Siku moja nilitoka mkoani kuja Dar nikiendesha gari, nilikuwa peke yangu. Kwa sababu ya Uchovu nilipofika Chalinze nilizidiwa na uchovu na ilikuwa usiku sana. Nikahofia naweza kusababisha ajali kwa sababu usingizi ulikuwa umenizidi sana kiasi cha kushindwa kuvumilia, nikaona isiwe tabu, nikaamua kulala chalinze, japo asubuhi saa mbili nilikuwa na appointment jijini kwenye ofisi fulani. Nikaamua kuwa alfajiri nitaamka saa kumi ili kukipambazuka niwe Dar tayari.
Alfajiri, Nikiwa nakaribia Kibaha maili moja tayari pilika pilika za magari na daladala zilikuwa zimeanza japo magari ni machache. Nikafika sehemu (jina limenitoka), ila ni kabla ya Kibaha maili moja, nikakuta watu barabarani wanasubiri usafiri, Wakanisimamisha, Wakaniomba wachangie nauli maana daladala hazitokei alafu kulikuwa na hali ya mvua basi nikawatajia amount niliyotaka la sivyo niwaache. Wakawa tayari kulipa basi wakapanda wanawake wawili na wanaume wawili. Mgawanyo huo wa jinsia ulilinifanya nijiulize maswali ya tafakuri..
Basi tukachangamsha njia na story za hapa na pale, nikapiga swali la kizushi wanaenda wapi muda huu mbona mapema kwenda kazini? Wakanijibu, hatuendi kazini iLa tumetoka kazini. Nikaanza kudadisi, dada mmoja akasema tumetoka River road (sijui kama niko sahihi, au nimesahau)..., Nikamwambia ndo nini? akiwa anataka kusema, mwenzake akamkatiza na kumkaripia kwa nini anasema sema hovyo anataka watu wajue kazi wanayofanya? Basi mimi nikapotezea tukaendelea na safari.
Jamani wakati wengine tunaenda kazini kumbe wengine wanarudi kulala.
Wenyeji wa maeneo hayo mnaweza kunirekebisha kama nilikosea jina la hiyo sehemu, bila shaka itakuwa night club/bar au starehe ya namna fulani. Karibuni muweke mambo sawa, pia tuambieni nini kinaendelea huko?