Unabii wa Mwalimu Nyerere watimia

Unabii wa Mwalimu Nyerere watimia

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,502
Reaction score
911,254
Nyerere alitabiri kiongozi anaweza kutoka mahali popote lakini kiongozi bora atatoka CCM. Muda mrefu nimekuwa nikiuponda huu unabii hadi nilipoanza kusoma makala za Dakitari Mange Kimambi. ( Nimempa udakitari kuanzia leo kwa mamlaka sambamba na ya wale wanaojipa uprofesa na udakitari)

Mange ni kada machachari wa CCM sasa tunataka nini? Amekuwa akitoa ushuhuda matendo ya wenzie ni maovu sasa tunataka nini?

Kama Bwana wetu Kristu Yesu alipotoa ushuhuda kwa waovu si walimchukia? Sasa ni zamu ya Dakitari kuchukiwa kwa kukemea kizazi hiki kiovu na kizinifu! Huyu mdada ni nabii haswaaaa!

Unapoona watawala wanayagwaya maandamano ujue fika matendo yao ni maovu: wao ni kizazi cha kiza na utelezi.

Mchana saa sita wanapapasa kama ni saa sita usiku wa manane.

Ukweli ni nuru lakini wao hawataki ukweli bali wanajivunia kiza kwa sababu matendo yao ni aibu hata machoni pao.

Mange ukifumbia macho lugha zake za matusi tu sioni mpenda haki na maendeleo atamchukiaje? Wanaomchukia ni wabinafsi wanaoifilisi nchi hii.

Mtenda haki atapenda maandamano hatayachukia kwa sababu yanalenga kukemea maovu ya jamii.

Sasa wewe usiyependa kuwajibishwa na umma unafanya kazi ya nani? Hivi hamjui maandamano nacho ni kiwanda namba 3, 061? Kwanini hamkitambui? Eti tuwaache wawaletee watanzania maendeleo hivi hujui maandamano ndiyo mwanzo na mwisho wa maendeleo. Hivi nani kawaambia tunataka mtuletee maendeleo? Maendeleo huletwa na watu wenyewe siyo na watawala hasa hawa viwavi jeshi kulingana na ushuhuda wa kweli wa JK. Kama CCM ingelikuwa na nia ya kutuletea maendeleo wangejivunia maandamano ya kukemea mfumo uliokithiri dhuluma dhidi ya Mwenyezi Mungu na viumbe vyake. Maendeleo kwa kutembeza bakuli la ombaomba kweli. Hivi hawa watawala na ombaomba barabarani wanatofauti ipi?

India walipewa na Mwenyezi Mungu Mahtama Gandhi, Sauzi aliwapa Mandela na warudi walipewa Vladmir Lenin na sisi tusome alama za wakati tumepewa Mange Kimambi tumsikilize na tufanye maamuzi kulingana na utashi wetu.

Wako wanaokhoji matokeo ya Urais ya 2015 na wanaamini kuna dhuluma kubwa dhidi ya wapigakura na wasingependa wadhulumiwe 2020. Hivyo, wanadai sheria za uchaguzi zitinduliwe sasa kulinusuru taifa hawana jukwaa la kufikisha malalamiko yao zaidi ya kuandamana.

Wako wanaokerwa na kesi za kubambikiziwa za uchochezi au/ na utakatishaji wa fedha na wangependa muundo wa jeshi la polisi ubadilishwe ili wawajibike zaidi kwa wananchi badala ya kuwa jeshi la kulinda wizi na ubadhirifu wa mali ya umma unaofanywa na watawala. Hawana jukwaa la kufikisha ujumbe zaidi ya maandamano.

Wako wamechoshwa na utekwaji na mauaji yanayoendelea kwa misingi ya kisiasa. Hawaoni jitihada zozote za jeshi la polisi kuchukua hatua.

Wako wamechoshwa na nafasi za uongozi wa umma kumilikishwa makada wa CCM na kugeuza nchi kuwa ni mali yao tu. Huu ukabila na udini mpya wa uccm pia unaongeza misuguano kwenye jamii. Nchi hii siyo mali yao na jukwaa la kulisemea hili ni maandamano hakuna jinsi.

Baada ya uchaguzi wa 2015, waliotaka kuandamana kupinga matokeo ya Urais walizuiwa na polisi kwa kauli ya Kova eti siyo wakati mwafaka! MWAFAKA? Hilo ni tusi kwa wapigakura

Hongera Mwenyezi Mungu kwa kutupatia jemedari Mange Kimambi aendelee kuwaumbua wote ambao ni uzao wa kiza na utelezi.

JINA LA BWANA LIHIDIMIWE MILELE AMINA.
 
Nyerere alitabiri kiongozi anaweza kutoka mahali popote lakini kiongozi bora atatoka CCM. Muda mrefu nimekuwa nikuuponda huu unabii hadi nilipoanza kusoma makala za Dakitari Mange Kimambi. ( Nimempa udakitari kuanzia leo kwa mamlaka sambamba na ya wale wanaojipa uprofesa na udakitari)

Mange ni kada machachari wa CCM sasa tunataka nini? Amekuwa akitoa ushuhuda matendo ya wenzie ni maovu sasa tunataka nini?

Kama Bwana wetu Kristu Yesu alipotoa ushuhuda kwa waovu walimchukia, sasa ni zamu ya Dakitari kuchukiwa kwa kukemea kizazi hiki kiovu na kizinifu! Huyu mdada ni nabii haswaaaa!

Unapoona watawala wanayagwaya maandamano ujue fika matendo yao ni maovu: wao ni kizazi cha kiza na utelezi.

Mchana saa sita wanapapasa kama ni saa sita usiku wa manane.

Ukweli ni nuru lakini wao hawataki ukweli bali wanajivunia kiza kwa sababu matendo yao ni aibu hata machoni pao.

Mange ukifumbia macho lugha zake za matusi tu sioni mpenda haki na maendeleo atamchukiaje? Wanaomchukia ni wabinafsi wanaoifilisi nchi hii.

Mtenda haki atapenda maandamano hatayachukia kwa sababu yanalenga kukemea maovu ya jamii.

Sasa wewe usiyependa kuwajibishwa na umma unafanya kazi ya nani? Hivi hamjui maandamano nacho ni kiwanda namba 3, 061? Kwanini hamkitambui? Eti tuwaache wawaletee watanzania maendeleo hivi hujui maandamano ndiyo mwanzo na mwisho wa maendeleo. Hivi nani kawaambia tunataka mtuletee maendeleo? Maendeleo huletwa na watu wenyewe siyo na watawala hasa hawa viwavi jeshi kulingana na ushuhuda wa kweli wa JK. Kama CCM ingelikuwa na nia ya kutuletea maendeleo wangejivunia maandamano ya kukemea mfumo uliokithiri dhuluma dhidi ya Mwenyezi Mungu na viumbe vyake. Maendeleo kwa kutembeza bakuli la ombaomba kweli. Hivi hawa watawala na ombaomba barabarani wanatofauti ipi?

India walipewa na Mwenyezi Mungu Mahtama Gandhi, Sauzi aliwapa Mandela na warudi walipewa Vladmir Lenin na sisi tusome alama za wakati tumepewa Mange Kimambi tumsikilize na tufanye maamuzi kulingana na utashi wetu.

Wako wanaokhoji matokeo ya Urais ya 2015 na wanaamini kuna dhuluma kubwa dhidi ya wapigakura na wasingependa wadhulumiwe 2020. Hivyo, wanadai sheria za uchaguzi zitinduliwe sasa kulinusuru taifa hawana jukwaa la kufikisha malalamiko yao zaidi ya kuandamana.

Wako wanaokerwa na kesi za kubambikiziwa za uchochezi au/ na utakatishaji wa fedha na wangependa muundo wa jeshi la polisi ubadilishwe ili wawajibike zaidi kwa wananchi badala ya kuwa jeshi la kulinda wizi na ubadhirifu wa mali ya umma unaofanywa na watawala. Hawana jukwaa la kufikisha ujumbe zaidi ya maandamano.

Wako wamechoshwa na utekwaji na mauaji yanayoendelea kwa misingi ya kisiasa. Hawaoni jitihada zozote za jeshi la polisi kuchukua hatua.

Wako wamechoshwa na nafasi za uongozi wa umma kumilikishwa makada wa CCM na kugeuza nchi kuwa ni mali yao tu. Huu ukabila na udini mpya wa uccm pia unaongeza misuguano kwenye jamii. Nchi hii siyo mali yao na jukwaa la kulisemea hili ni maandamano hakuna jinsi.

Baada ya uchaguzi wa 2015, waliotaka kuandamana kupinga matokeo ya Urais walizuiwa na polisi kwa kauli ya Kova eti siyo wakati mwafaka! MWAFAKA? Hilo ni tusi kwa wapigakura

Hongera Mwenyezi Mungu kwa kutupatia jemedari Mange Kimambi aendelee kuwaumbua wote ambao ni uzao wa kiza na utelezi.

JINA LA BWANA LIHIDIMIWE MILELE AMINA.

Hakuna kitu kibaya na dhambi mbaya duniani kama kuandika ' Mkeka ' halafu ukiutathmini kwa kuupitia wote unakuta hakuta ' dini ' lolote zaidi tu ya Pumba kama siyo Takataka tupu.
 
huu uz hautakaa!
jf nayo wakisikia maandamano wanagwaya. ila wakisikia marufuku maandamano wanaacha hiyo topic. kibaya umemchnganya na Mange ndio kabisaaaa!! dk 2 nying utakua umefutwa
 
Naona mnatishia nyau....labda hayo maandamano mtayafanyia mitandaoni na sio kule kwetu Mwandiga....Mimi nasikitika tu kwamba hatuna chama cha upinzani imara....chadema hawana mikakati ya kuing’oa CCM ndio maana utaona sasa wame abandon chama chao na kumfanya Mange mshauri wao.....
 
26/04 si mchezo

kwani dodoma wanasemaji?
Kaka Jenta hide my id pls
 
huu uz hautakaa!
jf nayo wakisikia maandamano wanagwaya. ila wakisikia marufuku maandamano wanaacha hiyo topic. kibaya umemchnganya na Mange ndio kabisaaaa!! dk 2 nying utakua umefutwa
Jina Mange tu ni shida hapa.Huu uzi utaunganishwa tu lakini ipo siku watamtambua huyu dada kwasababu anasimamia haki licha ya lugha zake kali.
 
Hakuna kitu kibaya na dhambi mbaya duniani kama kuandika ' Mkeka ' halafu ukiutathmini kwa kuupitia wote unakuta hakuta ' dini ' lolote zaidi tu ya Pumba kama siyo Takataka tupu.
Kweli mwanadamu huangamia kwa kukosa maarifa na ukibishana na zezeta basi na wewe ni zezeta tu hakuna jinsi!
 
KEYBOARD WARRIORS.... Andamaneni tuwatwange halafu mrudi hapa mwezi MAY na makovu.Akili ya kufanya kazi itakuwa imewarudia.
Hata kaburu alijivunia hayo lakini za mwizi ni arobaini mtaachia ngazi saa sita mchana tena bila kuaaga huo nao ni unabii
 
Naona mnatishia nyau....labda hayo maandamano mtayafanyia mitandaoni na sio kule kwetu Mwandiga....Mimi nasikitika tu kwamba hatuna chama cha upinzani imara....chadema hawana mikakati ya kuing’oa CCM ndio maana utaona sasa wame abandon chama chao na kumfanya Mange mshauri wao.....
Kiongozi wenu na Mwenyekiti wenu wa Chama anajiita Jiwe sasa unategemea nini kuna maendeleo kutoka kwenye akili za jiwe?
 
Back
Top Bottom