Nilikuwa najiuliza sana wanaposema mvuto wa Mama Samia umepunguwa nawaelewa vizuri sana wiki hii.
Wiki hii nimebahatika kuona video nne. Mama Samia akiwa Hanang akiongea kwenye jukwaa, video ya Mama Samia aliongea waathirika, Mbowe akiongea kwenye msiba wa Askofu na Lissu akiongea kwenye msiba wa Askofu.
Haya matukio yalikuwa muhimu sana kwangu kwasababu kwenye wakati mgumu ndiyo tunaona utu. Kwa upande wa Mama kwanza mkutano wake ulijaa makada na mashati ya kijani wakati watu wa kule sio wapenda siasa na wanaweza kuchagua chama chochote kule.
Pili amewekewa kapeti jekundu sehemu na mkutano wa majanga!. Pamoja na mawaziri kuwa vijana sijaona hata waziri mmoja alinyanyua jiwe au chochote kile.
Kwa ujumla Raisi kabisa na team nzima yake imeonekana kulazimisha mahusiano ya watu hawakupata connection yeyote nao. Wakati wenzao kama Mbowe ameongea kwenye msiba na unaona kabisa watu wana connect naye na Lissu alikuwa anatoa stori yake binafsi na watu wana connect naye.
Tatizo kubwa la Mama Samia amekosa ile connection ambayo alikuwa nayo mwanzoni. Sasa hata mimi binafsi sioni kama yuko real tena badala yake kabaki kuwa mwanasiasa bila kuwa na utu kama mwanzo.
Yule Samia wa kuongea na Mbowe, Lissu, katiba mpya, mwenye kutaka mabadiliko sasa kabaki mwanasiasa ambaye haonekani kama anayofanya au kutaka ni kwa faida ya taifa bali kwa faida ya chama, marafiki na familia.
Hakuna mzalendo wa ukweli asiyetaka katiba mpya ambayo ni kwa manufaa ya nchi na sio mtu binafsi. Kama mtu haoni umuhimu wa katiba mpya basi hafai kwasababu kwanza kutokuelewa umuhimu ni tatizo lakini kikubwa ni kukataa kwa manufaa binafsi.
Swali mmoja nimekuwa najiuliza kama kipimo cha uzalendo. Je Mama Samia anapenda nchi yake kuliko madaraka? Jibu langu mwanzoni alipoanza ilikuwa ndiyo sasa kalewa madaraka jibu ni hapana. Tuendelee kuombea nchi tupate viongozi wazalendo wenye upeo.
Mimi binafsi naandika haya kwa masikitiko makubwa sana na naona kabisa sasa viongozi wanavyo anza kulewa madara na kuwa watu tofauti na Mama Samia naye naona hajaweza kukwepa mtego huo. Nilifikiri yeye ndiye angeweza kutusaidia kuleta katiba mpya, kubadilisha mifumo ya utendaji kuwa ya kisasa, kukomesha rushwa na kuweka demokrasia uhuru na ushindani ambako duniani kote ndiyo unaleta ubunifu na maendeleo. Badala yake tunaona amerudi kuwa Mama wa wapambe, machawa, na mtu wa kujali madara zaidi. Kama sio yeye iko siku tutapata mtu wa kutuvusha lakini Mama Samia naona kama anapoteza nafasi muhimu ya kukumbukwa kama shujaa.