Umri huu hauchezewi!

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Hii inaweza kukusaidia, hebu pitisha macho; inahusu umri!

1. Mwaka 1-5 ni umri wa kujifunza chochote kwa kuiga wakubwa.

2. Miaka 6-10 ni umri wa msingi wa uadilifu unaodumu maishani.

3. Miaka 11-17 ni umri wa makuzi na matamanio (haudumu).

4.miaka 18-25 ni umri wa ndoto kubwa za nia njema na matarajio makubwa (mfano; ndoto za kuwa bosi fulani hivi, higher position, kumiliki mambo makubwa n.k).

5. Miaka 26-30 ni umri wa kukosoa wengine, lawama nyingi na visingizio lukuki (huu pia ni umri halali kwa jela au kifungo, usipofungwa umri huo basi huko mbeleni hata ukija kupata kesi ni rahisi kuchomoa).

6. Miaka 31-35 ni umri wa majuto na roho mbaya (pia ni umri wa kutengwa au kujitenga na mambo yako hususani kwa wanaume).

7. Miaka 36-40 ni umri wa majukumu na talaka hususani wanawake.

8. Miaka 41-45 ni umri wa kujaribu nafasi nyingine ya mwisho kwa tahadhali kubwa, last Chance (umri wa masahihisho).

9. Miaka 46-50 ni umri wa liwalo na liwe (hakunaga majuto hapa).

10. Miaka 51-60 ni umri wa utulivu na kumtegemea Mungu (umri huu hata ukisikia mkeo au mmeo kachepuka unaona haikuhusu).

11. Miaka 61-70 ni umri wa upatanisho wa imani na jamii.

12. Miaka 71-80 ni umri wa kuhisi wewe ni wa leo au wa kesho.

13. Miaka 80-100 ni umri wa kutegemea mbeleko na kuona maruerue.

14. Miaka 100+ ni umri wa pambo la nyumba ( yaani unakuwa huna utofauti na picha ya ukutani au pambo la nyumbani).

Imeandikwa na Denis Mpagaze.
 
hata akina Kenyata yule rais wa kwanza wa kenya, na Moi waliukwaa wakiwa watu wazima
haya maisha na mafanikio hayajali umri. Kuna mzee wangu mmoja kaja kufanikiwa akiwa na umri wa miaka 70+, huko ujanani alii maisha ya kupambania mafanikio kaja kuyapata uzeeni sasa hivi anakula mavuno na mke wake, kuna wengine wanazaliwa tu wanakutana na utajiri wangali wachanga kama tifa wa diamond platinumz kukutana na mkataba wa benki kwenye kutangaza toto account ongeza na utajiri wa baba yake na mama yake. Bila shaka huyo mtoto sasa hivi ni binti kijana hajui umasikini ni nini. Kazaliwa kwenye bahari ya mafanikio
 
nina miaka 55 lakin mambo yangu kama ni mtu wa miaka 25 nikisikia kigodoro lazima niende nikifika kule nikuyarudi, nikiwekewa singer na vibati basi ni kuyarudi mpakaaa asubuh ndevu na sura vinanisaliti hahaha wakuu au kuna stage niliruka hapo chini
 
Back
Top Bottom