Umri wa kuanza darasa la kwanza uanzie miaka 10, sababu hizi hapa

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF

Makuzi ya binadamu wa mtanzania yanapitia magumu mengi, hivyo pia akili huchelewa kukomaa kupata uelewa wa kujifunza kitu Kwa umakini. Natoa sababu Kwa nini umri miaka 10 ndio unafaa mtoto kuanza la kwanza.

1. Umri ukiwa miaka kumi mtoto anakuwa amekomaa, huondoa woga na anaweza kuhoji kama kitu sio sahihi.
2. Waliokosa lishe bora huwa ndio wakati ambao makuzi ya akili yanakuwa sawa.
3. Mtoto hadanganyiki kirahisi na akifanyiwa vitu vya unyanyasaji wa kijinsia ana uweza wa kumweleza mama yake au baba yake.
4. Ni umri ambao vipaji huchipuka mtoto kujua anapenda nini Na ana kipaji gani.
5. Kutokukubali kuonewa na mtu yeyote Kwa kuwa sio muoga.
6. Urahisi wa kuweza masomo walimu hawapati shida.
7. Kama shule ipo mbali huyu ndiye mwenye uwezo wa kutembea umbali mrefu.
8. Akimaliza darasa la saba anaweza kusaidia shughuli za kilimo au kuanza kujitegemea
9. Hauhitaji kumlea kama mtoto ikiwa hakufaulu kuendelea na masomo.
10. Kutokana na umri anakuwa amepunguza michezo mingi hatarishi kwa kuwa tayari ana uelewa

Kumbukumbu zinaonyesha wengi waliofanikiwa wengi walianza shule wakiwa na miaka 12.
 
Kuna research ilifanyika baada ya ongezeko la watoto wenye Attention deficit hyperactivity disorderADHD Marekani kuwa kubwa kulinganisha na nchi za Ulaya.

Waligundua kuwa watoto wa nchi za Scandinavian hupata muda mwingi wa michezo katika elimu ya awali. Elimu hasa huanza mtoto anapofikisha miaka 5.

Miaka 10 ni kumchelewesha mtoto, huu ni muda mtoto anajiandaa na mitihani ya kumaliza shule ya upili, anajua kuandika insha, hesabu za kujumlisha, kutoa, kugawanya kuzidisha na percentage hata algebra.

My point is kumuwahisha sana mtoto shule kuna hasara hali kadhalika kumchelewesha.
 
Adhd?
Kuna research ilifanyika baada ya ongezeko la watoto wenye Attention deficit hyperactivity disorder is a condition that includes symptoms such as inattentiveness, hyperactivity and impulsiveness.
ADHD Marekani kuwa kubwa kulinganisha na nchi za Ulaya. Waligundua kuwa watoto wa nchi za Scandinavian hupata muda mwingi wa michezo katika elimu ya awali. Elimu hasa huanza mtoto anapogikisha miaka 5.

Miaka 10 ni kumchelewesha mtoto, huu ni muda mtoto anajiandaa na mitihani ya kumaliza shule ya upili, anajua kuandika insha, hesabu za kujumlisha, kutoa, kugawanya kuzidisha na percentage hata algebra.
 
ila tuwe wakweli mie wanaposema eti miaka 18 ni mtu mzima kwa watanzania nakataa, kuna watu miaka hiyo hawajielewi (wengi wa watanzania) hata kuhoji kitu hawezi yaani anapelekwa kama ndezi tu.

Mimi napendekeza shule tuanze na miaka 16 maana watanzania akili zetu ni ndogo sana wakati mwingine nahisigi hatuna akili kabisa (tunadaiwa akili)
 
Kuna research ilifanyika baada ya ongezeko la watoto wenye Attention deficit hyperactivity disorder
ADHD Marekani kuwa kubwa kulinganisha na nchi za Ulaya. Waligundua kuwa watoto wa nchi za Scandinavian hupata muda mwingi wa michezo katika elimu ya awali. Elimu hasa huanza mtoto anapofikisha miaka 5.

Miaka 10 ni kumchelewesha mtoto, huu ni muda mtoto anajiandaa na mitihani ya kumaliza shule ya upili, anajua kuandika insha, hesabu za kujumlisha, kutoa, kugawanya kuzidisha na percentage hata algebra.
Huna hoja wewe
 
ila tuwe wakweli mie wanaposema eti miaka 18 ni mtu mzima kwa watanzania nakataa kuna watu miaka iyo hajielewi (wengi wa watanzania ) hata kuhoji kitu hawezi yaani anapelekwa kama ndezi tu.

mi napendekeza shule tuanze na miaka 16 maana watanzania akili zetu ni ndogo sana wakati mwingine nahisigi hatuna akili kabisa (tunadaiwa akili)
Huwezi ku generalise, kuna watoto wanakomaa mapema. Kuna kesi moja ilitokea Ulaya, binti wa miaka 16 alitibiwa na wazazi wake walifahamishwa kuhusu tiba ya mtoto wao.

Mtoto alipeleka kesi mahakamani kuwa uhuru wake wa kutunza siri umeingiliwa. Alishinda kesi na alilipwa fidia.
 
Huwezi ku generalise, kuna watoto wanakomaa mapema. Kuna kesi moja ilitokea Ulaya, binti wa miaka 16 alitibiwa na wazazi wake walifahamishwa kuhusu tiba ya mtoto wao.

Mtoto alipeleka kesi mahakamani kuwa uhuru wake wa kutunza siri umeingiliwa. Alishinda kesi na alilipwa fidia.
Nisome upya madame, nimesema 18yrs kwa watanzania kusema wamekomaa ni uongo mtupu kwanza hata kujielewa 99% hawajielewi hata kujieleza hawajui yaani awe kasoma ama hapana

Kwa ulaya ni tofauti kule kweli 18yrs anajielewa nawe ndio umenambia hiyo kesi 16yrs huko Ulaya sawa niko bongo hapa

Bongo akili zinaanzaga kuja ana 30yrs ndio ana akili za 18yrs wa Ulaya na sehemu nyingine.
 
Ni vizuri kutoa mawazo yako, lakini naona mengi ya uliyoyaongelea ni ya kusahihisha taratibu zetu kuliko kushusha umri wa kuanza shule.

1: Suala la kuhoji ni zao la jinsi tulivyowalea watoto wetu tangu wakiwa wadogo. Kama mzazi hampi nafasi ya kujieleza mtoto na kuwa na mazungumzo chanya zaidi ya kukalipia usitegemee mtoto huyo kuja kuwa mjenga hoja na anaeweza kuhoji. Hii imeenda mpaka kwenye jamii nzima, anayehoji huonekana kama ana matatizo zaidi na ndiyo mzee ni mwema zaidi. Ukiangalia uwezo wetu wa kuhoji tunazidiwa na majirani zetu mfano Kenya.

2: Suala la afya za watoto, ni vyema kujibidisha kwa wamama kuandaliwa kabla ya kubeba ujauzito, kipindi cha ujauzito ili wawe na afya njema. Pia kuhakikisha watoto wetu wanapata lishe bora ili kuzuia kuyumba kwenye misingi ya afya zao.

3: Uwezo wa kuelewa: Watoto wana uwezo mkubwa wa kuelewa kwani tunaamini wakati wa utoto kunakuwa na nafasi ya kuweka vitu vipya kwenye akili. LAKINI, hili lisitumiwe vibaya kwa kuwarundikia watoto mambo mengi na mengine ambayo huwaweka busy bila msaada wowote wa kimaarifa hapo mbeleni.

Pia hii imepelekea watoto kuwa na mizigo mikubwa ya vitabu na daftari katika umri mdogo, hii hupelekea watoto kuumwa migongo kwa ubebaji wa vitendea kazi. Kama ujuavyo shule zetu hazina utaratibu wa kuacha vitendeakazi husika shuleni na ratiba za shule hazifuatwi kikamilifu, hii ingesaidia baadhi ya vifaa kuachwa nyumbani.

4: Michezo hatarishi: ni matokeo ya malezi na si umri. Unaweza kukuta mtoto wa miaka saba ana mwenendo mzuri kuliko miaka kumi kulingana na mwenendo wa malezi aliopewa. Hili linahusisha suala la kudanganyika pia.

5: Mtoto akianza darasa la kwanza na miaka 10, anamaliza na miaka 17, kidato cha 1-4 miaka21, kidato cha 5+6 ni miaka 23, chuo kama ni fani ya miaka 5 anamaliza akiwa na miaka 28. Hapo umebahatika kwenda bila ukinzani/mambo yamekunyookea.

Binafsi, ningefikiria kuondoa hili chujio la kidato cha tano na sita. Ili kuimarisha kidato cha kwanza mpaka nne ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama mbalimbali kwa serikali na wazazi. Na anaefauru vyema aende chuo chochote kulingana na ufaulu utakaowekwa. Walioshindwa kufikia kiwango waende VETA, ambayo nayo iimarishwe vizuri. Mtanisahihisha wadau.

Inabidi uwe na wakati mgumu wa uanze maisha uraiani au uendelee na shule? Watoa scholarship wanasemaje?

Ukiingia uraiani miaka miwili maisha ya ndoa yanakuita ndani ya miaka 3, hapo una 31, sijui utarudi shule lini. Ukisema ukasome kwanza bila kupita kazini napo utatumia miaka 2-3 unakuwa na 31.

Ukianza kazi tu, au kujiajili maisha ya familia haya hapa, uwe umebahatika kuipata kazi au kujiajili. Kwani ni miaka 2 tu unakuwa na miaka 33. Utahitaji watoto wangapi? Labda watatu, with spacing miaka 2, jumla ni sita. Hapo uwe umebahatika kupata mke au mme na muanze maisha na mtoto ndani ya mwaka wa 1. Ghafla, mtoto wa tatu, wewe uko na miaka 40. Mtoto wako wa mwisho ana miaka10, wewe una 50. Na hapo Mungu saidia mambo imenyooka kwelikweli. Na life expectancy ikoje? Ukipata zaidi ya hapo, wengine wanaweza kukuita babu au bibi.

Hapa ndo tunajikuta mafanikio uzeeni na hapohapo unaambiwa usitumie sukari, chumvi, usile wanga kwa wingi, nyama nyekundu, (sijagusa pombe/optional), nawe ndo unayaona mafanikio yako mbele ya uso wako.
 
Mtoa mada utakuwa unamtetea mwanao si vinginevyo.

Wakati umri wa kuishi unazidi kupungua wewe unakuja kuturudisha nyuma 😷, mpaka sasa inatakiwa mtoto aanze shule akiwa na miaka 6 au 7 ili kumpa mafasi ya kuanza kuelewa ma kujifunza stadi mbalimbali za elimu.
 
Afrika haipo sababu ya mtu kufika chuo kikuu! Kuna namna tunayotakiwa kufikiri kwa upya na kuchukua hatu kulingana na bara letu ni namna gani ya kujikomboa kiuchumi.

Hii kufikiri vya nje ndo vinatuponza na unamkuta mtu anakuja humu anaanza kufananisha elimu,mazingira ya ulaya na kwetu na unamuona mtu wa namna hiyo anaandika humu kiswaenglish unagundua tu kwamba hawa ndiyo wanao tuludisha nyuma kimaendeleo

Mtanzania unamkuta anafikiri kizungu zungu na kuongea kizungu na kufuata mifumo ya mafanikio kizungu ilihali alipozaliwa na anapoishi uchumi wake hautegemei msamiati wa teknolojia bali ni kilimo.

Na tunacho walithisha watoto kwa mfumo wa elimu hizi za kulipia pesa nyingi tegemeeni vitukuu na nyanya zetu kuja kuishi maisha mabaya sana ya kuigiza na hawataweza chochote na mwisho wa siku watalazimisha mzungu aje kuwaongoza na hapo ndipo ukoloni utarudi Africa na mambo kuwa pale pale mabaya zaidi.
 
Back
Top Bottom