Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,198
- 7,537
- Thread starter
- #61
Ukiacha matukio yatokanayo na nguvu za asili; Yale tuwazayo kwenye akili zetu ndio hutokea na kuwa kweli kwenye ulimwengu wa nje. Tofauti ya kimaendeleo kati ya nchi na chini hutokana na staili ya kufikiri ya wananchi wa nchi husika. Mara nyingi tumekuwa na tafsiri isiyokuwa sahihi juu ya mambo mbalimbali na hivyo kutupelekea kuchukua hatua zisizo sahihi na kupata matokeo yasiyopendeza. Hakuna mtu wa kumlaumu kwa Changamoto tulizonazo watanzania bali sisi wenyewe na tutapiga hatua kwa kadiri tutakavyoamua wenyewe.