Umri umeenda, nataka kuoa ila kimaisha sijajipanga naombeni ushauri pa kuanzia

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,637
Umri wangu kwa sasa ni miaka 33 siku si nyingi nitakuwa 34 umri wangu kila nikijiangalia umekwenda mno kwani mpka hivi sasa

1.sina mtoto

2.sijaowa wala sina familia

3.kimaisha bado sijasimama vizuli

4.mchumba ninae ila nina wasiwasi sijui kama Kwao watamkubalia kuolewa na kijana ambae kimaisha bado hajasimama vizuli maana sina ajira na biashara zangu ndo vile za kubahatisha.

Wadau zangu naombeni ushauli presha ya umri wangu kusonga mbele huku nikiwa hakuna nilichokifanya roho huwa inaniuma.
 
Anza sasa jikubali hujachelewa bado.
 
Kama mchumba unae kwanini usimzalishe? Vijana siku hizi akiona hakueleweki anamzalisha binti hlf kubariki ndoa inakuja badaye, sasa wew unataka ufunge ndoa kama mtoto wa Kimei! Shaur yako

Au unataka ujenge nyumba ya milion 200 ndy useme utakubalika?

Unatakiwa uanze hapo hapo ulipo
 
Angekuja wa kike mwenye 33 aseme kama wewe hana ndoa na hana uelekeo wa maisha hadi sasa tungekuwa tunakimbilia comment ya 50+ na kashfa za kutosha.....hakuna rangi asingeiona kwenye hizo comment

Life ain't fair

Endelea kupambana na maisha,hata kama umechelewa isikupe pressure ya kushindwa kuzidi kupambana na maisha
 
1. Usioe aliyekuzidi elimu
2. Usioe mke ambao kwao wapo mambo safi saaaana hutofikia her expectations atakusumbua
3. Kaoe kijijini kwenu mtoto aliyemaliza la saba au aliyeishia form three D
4. hakikisha unayemuoa unamfungulia kajigenge akusaidie maisha.
5. Huyo uliyenaye unajua ni kwa nini bado upo naye? changanya na za mbayuwayu
 
Kijana pambana kuanzia sasa wala hujachelewa kabisa kama unaweza zaa nae tu muanze maisha kikubwa ridhiki ya kula mnapata usiwe na ofu juu ya familia ya binti na jamii kwa ujumla kikubwa angalia maisha yako na mungu atakubariki ndoa itafungwa hata badae huko
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom