Umri wako ni tabia yako! Hivi ndivyo ilivyo jifunze tabia 14

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Kila umri una mawazo na tabia yake tofauti

1. Miaka 1~5 ni umri wa kujifunza chochote kwa kuiga wakubwa
2. Miaka 6~10 ni umri wa msingi wa uadilifu unaodumu maishani
3. Miaka 11~17 ni umri wa makuzi na matamanio (haudumu)
4.miaka 18~25 ni umri wa ndoto kubwa za nia njema na matarajio makubwa (mfano; ndoto za kuwa bosi flani hivi, higher position, kumiliki mambo makubwa n.k)

5. Miaka 26~30 ni umri wa kukosoa wengine, lawama nyingi na visingizio lukuki (huu pia ni umri halali kwa jela au kifungo, usipofungwa umri huo basi huko mbeleni hata ukija kupata kesi ni rahisi kuchomoa)

6. Miaka 31~35 ni umri wa majuto na roho mbaya (pia ni umri wa kutengwa au kujitenga na mambo yako hususani kwa wanaume)

7. Miaka 36~40 ni umri wa majukumu na talaka hususani wanawake

8. Miaka 41~45 ni umri wa kujaribu nafasi nyingine ya mwisho kwa tahadhali kubwa~ last Chance (umri wa masahihisho)

9. Miaka 46-50 ni umri wa liwalo na liwe (hakunaga majuto hapa)

10. Miaka 51~60 ni umri wa utulivu na kumtegemea Mungu (umri huu hata ukisikia mkeo au mmeo kachepuka unaona haikuhusu)

11. Miaka 61~70 ni umri wa upatanisho wa imani na jamii

12. Miaka 71~80 ni umri wa kuhisi wewe ni wa Leo au wa kesho

13. Miaka 80~100 ni umri wa kutegemea mbeleko na kuona maruerue.
14. Miaka 100~zaidi ni umri wa pambo LA nyumba ( yaani unakuwa huna utofauti na picha ya ukutani au pambo la nyumbani)
 
Back
Top Bottom