Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,198
- 7,539
Unapoangalia nje kupitia dirisha la kioo, kuna vitu vingi vinavyoweza kuonekana. Hata hivyo utakachokiona itategemeana na dhamira, malengo na hali ya kifikra uliyonayo kwenye kichwa chako.
Kupitia kwenye dirisha hilo hilo, kuna atakayeona majengo mazuri, kuna atakayeona jinsi jua linavyochomoza, kuna atakayeona maji, kuna atakayeona kizunguzungu kama anataka kudondoka, kuna atakayeona kama jengo linadondoka kuna atakayeona kioo kina mpasuko n.k Yaani kwa Ujumla kila mmoja ataona vile alivyoji “ tune” kuona na hapo ndipo kufanikiwa au kufeli huanzia.
Kwa bahati mbaya, Watanzania tuliowengi kila tunapochungulia kwenye dirisha la nyumba yetu; hakuna tunachoona zaidi ya mipasuko iliopo kwenye kioo. Yaani kila anayechungulia anarudi kuwaambia wenzake hivi mshachungulia dirishani? Kuna mipasuko pale kwenye kioo halafu kama inaendelea vile!? kisha kila mtu anarudi ndani na kuwatisha wenzake na wote wanaungana kuogopa "creaks" kwenye kioo na baada ya hapo wote wanarudi ndani huku wakiwashawishi wale wanaoona possible opportunities nao waone creaks dirishani kisha wa - concentrate hapo tu!
Ni kweli inawezekana kuwe na mipasuko lakini hiyo haikufanyi usione vitu vingine vizuri kupitia dirisha hilo hilo na kufikiria namna ya kuvitumia vile uvionavyo kwa manufaa yako na ya wengine wakati pia unafikiria ni kwa vipi utakabiliana na mpasuko bila kuharibu dirisha.
Nitoe mfano kwenye Sekta ya Elimu. Zilivyoanzishwa shule za kata; walikuwepo watu miongoni mwetu ambao walizipinga sana kuwa hazifai kabisa wakasema "ma" –CCM yanapoteza muda. Hoja yao ilikuwa kwamba hazina waalimu, hazina madawati hazina maabara n.k na hivyo wakahitimisha kuwa hizo si shule bali ni bomu. Badala ya kuona zaidi positive side and possible opportunities zilizokuwepo kwenye shule hizo na kushauri namna ya kuzitumia na kuboresha panapostahili, wao walikuwa wanaona vikwazo tu na hivyo kuwakatisha tamaa wengine. Sasa leo watu wangapi wamenifaika na shule hizo?
Sasa ni shule hizo hizo ambazo wengine waliona zaidi positive side na wakazitumia vizuri na wengine sahizi wana Phd’s. Wengine hawana Phd’s lakini wana elimu ambayo imewasaidia kuwa na na mchango muhimu kwenye nchi hii na Miongoni mwa wanafaika wa shule hizi ni mimi mwenyewe na zisingekuwepo nisingezoma.
Kwa hiyo kama Nchi tuna changamoto nyingi, CCM wanafanya mambo mengi mazuri tu ila changamoto nazo bado zipo nyingi. Hata hivyo hakuna namna ambayo tunaweza tusipite kwenye changamoto kwa sababu hivyo ndivyo dunia ilivyo. Ili ufanikiwe lazima Pia ufeli wakati mwingine, upite kwenye maumivu na sulubu mbalimbali. Ndio maana unaona Nyerere alilaumiwa kwa mambo mengi sana, kadhalika Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Sasa Rais Magufuli licha ya kwamba hawa wote wana staili tofauti za ku approach mambo mbali mbali.
Kwa hiyo, inafaa tuwe tunaona ni fursa gani ambazo kupitia mazinngira yaliyopo na sera hizi hizi za CCM tunaweza kuzitumia kuifanya Tanzania kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi. Pale ambapo kuna changamoto, tuwe “optimists” kwa kuchangua njia ambayo angalau inaweza kuwa na matokeo bora zaidi.
Kwa mfano, kama unaona mwenzako si mwana demokrasia wa kweli, hiyo kwako ni fursa ya wewe kuwa mwana demokrasia ili uwe mfano. Kama unaona mwenzako hana utu, huruma, ubinadamu, Kama unaona mwenzako ana lugha za kuudhi, basi wewe kuwa na lugha nzuri ili watu wajifunze kwako n.k wewe kuwa kinyume chake. Tujifunze kuangalia mambo kwa jicho positive na tutaona fursa nyingi ambazo tukizitumia vizuri kwa pamoja tunaweza kuifanya Tanzania kuwa nchi bora zaidi na ni katika msingi huo tunaweza kupata maendeleo ya kweli.
Ukiona kila ukitazama kwenye dirisha la kioo wewe unachoona ni mipasukopasuko tu, ujue una tatizo kubwa kwenye mfumo wako wa kufikiri na hiyo ndio huitwa “Pessimism” .Tuangalieni ni vitu gani ambavyo vinaweza kutusaidia kupiga hatua badala ya kung’ang’ania kuzungukia kwenye kamduara ambako hakatusaidii.
Hata nchi zilizoendelea ambazo wengi hupenda kukimbilia, uzuri wake ni matokeo ya staili za kufikiri za watu wake.