Umri wa dunia ni upi hasa?

Umri wa dunia ni upi hasa?

Leteni na mistari kutoka kwenye kuruan huwenda ikawa na mwanga zaidi.
 
jinsi ya mtiririko wa uumbaji wa biblia na hali halisi haviendani kabisa. ipo contradicted kwa wasiokuwa na mawazo chanya na tafitivu. biblia ni kitabu kilichoundwa maalumu kumfunika mtu asitambue ukweli uliopo. wakati maisha na elimu ya sayansi inaonyesha wazi kuwa huo uumbaji wa biblia ni vitu vya kufikirika zaidi na haviendani na hali halisi. mfano ni kaini aliwekwa alama kwenye paji ili huko aendako asipigwe kwa tendo alilolofanya kumuua nduguye. kama walikuwa wanne na mmoja kauliwa angekwenda kupigwa na nani na alipooa alimuoa nani mashariki mwa bustani?

. 14Leo umenifukuza kutoka ardhi yenye rutuba na mbali nawe. Basi, nitakuwa mtu wa kutangatanga, asiye na makao maalumu duniani, na yeyote atakayeniona ataniua.” 15Lakini Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Sivyo! Atakayekuua wewe Kaini atalipizwa mara saba.” Basi, Mwenyezi-Mungu akamtia Kaini alama ya tahadhari, ili yeyote atakayemwona asimuue. 16Kisha Kaini akaondoka mbele ya Mwenyezi-Mungu, akawa anaishi katika nchi ya Nodi,4:16 Nodi: Maana yake “kutangatanga.”" class="ng-isolate-scope" style="box-sizing: inherit; color: rgb(0, 140, 186); line-height: inherit;"> upande wa mashariki wa Edeni.

Maisha ya watu wanne ambao hawakujua hili wala lile kutambua kuwa atauliwa na yeyote atakayemuona bila kujua kosa lake ni ujuha tuu wa imani. ili kuweza kukubaliana na hizi hadithi kunahitajika upumbavu wa hali ya juu. huwezi kuogopa kitu ambacho hakipo na wala hujakiona.

Uumbaji wa Biblia ni mambo ya kusadikika lakini uwezo binafsi wa binadamu/mtu katika kujenga na kutenda ni mkubwa zaidi ya imani na imani yabidi kujengwa katika uwezo wa binadamu/mtu kutenda. huu uwezo kwa wasioufahamu au kuutambua ndio hugeuka imani. nami imani naitafsiri kama upungufu wa maarifa, kwa kufikiri kuwa kuna maisha fulani mazuri sana baada ya kufa na huu ndio mtego wenyewe.

nimewaza kwa kuandika
 
Mwingine yupo tayari kumlipua au kumkata shingo mwenzie kwa imani ya kwenda peponi baada ya kifo! Hiyo imani ya kumwaga damu ya binadam mwenzio ili we uende peponi ni ya vipi?
 
haswa hapa ndio mimi naona pana shida siku za kibiblia ni sawa na calculation ya siku zetu za masaa 24 za leo?la sivyo hatuwezi kuelewa ikiwa ktk biblia wanaongelea ikawa jioni ikawa asubuhi siku moja(tena note sio siku ya kwanza ni siku moja)
yani watu wanabishana pasipo kuanza na mambo ya msingi kabisa.
umemjibu vizuri sana
Ndio mtuambie ni calendar ipi? Othrws biblia watu hawaijui... kwanin isijulikane? Days zinasababishwa na jua so kwa mungu pia kuna jua? Mnataka kituambia kwamba Mungu nae yupo kwenye sayari? Hizi dini ni hisia tu... watu huwa wanadai wanawasiliana na roho mtakatifu..... why hawamuulizi dunia ina umri gni? Je big bang ni kweli?
 
nipe evidence na fact ya big bang theory! halafu uniambie kwa nini hao wanasayansi wenyewe after time wanakanusha hizohizo theories zao. especially big bang thoery.
nilishawahi kumwambia kiranga kuwa big bang theory is the most famous theory not the best/factual theory ya kueleza chanzo cha ulimwengu hadi hivi tunavyoongea hakuna thoery ya kisayansi inayoeleza "ukweli" namna gani ulimwengu umeanza.
wanasayansi nao walewale tu wanakisiakisia tu.
Ni theory and not law... nadharia ambayo bado ipo kwenye utafiti... once proved inakuwa law. Ni sayansi pekee ambayo ikabaini kitu fulani sio kweli inaachana nacho na kumove forward sio dhambi unlike dini zetu.
 
Hii habari tumeshaijadili. Sijui kwa nini umeileta tena. Baada ya hii universe ipo nyingine,baada ya hiyo universe ndiyo ipo ile universe ya watu walioleta space craft kuigundua dunia yetu. Wakafika wakashuhudia sayari takriban 15 zilizototolewa kwenye jua. Wakaondoka,wakarudi baadaye,dunia imeshaanza kuwa ngumu;volcanoes,earthquakes,hurricanes,everything bad. Haikuwezekana kutua .Wakazunguka kutazama halafu wakaondoka. Wanarudi tena baadaye wanatua:watafiti,wanasayansi wanachukua samples za udongo,wanachunguza atmosphere,wanaangusha kwenye dunia chemicals zinazohitajika kuharakisha mabadiliko wanayoyataka. Halafu wanarudi baadaye kuwaleta dinassours. Lazima waanze na dinassours,lazima waanze na bulky animals na bulky trees,kwa sababu the world is young and only crude things can survive on it. Hiyo mimea inabreathe out oxygen,baadaye binadamu wanaweza kuletwa . Halafu wanarudi baadaye,in space ships,wanawaleta primitive human beings,not apes,human beings,and civilization begins. Every few thousand years the atom bomb is discovered,people fight and the world returns to the stone age and civilization begins all over again.
 
Miaka elfu kwa Mungu ni kama siku moja. Miaka ya Mungu hakuna anayejua kwa sababu yeye ni Alfa na Omega na ni mambo machache sana amemfunulia mwanadamu. Miaka yake haijulikani. Ukisoma kitabu cha Ayubu, Mungu alijifunua kwa Ayubu na akamuuliza maswali ambayo Ayubu alishindwa kujibu na kuishia kutubu kwa yale aliyokuwa anamlalamikia Mungu. Tunachotakiwa ni kumcha huyu Mungu aliyeumba Mbingu na Nchi. Biblia inasema mawazo yake siyo mawazo yetu na njia zake siyo njia zetu, kama vile mbingu zilivyojuu sana ndivyo mawazo yake yalivyo. Miaka ya dunia kwa ujumla hakuna anayejua kwa sababu mwanadamu aliumbwa na kuikuta dunia. Wale wasomi wa theology wanasema pia kulikuwepo wanaadamu walioishi katika dunia hii kabla ya adamu. Mwisho ni kwamba miaka ya Mbingu na nchi hakuna anayejua na pia miaka ya Mungu hakuna anayejua. Tafuta yale yanayokupeleka umwabudu Mungu aliye hai hayo mengine umwachie Mungu maana majibu mengine hatuna. Biblia inasema yale aliyomfunulia mwanadamu ni hili mwanadamu hayafanye na yale ambayo ameyaficha hayo ni ya kwake hayatuhusu.
 
Back
Top Bottom