kama ilivyokuwa Somalia.. nani alifikiria Somalia ingekuwa hivi ilivyo leo?
 
My question is how strong is the civil society in Tanzania?Hili si tatizo la CCM ni tatizo la jamii!!Chama kiko madarakani na kinafanya mambo jinsi jamii inavyokichukulia.
 
Hujajibu swali.

Kwa serikali chovu kama hii ya CCM imeshindwakubuni vyanzo vipya vya mapato na badala yake kila mwaka kodi inaongezwa kwenye bidhaa za vileo na vinywaji baridi na sigara, Tandale one wewe ni kilaza kweli na kwa taarifa yako ndio maana wananchi wanakamuliwa zaidi kwenye bia, soda na sukari, uliza pale TBL kama isingekuwa kodi za serikali ya CCM basi bia inatakiwa kuuzwa Tshs. 680.
 
Kuna uwezekanao kabisa serikali moja kupandisha bei ya bidhaa fulani ili kurekebisha bajeti yake. Hii hutokea sana katika nchi zzenye vyanzo finyu vya kongeza mapato ya serikali. Hivyo kulinganisha kiwango cha kuongezeka kwa bidhaa nchi tofauiti kutaonyesha jinsi serikali hiyo inavyotegemea chanzo hicho. Kwa mfano wako huu wa soda, mimi naishi EU, bei ya coke ya kopo ml 300 ilikuwa euorcent 49 2004 na sasa ni cent 54. Kwa hiyo jibu lako kuhusu kuongezeka kwa bidhaa za mlaji sehemu nyingi zimeongezeka. Mkate toka cet 49 mpaka cent 62 huku niishiko. sasa Tanzania mkate ni bei gani au umeongezeka vipi wewe unajua. Kama unafuatilia mabo ya uchumi pale mafuta yalipopanda sana nchi za magharibi waliutaka OPEC kuongeza uzalishaji ili bei ipungue., demand vs supply principle. OPEC walikataa kwa kuziambia nchi zipunguze kodi inayotozwa kwenye mafuta kwani nchi nyingine kodi ilifikia 70%. Wakagoma kusikiliza ushauri huo na bei ikapungua kwa kuwa speculants walijua imefika kikomo. Kwa maana hiyo serikal zinachangia mwongezeko wa bei wa bidhaa fulani fulani ilikuziba nakisi kwenye bajeti zao. Kila nchi ina economic indicator zake, zinazofuatwa na Marekani au THE Gx zaweza kutokuwa na maana kwenye uchumi wetu, japo kutokana na utegemezi wetu zinaweza kuleta nakisi kwenye bajeti yetu na kusababisha Mfumuko wa bei. Matumizi yasiyo na sababu au udhibiti mbovu wa mapato kwa serikali iliyoko madarakani unachangia kuleta mfumuko wa bei. Ushabiki au la serikali yeyote lazima ichague je uchumi utaongoza siasa au siasa itaongoza uchumi. Uchumi ukiongoza siasa kuna uhakika wa kukua au kuwa stable. Mfano Kenya kama siasa ingeongoza uchumi machafuko ya kisiasa yaliyotokea yangewaacha pabaya. Siasa kuongoza uchumi , mfano Tanzania toka vita ya Nduli hatujatengemaa wala kuzinduka kutoka kwenye mtizamo huo
 
Kwa serikali chovu kama hii ya CCM imeshindwakubuni vyanzo vipya vya mapato na badala yake kila mwaka kodi inaongezwa kwenye bidhaa za vileo na vinywaji baridi na sigara, Tandale one wewe ni kilaza kweli na kwa taarifa yako ndio maana wananchi wanakamuliwa zaidi kwenye bia, soda na sukari, uliza pale TBL kama isingekuwa kodi za serikali ya CCM basi bia inatakiwa kuuzwa Tshs. 680.

Kipi bora basi?Kupanua wigo wa kodi za ndani au kuongeza utegemezi wa bajeti kwa wahisani?
 
Back
Top Bottom