Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,914
Kimsingi, haya mambo yanachanganya.
Kuna kipindi huwa nahisi kuna hawa viongozi wa dini wanajua hivi vitu hakuna ila wanawazuga tu wafuasi wao, kwa sababu wanazozijua wao, Niliwahi kumsikia Dr.W.Slaa akisema kuwa kipindi bado yuko padre alishawahi kutumwa na kanisa, atembee katika vijiji vya karatu kufundisha watu kwamba hakuna uchawi, na katika kitabu hicho cha padre Gregory, kinachoitwa HAKUNA BINADAMU MCHAWI ILA SHETANI, mwishoni ni kama anasema kuwa huo ndio msimamo wa kanisa, Kanisa takatifu la mitume la Roma. (The Holy, Apostolic, Catholic Roman Church).
Amefafanua kuwa kwenye Biblia uchawi umetajwa, ila katika mazingira ya imani tu, kuwa watu waliamini hivyo, na kuna mfano wa wachawi wa Farao kufanya uchawi wa kugeuza fimbo kuwa nyoka, yeye anadai ile ilikuwa aidha kiini macho, au vitu vingine lakini sio uchawi.
Mtazamo huu wa wakatoliki, japo unanishangaza, lakini naupenda.
Kuna watu hata hawajui uchawi ni nini,kwasababu hiyo ndio maana wanakwenda kuutafuta mahali ambapo haupo,ni sawa na uende kuchimba chini ukitarajia ukute sahani ya pilau ikiwa na vipande vya nyama ya kuku
Mtu yoyote ambae ni mzima wa akili au ni msomi tunaweza kutarajia mtu huyu asifanye mabo kama mtu mwenye matatizo ya akili au mtoto mdogo,mtot akifanya mambo kama ya mtu mzima ni faida lakini mtu mzima akifanya mambo kama ya mtoto hilo litakuwa ni janga na hasara kubwa
Uchawi ni nguvu kama nguvu zingine,mfano umeme n.k,mtu ambae atataka afanye utafiti kuhusu uchawi halafu asizingatie hilo huyo atakuwa ni mwendawazimu,mtu akitaka kuujua au kujua kama upo halafu asizingatie hilo ne ni mwendawazimu
Kwasababu ni nguvu basi nao pia una kanuni zake na ili uweze kuutumia au kutaka kuona uwepo wake ni hadi uweze kujua kuhusu kanuni zake na uweze kuzifuata,mtu ambae anaweza kudhani kuwa unaweza tu kwenda popote na kuutafuta uchawi na kuupata huyo nae ni mwendawazimu kwasababu hakuna nguvu inayopatikana popote tu
Mtu yoyote ambae anasema tu ngoja niwaambie watu waniloge na kama wakishindwa basi uchawi utakuwa haupo huyo nae ni mwendawazimu kwasababu ukimuuliza kama hiyo ni kanuni ya uchawi hawezi kukujibu na inawezekana hata hajui kama uchawi una kanuni
Kimsingi kama binadamu ambao tunatumia uwezo wetu vizuri wa kutafakari mambo hatuwezi kwenda kama wendawazimu kwenye jambo lolote lile
Uchawi unafanya mambo kila uchao huku kwenye maeneo ambayo tunaishi na niliwahi kutoa ushuhuda wangu hapa kuhusiana na tukio la sofa kuungua moto kwenye chumba ambacho tulikuwamo,kuna mengi nimeyashuhudia na kuna mengi jamaa zangu wameyashuhudia,sio lazima tubishane kwenye kila jambo lakini kama kweli hawa wanasayansi hawajui uwepo wa uchawi nina sababu za kuwaita wajinga sana
Kama wanajua halafu wana sababu zao za kuficha hilo angalau linaweza kuwa na mashiko
Mtu anaweza kuficha jambo kwasababu zake mwenyewe na wengi inakuwa ni kwasababu za kipato lakini kiukweli kama unaweza kudhani kuwa uchawi haupo kwasababu tu hujawahi kuuona au kuona ukitenda kazi basi wewe una tatizo kubwa sana
Kama mtu anadhani uchawi unaweza kutumika kijinga jinga tu bila kufuata kanuni halafu mtu huyo huyo hakubaliani na umeme kutumika kijinga jinga tu bila kufuata kanuni huyu mtu atakuwa na tatizo kubwa sana
Kusema tu kwenda vijijini kutafiti kama uchawi upo na ukaukosa kisha kuhitimisha kuwa haupo ni sawa na mtu ambae ameshika kamba ya katani iliyokauka halafu akaigusisha kwenye nyaya za umeme kisha akasema kama kuna umeme hapa basi unipige shoti nife na baada ya kuigusisha kamba yake kwenye nyaya hizo na matokeo aliyoyatarajia yasitokee na akahitimisha kuwa hakuna umeme huyu mtu atakuwa ni mjinga sana
Iikie mahali tuache kutumia akili za kuazima na tutumie zetu wenyewe kwa kutafakari mambo
Mkuu,ukija Mwanza nitafute nikuambi jambo kuhusiana na haya makitu!