Unachoona ni mipasuko kwenye dirisha la kioo!?

Unachoona ni mipasuko kwenye dirisha la kioo!?

Ahsante sana Mkuu "...Kwa mfano, kama unaona mwenzako si mwana demokrasia wa kweli, hiyo kwako ni fursa ya wewe kuwa mwana demokrasia ili uwe mfano. Kama unaona mwenzako hana utu, huruma, ubinadamu, Kama unaona mwenzako ana lugha za kuudhi, basi wewe kuwa na lugha nzuri ili watu wajifunze kwako n.k wewe kuwa kinyume chake."
 
Ujumbe mzuri kabisa ila umeharibu hapo ulipoanza kuzungumzia ccm!
Unakubuka wazo la shule za kata na jinsi zilivyokuwa zimepata upinzani bila ya wanaozipinga kutoa njia mbadala ya kuwafanya vijana kama sisi tusome? Unakumbuka shule hizo zilivyoanza kwenye mazingira magumu na sasa zilipo? hivi unajua kuna watu ambao ni PHD holders sasa na ni products ya shule hizo? unajua kuna wengine wanafanya kazi mpaka UN na ni product ya shule hizo?
 
Ila kitu kingine pengine nikuelimishe tu, huwa kwa kawaida mada zenye wachangiaji wengi ni zile zisizokuwa na mashiko, kwa hiyo unapoleta mada usilete ili upate wachangiaji wengi bali ili ufikishe ujumbe unaodhani ni sahihi na muhimu. Ushiishi kwa kupenda kushangiliwa na mob Psychology.

Hii ndio raha ya demokrasia unamwagika upendavyo. Kama ni hivyo usemavyo hiyo Injili na Quran haikuwa na haja ya kusambazwa dunia nzima, kwani zingebaki hapo zilipoanzia bado ingekuwa sawa tu. Mambo ni watu. Sipingi kwamba zisizo na mashiko ndio zenye wachangiaji, ila hii yako umejuaje ina mashiko? Na kwakuwa unadhani inakonga nyoyo za kundi fulani walipaswa kuichangia, hata wao hawachangii. Sasa unatarajia vipi huo ujumbe wako kufikia watu? Punguza baadhi ya vionjo ili upate wote, kinyume na hapo utabaki kila post yako kuwataja wanaokupuuza kama sehemu ya kupata wachangiaji.
 
Kwasababu ina scientific logic na mimi ni moja ya mnufaika wa ninachokizungumzia.

Mkuu hata wale wanaopata wachangiaji wengi hata kama ni udaku hudhani wana hoja ya maana ndio maana hupata wachangiaji wengi. Tunatofautiana mitazamo.
 
wao hawachangii. Punguza baadhi ya vionjo ili upate wote.
Mkuu, ushauri wangu kwako, kwenye maisha yako usifanye vitu ili watu wakushangilie, Fanya vitu kwa kuwa unaamini unachofanya ni sahihi na nimuhimu kufanya. Ukifanya hivyo utakuwa na nafasi kubwa ya kutojuta kwenye maisha yako, na hata siku ukiwa juu ya kitanda hospitalini ukaambiwa umebakiza siku2 ufe, na ukaulizwa ni nini unajutia kwenye maisha yako au ni nini ambacho ungepewa muda Wa kuishi zaidi ungekifanya tofauti, utajikuta huna LA kujutia.

Jambo hilo LA kutaka kushangiliwa na wengi ndilo limetupoteza na kutufanya tuwe watu Wa ajabu na wanafiki waandamizi.
 
Hongera sana kijana wangu....nimeishamuagiza Pole×2 kwamba mkuu wa mkoa au wilaya yoyote akifa akupachike kwenye nafasi yake fasta. Niko ki-shilawadu zaidi.
 
Kweli mkuu huoujumbe umewaigia walizani ni mashindano wafanyie wananchi wakuchague kipindikijacho siopumba na ma neno ccm juuuu mbelekwambele
 
Unawezaje kuwa na amani kama toka 1961 mpaka 2018 unaona mpasuko ule ule wa maadui watatu ya uduni wa elimu ,umaskini na maradhi! Watu wamesoma kata wana PHD zisizosaidia jamii inayowazunga. Kama unayaona mazuri ilhali watu wa mashariki ya mbali waliokuwa kama sisi miaka ya mwanzoni mwa 1900 wametuacha kiuchumi kifikra na kimaendeleo ,utakuwa na PHD ya shule za kata kweli.
 

Unapoangalia nje kupitia dirisha la kioo, kuna vitu vingi vinavyoweza kuonekana. Hata hivyo utakachokiona itategemeana na dhamira, malengo na hali ya kifikra uliyonayo kwenye kichwa chako.

Kupitia kwenye dirisha hilo hilo, kuna atakayeona majengo mazuri, kuna atakayeona jinsi jua linavyochomoza, kuna atakayeona maji, kuna atakayeona kizunguzungu kama anataka kudondoka, kuna atakayeona kama jengo linadondoka kuna atakayeona kioo kina mpasuko n.k Yaani kwa Ujumla kila mmoja ataona vile alivyoji “ tune” kuona na hapo ndipo kufanikiwa au kufeli huanzia.

Kwa bahati mbaya, Watanzania tuliowengi kila tunapochungulia kwenye dirisha la nyumba yetu; hakuna tunachoona zaidi ya mipasuko iliopo kwenye kioo. Yaani kila anayechungulia anarudi kuwaambia wenzake hivi mshachungulia dirishani? Kuna mipasuko pale kwenye kioo halafu kama inaendelea vile!? kisha kila mtu anarudi ndani na kuwatisha wenzake na wote wanaungana kuogopa "creaks" kwenye kioo na baada ya hapo wote wanarudi ndani huku wakiwashawishi wale wanaoona possible opportunities nao waone creaks dirishani kisha wa - concentrate hapo tu!

Ni kweli inawezekana kuwe na mipasuko lakini hiyo haikufanyi usione vitu vingine vizuri kupitia dirisha hilo hilo na kufikiria namna ya kuvitumia vile uvionavyo kwa manufaa yako na ya wengine wakati pia unafikiria ni kwa vipi utakabiliana na mpasuko bila kuharibu dirisha.

Nitoe mfano kwenye Sekta ya Elimu. Zilivyoanzishwa shule za kata; walikuwepo watu miongoni mwetu ambao walizipinga sana kuwa hazifai kabisa wakasema "ma" –CCM yanapoteza muda. Hoja yao ilikuwa kwamba hazina waalimu, hazina madawati hazina maabara n.k na hivyo wakahitimisha kuwa hizo si shule bali ni bomu. Badala ya kuona zaidi positive side and possible opportunities zilizokuwepo kwenye shule hizo na kushauri namna ya kuzitumia na kuboresha panapostahili, wao walikuwa wanaona vikwazo tu na hivyo kuwakatisha tamaa wengine. Sasa leo watu wangapi wamenifaika na shule hizo?

Sasa ni shule hizo hizo ambazo wengine waliona zaidi positive side na wakazitumia vizuri na wengine sahizi wana Phd’s. Wengine hawana Phd’s lakini wana elimu ambayo imewasaidia kuwa na na mchango muhimu kwenye nchi hii na Miongoni mwa wanafaika wa shule hizi ni mimi mwenyewe na zisingekuwepo nisingezoma.

Kwa hiyo kama Nchi tuna changamoto nyingi, CCM wanafanya mambo mengi mazuri tu ila changamoto nazo bado zipo nyingi. Hata hivyo hakuna namna ambayo tunaweza tusipite kwenye changamoto kwa sababu hivyo ndivyo dunia ilivyo. Ili ufanikiwe lazima Pia ufeli wakati mwingine, upite kwenye maumivu na sulubu mbalimbali. Ndio maana unaona Nyerere alilaumiwa kwa mambo mengi sana, kadhalika Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Sasa Rais Magufuli licha ya kwamba hawa wote wana staili tofauti za ku approach mambo mbali mbali.

Kwa hiyo, inafaa tuwe tunaona ni fursa gani ambazo kupitia mazinngira yaliyopo na sera hizi hizi za CCM tunaweza kuzitumia kuifanya Tanzania kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi. Pale ambapo kuna changamoto, tuwe “optimists” kwa kuchangua njia ambayo angalau inaweza kuwa na matokeo bora zaidi.

Kwa mfano, kama unaona mwenzako si mwana demokrasia wa kweli, hiyo kwako ni fursa ya wewe kuwa mwana demokrasia ili uwe mfano. Kama unaona mwenzako hana utu, huruma, ubinadamu, Kama unaona mwenzako ana lugha za kuudhi, basi wewe kuwa na lugha nzuri ili watu wajifunze kwako n.k wewe kuwa kinyume chake. Tujifunze kuangalia mambo kwa jicho positive na tutaona fursa nyingi ambazo tukizitumia vizuri kwa pamoja tunaweza kuifanya Tanzania kuwa nchi bora zaidi na ni katika msingi huo tunaweza kupata maendeleo ya kweli.

Ukiona kila ukitazama kwenye dirisha la kioo wewe unachoona ni mipasukopasuko tu, ujue una tatizo kubwa kwenye mfumo wako wa kufikiri na hiyo ndio huitwa “Pessimism” .Tuangalieni ni vitu gani ambavyo vinaweza kutusaidia kupiga hatua badala ya kung’ang’ania kuzungukia kwenye kamduara ambako hakatusaidii.

Hata nchi zilizoendelea ambazo wengi hupenda kukimbilia, uzuri wake ni matokeo ya staili za kufikiri za watu wake.
Ukweli ndo huu
 
Unawezaje kuwa na amani kama toka 1961 mpaka 2018 unaona mpasuko ule ule wa maadui watatu ya uduni wa elimu ,umaskini na maradhi! Watu wamesoma kata wana PHD zisizosaidia jamii inayowazunga. Kama unayaona mazuri ilhali watu wa mashariki ya mbali waliokuwa kama sisi miaka ya mwanzoni mwa 1900 wametuacha kiuchumi kifikra na kimaendeleo ,utakuwa na PHD ya shule za kata kweli.
Kwa hiyo wenye PHD ambao hawana impact kwenye jamii ni wale waliosoma shule za kata na waliosoma shule nyingine wana PHD na pia wana impact kwenye jamii? usipinge vitu tu ili mradi upinge.

Hoja yangu ni kwamba inapotokea chama, serikali au hata mtu aka innovate wazo linalolenga kutatua tatizo fulani nchini, badala ya kukatishana tamaa, tunatakiwa tuangalie possible opportunities zilizopokwenye wazo hilo na kuzitumia kwa maslahi ya wote na ikibidi tuboreshe badala ya kukatishana tamaa ili tubaki pale pale.
 
Tatizo wengi wenu hamna mnachowaza zaidi ya siasa za madaraka. Shida watu hawaelewi kwamba ili uwe kiongozi si lazima uwe rais, hapo ulipo tayari wewe ni kiongozi na unaweza ukafanya mambo mengi mazuri kwa manufaa ya jamii ya mwanadamu na nchi yako kwa ujumla. Hivi unajua U.A.E inaongozwa na mfalme?
Mleta post wewe akili zako zimejaa CCM tu kichwani huna unalowaza zaidi ya kutetea chama Tawala

Hoja za shule za kata kila mtu anajua uwezo wa hao watu wa kufikiri, Tambua shule sio kumaliza na kujaza makaratasi kama vyeti, Shule unaenda kupata maarifa ili yakusaidie kupambana na mazingira yanayobadilika na kuisaidia jamii husika toka hatua moja ya maendeleo kwenda nyingine

Leo hii wanafunzi hawa wa kata ukimpa afanye kazi hata kwa kiswahili anachoandika bora mtoto wangu wa kindegatan tunaweza hata piga story zake za katuni kuliko hawa graduate wa kata

Kama kuna mtu yupo vizuri kichwani na kutumia vizuri elimu tambua wengi familia zao zinajiweza

Wewe shule za kata zimekufanya ufikiri upande mmoja wa ccm tu hujui kinachoendelea huko Davos wanakojadili uchumi

I stick you are idiot on Economic and Political perspective, Punguza Povu shule sio kujaza makaratasi ya Toilet paper au kuwaza chama kama wewe
Shame on you
 
Wewe shule za kata zimekufanya ufikiri upande mmoja wa ccm tu hujui kinachoendelea huko Davos wanakojadili uchumi
1. Any way wewe umesoma shule gani kwanza na ni nini kinachoashiria kuwa uwezo wako wa uelewa wa mambo na kukabiliana na mazingira ili kuleta matokeo bora zaidi ni mkubwa kuliko wengine ?

2. Haujui kuwa CCM ndicho chama kinachoongonza kwa kuwa na able bodied and competent Human resources kwenye field ya uongozi? Rejea hapa,
Rasilimali watu ndani ya vyama vya siasa

Davos kuna nini kinachohusiana na mada hii, na unataka tufanye nini? inawezekana una wazo zuri ila tu hujaweza kulieleza vizuri.
 
Back
Top Bottom