Mchumba wangu anahitaji tuzae mtoto wakati mie mwenyewe kimaisha bado sijasimama

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,688
2,000
Nina mchumba wangu huyo amekuwa akinishawishi tuzae mtoto upande wangu kiukweli kimaisha bado sijasimama hapa nilipo ninawaza hiyo mimba nitaileaje mtoto nitamleaje wakati kipato changu chenyewe hakieleweki lakini pia kwao sijulikani na yeye kwetu hatambuliki.

Lakini binti amekomaa tuzae mtoto ananiambia tusichelewe sana sababu ya umri wetu umeenda haya mambo mengine yatajiseti mbele kwa mbele mpaka sasa sijachukua maamuzi yeyote yale ila tuu naombeni ushauri mzuri wa busara kutoka kwenu makonki wa JF.

Uamuzi upi sahihi wa kuchukua tuzae tuu au tuendele kusubili wakati sahihi japo mwenzangu ana kiu ya kupata mtoto.

1627992537814.png

 

kuku sharo

Senior Member
Aug 13, 2020
143
250
Sasa huyo mtoto unaeogopa asizaliwe wakat huu, akizaliwa ndo atakua anakula magunia ya msosi kwa siku?, au ndo atakua kama jini anaamka usiku anameza pesa yako hyo kidogo unayoipata kwenye mishe zako!

Ngoja sasa we si unajifanya et hautaki kuitwa baba sasa hvi, unajifanya una magumu wakati bi dada ndo kaiva kunyonyesha, subili wenye hamu ya kuitwa baba waje wafanye yao, wakusaidie kupachika mtoto!

Halafu yakikukuta ya kukukuta usirudi hapa kutupgia kelele, upambane na hali yako hukohuko maana haujielew! Kuna watu wanashikishwa mavuno ya starehe za watu, leo wew unaombwa eti had uje kuomba ushauri hapa!
 

Luvanga1

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
2,013
2,000
Ngoja nikwambie kitu ndugu yangu.... Mtoto ni Baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Usiogope kisa huna mishe za kueleweka, God's good.

You never know, kupata kwako mtoto ndio mambo yako kuwa sawa, na Mungu analeta maajabu yake kwa mtu yoyote
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom