Umuhimu wa Kuweka Spare Parts Halisi kutoka jerry spare parts and services Tanzania – Je, Watumiaji Wengi Wanaelewa?

Umuhimu wa Kuweka Spare Parts Halisi kutoka jerry spare parts and services Tanzania – Je, Watumiaji Wengi Wanaelewa?

Joined
Mar 15, 2018
Posts
59
Reaction score
60
Kama fundi ambaye nimekuwa kwenye hii fani kwa muda sasa, nimegundua jambo moja ambalo linaumiza wateja wengi – matumizi ya spare parts zisizo halisi kwa sababu tu ya bei kuwa ndogo.

Watu wengi wanapokuwa kwenye harakati za kutengeneza magari yao, hasa kwenye maeneo muhimu kama brake system, engine parts na oil filters, hupendelea spare parts za bei nafuu (aftermarket), wakiamini wanapunguza gharama. Lakini ukweli ni kwamba sehemu hizi feki huleta matatizo ya muda mrefu ambayo mwisho wa siku huongeza gharama kuliko mtu ambaye angeweka original parts.
255jerry_1745278253343.jpeg

Kwa mfano, brake pads feki huisha haraka na mara nyingi husababisha kuchakaa kwa diski. Oil filter isiyo halisi huzuia mtiririko wa mafuta vizuri, hali inayoweza kuharibu injini. Spark plugs za kiwango cha chini hupunguza utendaji wa gari na kuongeza matumizi ya mafuta. Haya yote yanaathiri si tu ufanisi wa gari, bali pia usalama wako barabarani.

Wateja wengi ninapokutana nao, huja wakilalamika gari linapata matatizo mara kwa mara. Kwa uchunguzi wangu, mara nyingi huwa wamewekwa spare parts zisizo halisi, kwa sababu aidha hawakujua tofauti, au walivutwa na bei ndogo. Hili ni tatizo kubwa ambalo linahitaji elimu kwa umma.​
Maswali
  1. Unapochagua spare parts kwa gari lako, unaangalia ubora au bei?
  2. Umewahi kupatwa na changamoto gani kutokana na kutumia spare parts feki?
  3. Je, unafahamu aina sahihi ya mafuta ya injini kwa gari lako (mfano: 5W-30 dhidi ya 10W-40)?
Tuchangie uzoefu na tujifunze pamoja kwa faida ya wote.
Kwa wale wanaohitaji spare parts halisi za magari pamoja na ushauri wa kitaalamu, mnakaribishwa Jerry Spare Parts Garage iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam. Tunauza spare parts bora, tunatoa huduma ya kitaalamu, na tunahakikisha mteja anarudi nyumbani akiwa na suluhisho la kudumu.

Mikocheni, Dar es Salaam
Simu/WhatsApp: 0715 666 656
Instagram: @255jerry
 
Sina gari. Nauliza for the future.

Kama muuzaji asiponiambia nitajuaje nauziwa spare og, fake, used, used feki au used original?

Sidhani kama bei ni factor kwakua naweza uziwa kwa bei ya original bila kujua.
 
ngoja aje.

lakini kwenye mabadiriko yagari yako ndioutajua uliuziwa feki au laa
 
Guarantee that matters. Huwezi niambia ni original baada ya muda ikaharibika.

Je mnatoa guarantee kwa service na part's mnazoweka ?

Vinginevyo ni ujanja janja tuu nasubiri majibu ya swali langu

Extrovert
 
Kama hujawahi kumiliki gari lakini unajiandaa kwa siku za mbele, ni muhimu kuelewa jinsi ya kutofautisha spare parts halisi (original), bandia (fake), zilizotumika (used), na used original. Kwa kawaida, vipuri halisi huja kwenye vifungashio vyenye nembo, serial number, na muonekano bora wa ubora, wakati feki vinaweza kuwa na maandishi yasio honekana vizuri na finishing hafifu. Bei siyo kigezo cha kutegemea, kwani unaweza kuuziwa fake kwa bei ya original. Ili kujilinda, ni muhimu kununua kwenye maduka yanayoaminika, kuomba risiti yenye maelezo, na kuwa na fundi mwenye uelewa na uaminifu. Au unawza kutupigia simu kwa maelezo zaidi 0715666656
 
Kwa mzoefu wa magari tunajua spare parts fake na original hasa Kwa magari ya Toyota, spares za Toyota ukifika dukani utazikuta Kwa bei zaidi ya 4 Kwa spare hiyohiyo moja

Mimi huwa nazunguka mwenyewe kuulizia spare huku nikilinganisha ubora pamoja na bei
 
Kama hujawahi kumiliki gari lakini unajiandaa kwa siku za mbele, ni muhimu kuelewa jinsi ya kutofautisha spare parts halisi (original), bandia (fake), zilizotumika (used), na used original. Kwa kawaida, vipuri halisi huja kwenye vifungashio vyenye nembo, serial number, na muonekano bora wa ubora, wakati feki vinaweza kuwa na maandishi yasio honekana vizuri na finishing hafifu. Bei siyo kigezo cha kutegemea, kwani unaweza kuuziwa fake kwa bei ya original. Ili kujilinda, ni muhimu kununua kwenye maduka yanayoaminika, kuomba risiti yenye maelezo, na kuwa na fundi mwenye uelewa na uaminifu. Au unawza kutupigia simu kwa maelezo zaidi 0715666656
Mkuu nadhani hujanijibu swali langu. Kwa kila spea original unayoweka pamoja na ufundi unaofanya hapo ofisini kwako au kwenu je? Mnatoa guarantee kwenye kazi yenu regardless ya spare parts.
 
Back
Top Bottom