Umri umeenda, nataka kuoa ila kimaisha sijajipanga naombeni ushauri pa kuanzia

Kama mchumba unae kwanini usimzalishe? Vijana siku hizi akiona hakueleweki anamzalisha binti hlf kubariki ndoa inakuja badaye, sasa wew unataka ufunge ndoa kama mtoto wa Kimei! Shaur yako

Au unataka ujenge nyumba ya milion 200 ndy useme utakubalika?

Unatakiwa uanze hapo hapo ulipo
Huyo Muwoga wa Maisha na ana ndoto za alinacha ndiyo maana atachelewa sana asipo iishi uhalisia wake!!
 
1. Usioe aliyekuzidi elimu
2. Usioe mke ambao kwao wapo mambo safi saaaana hutofikia her expectations atakusumbua
3. Kaoe kijijini kwenu mtoto aliyemaliza la saba au aliyeishia form three D
4. hakikisha unayemuoa unamfungulia kajigenge akusaidie maisha.
5. Huyo uliyenaye unajua ni kwa nini bado upo naye? changanya na za mbayuwayu
Yaani wwe bado unataka kumzidishia umasikini,Kama kwa Mchumba wake kuna furusa bora azitumie kupanda kiuuchumi kuliko kwenda kijijini na kuchukua Mzigo zaidi!! Lakini akiona Mchumba haeleweki ampige chini faster afanye mipango mingine!!
 
Daa hili ni tatizo kubwa sana hasa kwa wengi walio graduate, ngoja niendelee kusoma comments za wadau.
 
Changamoto kubwa wanakutana nao vijana wanapotaka kuanza maisha huwa sio swala la mahari, au kukosa pesa ya kufanya harusi yenyewe especially wale wanaofanya harusi ya gharama.

Shida huwa ni moja, vijana wengi huwa wanashindwa kujitambulisha ukweni kwasababu za kiuchumi.

Wazazi especially wa mtoto wa kike huwa hawapendi kuona binti yao anaanzia chini especially kama walimsomesha kwa shida. Huwa wanataka aanze na kijana ambaye yupo vizuri kimaisha.

Hii ni stigma ambayo vijana wengi wa kiume wanatembea nayo moyoni pale wanapokuwa hawana maisha yenye uelekeo.

Hili ni tatizo. Wazazi huwa wanachangia sana kuwavurugia vijana wao future kutokana na matakwa yao binafsi. Wazazi hawa hawa ndio huwa wanawaambia mabinti kuwa wanaume ni mashetani, wazazi hawa hawa ndio huwa wanawaambia mabinti zao kuwa ni marufuku kuolewa na mtu ambaye hana pesa au mwenye maisha ya kawaida. Wazazi hawa hawa ndio huwa wanaambia binti zao wakipata kazi wasielekeze bidii kwenye kujenga maisha na wanaume sababu mbeleni wataachwa badala yake huwahimiza kujitafutia mali binafsi kama viwanja, nyumba na biashara wakiwaandaa kisaikolojia kuharibu ndoa badala ya kuijenga.

Ndio maana leo vijana huwa wanapata kigugumizi sana kwenda kujitambulisha au inawalazimu kujiumiza kwa kujitutumua kwa mali au pesa wasizoziweza kujimudu nazo.

Imagine mtu anakopa milioni 15 ili tu kusimamia ndoa kuanzia send off ya mwanamke na gharama za harusi kisha wanaingia kwenye ndoa na hali ya madeni na purukushani za maisha.
So kimsingi wazazi wa pande zote hebu leave these kids alone jamani if necessary. Kama. Watoto wanapendana na wanalindana why don't give them your full support....

Na wala haitaki uwe mzazi mwenye pesa bali sapoti muda mwingine ni kuachana na mawazo ya ubinafsi na uwajali hawa watoto kwa kuwapa baraka za kuanza pamoja. Kama hawajiwezi basi jaribuni hata kuwapa msaada wa mawazo na wa mali pa kuanzia..... Kumbuka huyu kijana au binti ndie anakwenda kukutunzia mwanao wa kike /wakiume kipindi wewe unazeeka.

Wazazi wa namna hii mnawapa mitihani hawa vijana na wengi wao wanakwama hapa hadi wanaishia kuzaa na binti zenu kiwizi wizi na kuwatelekeza sababu ya changamoto za maisha.

Kuoa sio tukio la gharama ni sisi wanadamu tumeamua kulifanya kuwa hivyo. Ndoa inataka tu, sapoti ya wazazi kujiridhisha kuwa binti yao anakwenda kufanya maisha na mtu mwenye uelekeo wa maisha na si mwenye vitu na vigezo wanataka.
Binti yenu ndie aneolewa ninyi hamuolewi. Waache wakajipange na kufanya maisha yao..... Wasapotini kwa kile mnaweza kiroba cha mahindi na mashuka na sufuria pia ni zawadi ya heshima toka kwa wazazi kwa vijana wanaokwenda anza life.
Acheni kuwajaza hawa mabinti hofu za kijinga sijui huyu kijana kama hana kazi na maisha hataweza kukuhudumia na kutunza familia, wewe mzazi umekuwa mtoa riziki tena?!

Sasa ona kijana kama huyu mleta mada, anaamini hawezi kupata mtoto, wala kuwa na mke sababu hana kipato, tokea lini watu wanaanza maisha wakiwa na pesa na kipato cha uhakika?!
 
Angekuja wa kike mwenye 33 aseme kama wewe hana ndoa na hana uelekeo wa maisha hadi sasa tungekuwa tunakimbilia comment ya 50+ na kashfa za kutosha.....hakuna rangi asingeiona kwenye hizo comment

Life ain't fair

Endelea kupambana na maisha,hata kama umechelewa isikupe pressure ya kushindwa kuzidi kupambana na maisha
But wanawake wengi waliokwama kimahusiano ni kuchagua na wao kutaka.
 
Mkuu hata kumuhudumia chakula na malazi dudu litahusika?

Mwanamke anahitaji dudu tu, hayo mengine yote yanavumilika.... labda ukwapue wa kishua asiyejua shida.

Tatizo ni mkumbo na maigizo ya kuishi mjini kwa matarajio makuuubwa, rudi kijijini kwenu wadogo zako wote wameshaoa... hawana hata hicho kipato chako ila wanaendesha familia zao vizuri tu.
 
Mwanaume kujiandaa ni bichache sana wewe uwe na godoro, shuka 2 jiko lolote na kupanga chumba maisha yanaanza

Huwezi jua itakayemuoa ndo atakupa changamoto ya kufanikiwa

Mie nilianza na kitanda jiko sefuria mbili, godoro na stuli mbili

Maisha yanasonga usiogope Kama mwanaume
 
Back
Top Bottom