Unabii wa Mwalimu Nyerere watimia

Unabii wa Mwalimu Nyerere watimia

Sisi Ccm hatupendi kuambiwa ukweli, ukisema ukweli tutakutafuta tutakusingizia kesi au kukupoteza kabisa kwenye ramani ya dunia. Kuweni makini
 
Katika Saikolojia ya Kiuandishi ukiona Mtu anakosea tu katika Kuandika vizuri au neno vyema katika Headline yake basi jua ya kwamba huyo ana matatizo ya ' akili ' ambayo hata Madaktari Bingwa wa duniani hawataweza kumtibia na sana sana watashauri tu akatupwe Baharini awe ' Kitoweo ' cha Kutukuka cha Papa kama siyo Nyangumi kwani hana tena faida ya kuendelea kuishi na Binadamu wengine hapa Ulimwenguni.
Tunampenda sana ijapo tunatamami mungu ampende zaid.
أمين
KEYBOARD WARRIORS.... Andamaneni tuwatwange halafu mrudi hapa mwezi MAY na makovu.Akili ya kufanya kazi itakuwa imewarudia.
Usitutishe Usitutishe Usitutishe!
Nilikua majaribu kumnukuu Maalimu Sefu Sharifu
 
huu uz hautakaa!
jf nayo wakisikia maandamano wanagwaya. ila wakisikia marufuku maandamano wanaacha hiyo topic. kibaya umemchnganya na Mange ndio kabisaaaa!! dk 2 nying utakua umefutwa
Kumbe mange ni Homa yao?
 
Hizi habari naona zinakuja kwa kasi!!
Na siku 3 mfulilulizo naota Mimi ndiye nitarithi nafasi ya mago..ni!
Huwa nikizinduka nawaza Sana'a!! But hata swala linaloendelea now niliwah kuliota tangu 2015!
Na hata kuna MTU nilmwambia kuwa huyu jiwe hatofika 20!
Badala yake nilipewa mseto!!
Ngojaaa niendelee kufatilia ulimwengu wa roho!

NB:but kuna watu wanailinda Sana'a hii nchi nao cyo idar but n maombi ya watakatifu! Ambao wanalia na kufunga nakuomba kwa ajili ya TANZANIA but tutafanya nini endapo MUNGU Amemkataa???
MTU anambiwa ATUBU! anangaka nasikia majuzi kasema atakuwa kiongoz wa malaika ooops MUNGU tuepushe!!!
 
Nyerere alitabiri kiongozi anaweza kutoka mahali popote lakini kiongozi bora atatoka CCM. Muda mrefu nimekuwa nikiuponda huu unabii hadi nilipoanza kusoma makala za Dakitari Mange Kimambi. ( Nimempa udakitari kuanzia leo kwa mamlaka sambamba na ya wale wanaojipa uprofesa na udakitari)

Mange ni kada machachari wa CCM sasa tunataka nini? Amekuwa akitoa ushuhuda matendo ya wenzie ni maovu sasa tunataka nini?

Kama Bwana wetu Kristu Yesu alipotoa ushuhuda kwa waovu si walimchukia? Sasa ni zamu ya Dakitari kuchukiwa kwa kukemea kizazi hiki kiovu na kizinifu! Huyu mdada ni nabii haswaaaa!

Unapoona watawala wanayagwaya maandamano ujue fika matendo yao ni maovu: wao ni kizazi cha kiza na utelezi.

Mchana saa sita wanapapasa kama ni saa sita usiku wa manane.

Ukweli ni nuru lakini wao hawataki ukweli bali wanajivunia kiza kwa sababu matendo yao ni aibu hata machoni pao.

Mange ukifumbia macho lugha zake za matusi tu sioni mpenda haki na maendeleo atamchukiaje? Wanaomchukia ni wabinafsi wanaoifilisi nchi hii.

Mtenda haki atapenda maandamano hatayachukia kwa sababu yanalenga kukemea maovu ya jamii.

Sasa wewe usiyependa kuwajibishwa na umma unafanya kazi ya nani? Hivi hamjui maandamano nacho ni kiwanda namba 3, 061? Kwanini hamkitambui? Eti tuwaache wawaletee watanzania maendeleo hivi hujui maandamano ndiyo mwanzo na mwisho wa maendeleo. Hivi nani kawaambia tunataka mtuletee maendeleo? Maendeleo huletwa na watu wenyewe siyo na watawala hasa hawa viwavi jeshi kulingana na ushuhuda wa kweli wa JK. Kama CCM ingelikuwa na nia ya kutuletea maendeleo wangejivunia maandamano ya kukemea mfumo uliokithiri dhuluma dhidi ya Mwenyezi Mungu na viumbe vyake. Maendeleo kwa kutembeza bakuli la ombaomba kweli. Hivi hawa watawala na ombaomba barabarani wanatofauti ipi?

India walipewa na Mwenyezi Mungu Mahtama Gandhi, Sauzi aliwapa Mandela na warudi walipewa Vladmir Lenin na sisi tusome alama za wakati tumepewa Mange Kimambi tumsikilize na tufanye maamuzi kulingana na utashi wetu.

Wako wanaokhoji matokeo ya Urais ya 2015 na wanaamini kuna dhuluma kubwa dhidi ya wapigakura na wasingependa wadhulumiwe 2020. Hivyo, wanadai sheria za uchaguzi zitinduliwe sasa kulinusuru taifa hawana jukwaa la kufikisha malalamiko yao zaidi ya kuandamana.

Wako wanaokerwa na kesi za kubambikiziwa za uchochezi au/ na utakatishaji wa fedha na wangependa muundo wa jeshi la polisi ubadilishwe ili wawajibike zaidi kwa wananchi badala ya kuwa jeshi la kulinda wizi na ubadhirifu wa mali ya umma unaofanywa na watawala. Hawana jukwaa la kufikisha ujumbe zaidi ya maandamano.

Wako wamechoshwa na utekwaji na mauaji yanayoendelea kwa misingi ya kisiasa. Hawaoni jitihada zozote za jeshi la polisi kuchukua hatua.

Wako wamechoshwa na nafasi za uongozi wa umma kumilikishwa makada wa CCM na kugeuza nchi kuwa ni mali yao tu. Huu ukabila na udini mpya wa uccm pia unaongeza misuguano kwenye jamii. Nchi hii siyo mali yao na jukwaa la kulisemea hili ni maandamano hakuna jinsi.

Baada ya uchaguzi wa 2015, waliotaka kuandamana kupinga matokeo ya Urais walizuiwa na polisi kwa kauli ya Kova eti siyo wakati mwafaka! MWAFAKA? Hilo ni tusi kwa wapigakura

Hongera Mwenyezi Mungu kwa kutupatia jemedari Mange Kimambi aendelee kuwaumbua wote ambao ni uzao wa kiza na utelezi.

JINA LA BWANA LIHIDIMIWE MILELE AMINA.
Hivi mamaako mzazi yupo?
Na kama yupo ana uwezo wa kusoma?
na je akisoma huu uzi wako wataraji atajionea fahari machungu aliyopitia wakati wa kuzaliwa kwako?
na kuyaonea faraja na makuzi yako?!

Kabla hujaamua kupumua hewa chafu hadharani angalia mazingira yanayokuzunguka na wale wanaokuzunguka.!

Utamu wa ulichokila harufu ya kupumua kwako inaweza kuwa kero kwa wenye ustaarabu.
 
tatizo hawa ccm wanaona wamefika, nchi wanaipeleka wawezavyo, huku wanachi wachumia juani wakiangamia.

26/04/ save the date.
 
KEYBOARD WARRIORS.... Andamaneni tuwatwange halafu mrudi hapa mwezi MAY na makovu.Akili ya kufanya kazi itakuwa imewarudia.

Hawawezi kuandamana ...kama wataaandamana basi itakuwa ni maandamano ya mitandaoni
 
Back
Top Bottom