kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,197
- 16,868
Katika moja ya hotuba zake mwl. Nyerere alituonya juu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na matokeo ya upande mmoja kuukimbia na kuuacha upande mwingine wa muungano ukishangaa na kuduaa kwa kukimbiwa na wenzao. Alisema upande utakaowakimbia wenzao hautabaki salama. Alisema Zanzibar ni Zanzibar na Tanganyika ni Tanganyika kwa sababu ya muungano, nje ya muungano hakuna Zanzibar bali kuna Unguja na Pemba, Wazanzibara na wazanzibari, Maalim Seif na Dr. Shein, Karume, na Tanganyika kuna Wasukuma, Wazanaki, Wachagga, Wapemba, Wazaramo, n.k.
Hebu ona kinachotokea sasa Sudan baada ya Sudani Kusini kuwakimbia wenzao wa Sudan Khartum. Sudan Khartum wamebaki salama na Sudan Juba waliowakimbia wenzao wakajikuta kumbe hakuna Sudan Kusini ila kuna makabila ya Dinka na Nuer. Ona sasa dhambi ya kuwakimbia wenzao wa Sudani Kaskazini inavyowatafuna S. Sudan, maelfu wanakufa na mamilioni wameyakimbia makazi yao. Kumbe Nyerere bana hasemi uongo ni mtakatifu kweli nilikuwa nawabishia wanaotaka kumtangaza ni mwenyeheri na mtakatifu, lakini kwa hili moja, naunga mkono kuitwa mtakatifu.
Zanzibar iwachukulie hatua madhubuti (upper hand) wale wote wanaotaka Zanzibar iwakimbie wenzao wa Tanganyika kwenye muungano. Tena iwachukulie hatua za wazi na bila kumung'unya maneno, hatua na vitendo watakavyowachukulia watu hao wenye ndoto ya kutaka Zanzibar ijitenge kutoka kwenye Muungano sasa na leoleo vinginevyo kinachotokea Sudani Kusini ni cha mtoto kwa kitakachotokea Zanzibar kama ikifanikiwa kujitenga, itakuwa vita ya Unguja dhidi ya majambia kutoka Uarabuni
Siasa za Zanzibar zina wadau wafuatao ambao watakuwa chanzo cha vurugu za Zanzibar ikijitenga:
1. Kisiwa cha Pemba na Kisiwa cha Unguja
2. Watu wa Pemba na watu wa Unguja
3. Chama cha CUF na CCM
4. Watu wa Zanzibar waliotoka Tanganyika
5. Watu wa Pemba na Unguja walioko Tanganyika wanaokumbwa na sheria ya Ukazi ya Zanzibar
6. Wazanzibar walioko Tanganyika wanaotaka kugombea urais wa Zanzibar
7. Watu wa Unguja na Pemba wanaotaka kugombea Urais wa Zanzibar
8. Mgawanyo wa mali na rasilimali zilizoko Pemba na Unguja
9. Uislam na Ukristo Zanzibar
10. Historia ya mapinduzi ya Zanzibar