!!???Acha uongo jimbo la Biafra mauaji yaliyokuwa yanaendeshwa kule ulitaka viongozi waafrika wakae Kimya? Hafu Biafra na Nigeria kwa ujumla wakatoliki ni wachache sana wengi kule ni waaglikana sawa kijana.
tusidanganyane. tangu miaka nenda rudi wapemba wamekuwa hawapatani na waunguja. na chama cha cuf kimekuwa cha kipemba zaidi. wakati woote huo wamekuwapo kwenye muungano. mbona muungano haujazuia wazanzibar kugombana na kuhasimiana wao kwa wao?Zenji wakijitenga tu,
Imekula kwao.
Ulichosema kuhusu Tanzania ni swa lakini unakumbuka kuwa Wapemba wengi hawautaki muungano au wanataka wa Nkataba atii! lakini upande mwingine waunguja wanaupenda muungano uendelee na udumu, Je hapo huoni kuwa kama muungano usipokuwepo/ukivunjika Unguja na Pemba zitatengana?
Yeah ni kweli bhana ! Unajua Mh JK NYERERE ALIWAHI KUITABIRIA MEMA CDM NA SASA UKWELI UNAENDA KUTIMIA 2015 !
Kwa ufupi Zanzibar inahitaji kujitawala. Hakuna anayefahamu maslahi ya wazanzibari zaidi ya wao wenyewe. Na haiwezekani viongozi wa Tanganyika wakawafahamu wazanzibari kwa kuwa kuna wengi wao hawajawahi kufika chumbe. Wapo pia wazanzibari ambao hawajawahi kufika kizimkazi wakaona mataa ya dar es salamu. Kwa kuwa hakuna mwananchi wa kawaida anayefahamu siri iliyopo ya huu muungano unaolindwa na maBUBU wasiosema sababu za msingi za sisi kuungana mimi naona muungano uondoke halafu baadaye tuone ni nani alikuwa anafaidi na hatimaye tuone kama kunahaja ya kuungana.
Nyerere ni mtu tu aliyewahi kuona TV mapema na kusoma vitabu vya mantiki halafu akasema kama walivyosema wengine. TUACHE MAWAZO YA WATU TUANGALIE UHALISIA WA SASA.
Elimu yenyewe ya madrasa unataka upewe ukurugenzi wapi na wapi? Mkiambiwa mkasome mnasema wanawasengenywa tuwafanyeje? Unadhani huko Omani, Saudia, Iraq, Iran, Misri hawajasoma hiyo elimu mnayoiita elimu dunia? au mnadhani hivyo vyuo vikuu kataika nchi za kiarabu vinafundisha quran? Tatizo lenu mnataka kila kitu kiendeshwe kwa mujibu wa sharia law,
Waafrika atujielewi
Nyerere aliokuwa kiongozi mwenye maono, maneno yake yataendelea kuishi, tusiwasema Sudan peka yao, hata hapa Tanzania tunaelekea huko, kwani tumeyaona mengi, mfano kiongozi anatamka kwenye jukwaa eti chama fulani ni cha dini fulani au cha watu wa kutoak ukanda fulani, hivi huyo kiongozi hajui kwamba anatengeneza chuki? Hivi hiyo dini aua huo ukanda wa hao watu wanapotoka cham chaka hakina wafuasi wala viongozi?
Tunawaona wabunge wanasimama bungeni 'mheshimiwa spika matatizo ya mkoa..... au jimbo... watuachie wenyewe" Watanzania tunabaki tumeduwaa na kujiuliza inamaana huo mkoa hauna maangiliano na mikoa mingine!
nimeipenda hii.mimi binafsi sioni faida ya muungano. wazanzibar wanataka kupata misaada kutoka katika taasisi za kiislamu kama IOC lakini haiwezekani kutokana na muungano. muungano ukivunjika zanzibar itanufaika zaidi. si ajabu baada ya miaka michache ikawa dubai ndogo ya afrika.
Ni kweli watanzania wengi wanajua kuwa Mwl. Nyerere alikuwa na maono ya mbali. Kama ni safari moja Nyerere alikuwa umbali wa km 1000 huku wananchi wake wakiwa km 1. Licha ya watanzania kuwa na tunu ya kuwa na kiongozi mwenye maono tunashindwa kutumia bahati hiyo:
- Mtu anayekimbilia Ikulu mwogope kama ukoma. Hatumwogopa JK japo alionesha uchu wa kwenda Ikulu kwa miaka 10. Matokeo tunayaona. Inasadikika alikuwa tayari kuipindua serikali kama asingalipitishwa kuwa mgombea kupitia CCM.
- Alisema sera ya serikali tatu sio ya CCM ni ya CHADEMA, kama tunataka serikali tatu turudi kwa wana CCM tuwaulize kwanza kama wanataka serikali tatu au mbili. Unapokwenda Ikulu unaenda kutekeleza sera za chama chako sio sera za kwako na mkeo. Leo tunaona viongozi wanatekeleza serazaobinafsi.
- Kiongozi atakayechaguliwa kuwa raisi ni lazima aape kuilinda katiba ya nchi. Leo Zanzibar wanatunga katiba yao inayopingana na katiba ya Jamuhuri ya Mungano waTanzania hakuna kiongozi yeyote anayeitetea
- Kuna baadhi ya viongozi Nyerere kwa majina aliwakataa kushika nyadhifa za juu kama kuwa rais wanchi, leo hii sisi tunaona hao ndiyo majembe
- Nyerere alikataa kiongozi kupatikana kwa njia ya rushwa, leo tunaongozwa na wenye pesa za unga.
- Niambieni maono ya Nyerere yanasaidia kwa SIKIO LA KUFA lisilosikia dawa?
Kikwete alibainisha katika hotba yake ya ufunguzi wa Bunge, Zitto kabwe alithibitisha kukumbana na hilo katika kampeni zake na Hata james Mbatia juzi alibainisha hilo katika mkutano mkuu wa chama chake na mengi utayaona katika Uchaguzi wenu wa Serikali za mitaa na Ubunge. Mtu anachaguliwa kwa dini yake na si uwezo wake. Au nalo ulioni hilo mnashupalia Znz tu?
Msijifariji kwani hiyo ni changamoto kubwa ambayo inahitaji kufanyiwa kazi kabla kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika.
Kumbuka kuwa waarabu tunasema HUWEZI KUPIGA ULUZI WAKTI UNATAFUNA MUWA.
Mkuu usidanganyike na siasa za mitaani ,mfano wa kungalia ni pale inapotokea mada ya mungano(kasoro za mungano) kwenye baraza la wakilishi au bunge la jamuhuri ya tanzania tafauti kati ya mpemba na muunguja huondoka kunakuwa hakuna mpemba wala munguja kunakuwepo na mzanzibari.tafakari
na wewe na huyo nabii wako wa uongo....si huyo nyerere aki support hiyo sudan ijitenge?
Si yeye akisaidia kwa mafunzo?
Garang alikua hapa akisoma na kupata misaada....yote ni udini tuuuu
na anayo zungumzia nyerere kuhusu zanzibar ni udini pia haoni raha kuona waislam kule visiwani wakijitawala....walitawaliwa ...lakini ana ndoto ya kuwatawala ili kuhujumu uislamu
kwani kabla ya huu muungano si ilikuwapo zanzibar tena kubwa zaidi,
maneno ya nyerere ni ya unafiki na fikra za kikoloni..wagawe uwatawale....hii ndio falsafa yake kwa visiwa vile huu ni ukweli hata kiama...yule mzeee alikua ana chuki hasa na waislam wa zanzibar .
1995 nyerere alikuwepo akimpgia kampeni mkapa....alizunguka nchi nzima mpaka kapata ugonjwa ulomuondoa.
Kule zanzibar chama chake kilikua na hali ngumu...na matokeo rasmi ya wasimamizi ni kuwa ccm ilishindwa....CCM IKAPEWA USHINDI WA CHUMBANI tena kwa amri ya siri ya ccm na nyerere alukuwapo na anayajua haya,
mgogoro ukaibuka....watu wakatiwa misuko suko, walitiwa ndani na polisi walifanya uovu mbele ya camera za tv..nyerere yupo macho ..kama alikanyaga zanzibar mpaka amekufa....
Nyerere hakua na nia njema na zanzibar hata kidogo...aliacha ugomvi ule yeye akisulihisha migogoro ya watusi wenzake....zanzibar haikumhangaisha......zaidi ya kutoa matamko kama hayo ya kuwagawa.....alisema wazi kabla ya uhuru kuwa laiti angekuwa na uwezo basi angevi sokomeza mbali baharini visiwa hivi na kuvifukia...huyo ndio nyerere na zanzibar...
Wadanganye watoto na wanywa maji ya kijani
!!???
So ndio aunge mkono kujitenga badala ya suluhu....mbona wametulia leo ndani ya fed govement
Na viongozi gani hao wafrica?
Kwahio kujitenga wakatoliki kwa sababu ni wachache ni sawa lakini kujitoa waislam wa zenji kwake nongwa? Usimtetee alikua na kasoro zake na moja ya hizi ni islamphobia
Udini ulipandwa na watu waliokuwa wanafanya kampeni katika nyumba za ibada(makanisa & misikiti) hadi watu walikuwa wanatumiana sms katika simu zao, Unadhani Kikwete alipaswa kulalamika au alitakiwa achukue hatua? Na kama hakuchukua hatua basi dhambi hii ya udini hawezi kuikwepa.