Umri wa kustaafu uwe miaka 45/Utumishi kikomo iwe miaka 15

Umri wa kustaafu uwe miaka 45/Utumishi kikomo iwe miaka 15

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,018
Reaction score
20,489
Ninafikiri kwamba, Umri wa kustaafu utumishi wa umma ushuke na kuwa angalau miaka 45 hivi, ama tuweke ukomo wa utumishi wa umma uwe miaka 15 tu, ili mtu akistaafu apate fursa ya kuyaishi maisha mengine ya kujitafutia kipato nje ya utumishi akiwa na nguvu zake kamili, na kuruhusu kizazi kingine kushika nafasi yake.,

Utafiti wangu usiorasmi unaonyesha wastaafu wengi hawakai miaka 5 hadi 15 hivi baada ya kistaafu wanakumbwa na matatizo ya kiafya ikiwemo msongo wa mawazo na ugumu wa kupata kipato kipya.

Ajira zote ziwe na ukomo ili kutuhusu watu wengi nchi kutumikia serikali ya Tanzania, Wako watu katika utumishi wanavipawa vya biashara na fani nyingine nyingi za kujiajiri, lakini wanauwa talanta zao kwa kumezwa na utumishi hadi uzeeni. Watoke waje mtaani wafanye biashara waonje maisha ya umma wa kawaida.

Tutapunguza sana pengo la walalaheri na walala hoi, hata nidhamu ya utumishi dhidi ya umma itarejea.

Na Yericko Nyerere
 
Kwanza lengo la utumishi wa umma sio kusaidia watu wapate ajira waweze kuishi ndio maana ajira hutolewa kutokana na uhitaji wa jamii na si kutokana na idadi ya wanahitaji kazi,lengo ni kuitumikia jamii

Pili, kustaafu kwa hiyari inaruhusiwa muda wowote hakuna anaekuzuia
 
Takwimu hazi support hilo jambo kuleta tija.

Watumishi wa Umma Tanzania ni kama 500,000 kwa nchi ya watu milioni 70. Kuna incentive gani kwa wao kustaafu mapema?

Ingekuwa mimk ndo mtunga sheria ningeondoa umri wa watu kustaafu. Bali ningeruhusu mtu afanye kazi mpaka atavyojiskia kuacha.

We hujiulizi ni kwanini mtu akisfaafu anakaa kidogo na kufariki?
 
Wazee njooni mchangie hii mada msiipite pembeni pembeni huko mnaambiwa muachie hivyo viti mlivyovikalia vijana nao waanze kuvikali kabla umri haujawatupa mkono,

Wewe mpaka una miaka 70,80,90 hujastaafu hata kwa hiari Mzee wangu wewe umo tu eeh wewe umekalia tu kiti yaan wewe unapewa tu kiti kalia hicho kiti Mzee wangu mpaka unagonga 100 wewe umepewa tu kiti yaan inamaana hawa vijana wanaoibuka kila leo hawana chochote wanachoweza kuchangia chenye manufaa kwa taifa lao?

Wazee msinifukirie vibaya mimi nimechangia mada tu
 
Tatizo hawana hela ya kulipa mafao,mbona watumishi walio wengi wanataka kujitoa na walikuwa wanajitoa ,mifuko ya hifadhi IKAONDOA FAO LA KUJITOA.

asilimia kubwa ya watumishi ni wajasiriamali iwe biashara kilimo na ufugaji,pia wangependa wajitie kwenye ajira wakiwa bado na nguvu ,wakishalipwa MAFAO YAO ya kujitoa ,wasimamie miradi yao wakiwa bado na nguvu ,PIA wachukue mikopo ya PESHENI yao waongezee mitaji ya biashara zao.

Halafu nguvu walizobakiwa nazo mfano wakisema kujitoa kuanzia mika 40 au 45 wanakuwa bado na nguvu kubwa NA MITAJI ya kufanya ujasiriamali

NA KUFANYA KAZI PRIVATE SECTORS..

FAO LA KUJITOA KILA civil worker mwenye akili timamu analitaka anataka kujitoa ,asimamie biashara zake ambazo ataingiza hela nyingi na faida kubwa kuliko mshahara wa ajira za serikalini kwa kutumia mtaji alioupata serikalini hata akiamua kufuga tu.

HIYO SERIKALI UNAYOISHAURI ndiyo HAITAKI KULIPA MAFAO YA KUJITOA.

ila watumishi wengi waajiriwa wanataka KUJITOA HATA SASA wafanye mambo mengine,AJIRA ZA SERIKALI ni UTUMWA. ni umasikini..ndio mana ukitegemea mshahara peke utakuwa masikini.

kakindi kadogo sana cha watumishi wa serikali ndio wanaonufaika na POSHO ZA AJIRA.

1.Serikali itaingia GHARAMA kuajiri mara kwa mara ,na kulipa MAFAO mara kwa mara.

HAKUNA mtumishi wa serikali mwenye miaka 45 mwenye akili timamu ambaye ukimwambia tukulipe fao la kujitoa ,tuww tunakulipa pesheni kila mwezi,ubaki na nguvu zako ukazitumie kwenye miradi yako ja private sector UKIWA BADO NA NGUVU NA MTAJI..na uhakika wa pensheni kila mwezi..bado akangangania ajira ,hao ni wale wachache sana wanaofaidika na mfumo..wa kujilipa maposho..posho ila SIYO MSHARA PEKEE ndio umfanye abaki.

UNGEKUWA ni mtumishi wa serikali ungekuwa unalijua hilo.
 
45 haitowezekana labda 55. Mtu astaafu kwa hiari yaie @ 50, astaafu kwa sheria @ 55. Sababu ni hizi hapa;

Mfumo wetu wa elimu unatuweka sana shuleni, mtu anamaliza degree miaka 25+. Wapunguze muda wa kukaa shule ndipo waje wapunguze muda wa kustaafu. Elimu yetu, miaka 7 shule ya msingi, miaka 4, sekondari, miaka 2 high school, miaka 3-4 chuo, hapo mtoto anaanza shule na miaka sita au saba. 😁

Mbili ni kwamba, mfumo wetu wa mafao ni "merit-based/time-based" yaani ukikaa kazini miaka mingi na mafao yako ndo yanaongezeka. Ulaya unaweza piga kazi 15 years bado mafao yakawa makubwa na mazuri.

Mtu anakaa shule anasoma mavitu ambayo hayaji kuyatumia kazini, kupoteza muda tuu. Huo muda angekuja kuutumia kuzalisha/ajira. Mtu apate degree miaka 18, aingie kazini, miaka 55 astaafu. Miaka 50 astaafu kwa hiari, achukue chake akafie mbele akiwa na nguvu.
 
Mawazo ya kinyumenyume. Kumlipa pensheni toka miaka 45 hadi anakufa ni hasara. Pia mtu atajiendelezaje kuwa mbobezi na akifika tu 45 anastaafu?
 
Kwa wastani wa miaka 30 mtu anaanza kazi, akatumikia miaka 15 , nadhani ni nzuri..
Miaka 25 ni umri wengi wamemaliza vyuo... akianza ajira na 30 yrs ni sawa tu...

Baadhi ya taaluma wanaweza ongezewa umri wa kustaafu mfano doctors na baadhi ya professionals zinazochukua muda mrefu kusomea.

Tajiri ukianza kuitumia nguvu kazi yako kuzalisha ukiwa na miaka 30, umeshachelewa maisha yako. 😊
Huo ni muda mcheza soka ulaya anastaafu. Ni muda mtu ameshakuwa CEO ulaya/marekani. Ni muda mtu yupo kwenye senior role kwenye career yake. 😊

Wanakwambia life expectancy ni miaka 45, wewe uingie kwenye workforce una 30+. Sio sawa, japo serekali yenu imefanikiwa kuwaonyesha kama ni sawa. 😁

Algeria tuu hapo, mtoto miaka 18+ ana degree yake kitambo sana. Anabaki kuingia kwenye workforce.
 
Tajiri ukianza kuitumia nguvu jazi yako kuzalisha ukiwa na miaka 30, umeshachelewa maisha yako. Huo ni muda mcheza soka ulaya anastaafu. Ni muda mtu ameshakuwa CEO ulaya.

Wanakwambia life expectancy ni miaka 45, wewe uingie kwenye workforce una 30+. Sio sawa, japo seeikali yenu imefanikiwa kuwaonyesha kama ni sawa. 😁
Hivy waanze kazi/kaajiriwa katika umri upi?
 
Back
Top Bottom