Umoja wa vyuo vikuu Mwanza watangaza kumuunga mkono Lowasa

Umoja wa vyuo vikuu Mwanza watangaza kumuunga mkono Lowasa

Aibu aibu.ni wanafunzi wa chekechea au vyoo vikuu? Tanzania yangu mbona watoto wako hawajitambui? nani kawaloga? Naililia Tanzania ijayo kama ni wasomi wanamna hii TWA FA
 
Hawa sio wanachuo ni walevi vijana waliohongwa viloba na ubwabwa ili waseme hovyohovyo. Hongereni mnaojiita wachuo kwa kuhongwa ka waliii.
 
Halafu kuna ujinga huu wanakweza eti yeye ndiye mwasisi wa shule za kata! Waongo wakubwa hawa labda vijijini kwao, binafsi kata yangu huko Mbeya Rungwe shule ya kata ninayotoka imeanzishwa mwaka 2004 ambapo Lowassa wala hakuwa waziri mkuu hali kadharika UDOM kimeanza kujengwa kipindi cha mkapa. Watanzania acheni kumwita jambazi kwa jina la msafi.

Kimsingi wale wanaomshabikia Lowassa nafikiri watufute sera nyingine sio ya kusema kuwa Lowassa alianzisha shule za kata, ilhali hili swala lilianza toka Mkapa akiwa raisi kutokana na hitajiko hilo ndiyo walimu walijulikana kama voda vasta wakaanza kuajiriwa kukidhi hitaji la walimu katika mashule ? Na kama Lowassa ndiye mwanzilishi wa shule za Kata basi aliyestahili heshima Hizo ni waziri wa elimu wa wakati huo. Na kama Lowass anastahili heshima hiyo kwa vile alikuwa Waziri mkuu wa wizara zote basi anstahili lawama katika kufeli kwa wizara za afya ,maji,kilimo na ajira ambazo ndiyo kero tunazotaka aje kutokomboa



Ndugu yangu kila mtu ana waza anavyojua na anapima mwwnyewe yale yanayosemwa.
Lowasa amekuwa waziri mkuu kwa miaka miwili.

Lowasa anasifiwa kwa namna alivyo na uwezo wa kushawishi watu namna ya kuchangia maendeleo yao wenyewe.
Kumbuka hata matamasha alipigwa marufiku baada ya mahasimu wake kujaribu kuhamasisha matamasha na wakajikuta hakuna muitikio toka kwa wananachi.

Mfano upo pia kwa Magufuli yupo kwenye uwaziri wa ujenzi kwa zaidi ya miaka 15 leo hii barabara zote zinaitwa za Magufuli. Je,tuwatukane watu kwa sababu tu barabara zilianza kujengwa tangu enzi za mkoloni?
Mfano mwingine ni Prof.Mhongo aliyekaa kwa muda mfupi kwenye wizara ya nishati na madini na kusimamia kasi ya kupeleka umeme vijijini ,leo hii umeme unaitwa wa Muhongo. Mbona umeme vijijini ulianza tangu enzi za Nyerere? Watu wanaopenda kuona maendeleo wanaangalia kasi na nia thabiti ya kusimamia mradi husika lakini wanafiki na wapenda majungu wanaangalia mapungufu yanayojitokeza wakati wa kutekeleza majukumu ya kibinadamu.
Hata Nyerere anayeimbwa usiku na mchana kuna mambo mengi sana alishindwa kuyasimamia kwa ufanisi na yalikuwa ni mwanzo wa matatizo tunayoyaona leo lakini wenye akili zao wanaachana na yale mabaya wangaza na kukumbuka mema yake.
 
Taarifa kupitia chanel ten hivi punde imeonesha wanafunzi wa vyuo vikuu kwa umoja wao wakipaza sauti kumtaka Lowasa agombee urais na wapo nyuma yake..

The saga continues.. Sasa hivi hawamfati wanatamkia huko huko!!!

Vyombo vya habari vijitahidi kuweka rekodi vizuri.huo ni umoja wa wanafunzi wa ccm wa vyuo vikuu sio umoja wa vyuo vikuu kana kwamba ni wote
 
kaka chuo chako kipo na kiongozi mmoja jina lake la mwanzoni ni ndug. Christopher ndio alikuwa ana toa hotuba kwa niaba ya wana SAUT
 
Wasomi wengine wameumbwa kwa ajili ya kutuletea matatizo hapa nchini kwani mfano hai si up kwa yule rubani msaidizi wa ndege ya kijerumani aliyegongesha ndege ! sasa na hao wasomi wa mwanza maboya sanaaa kwanza wanaaibisha efforts za makamanda kama heche, machali
 
ww ndo hujitambui na mjinga kwan daima mjinga hajitambui na kukarir kumekuathir na weng wenu mnao mchukia lowasa n mafund wa kukarr na co kuelewa pole xana

Aliyekuzaa Nadhani Ndiyo Mjinga Kwa Kutuletea Watanzania Bomu Kubwa Aina Ya POPOMA Kama Wewe Na Hiyo Pole Jipe Mwenyewe.
 
Kuna maandishi kwenye daladala yanasema"usiyempenda kaja". Naona Mwaka huu huu msemo utahamia kwenye siasa.

Kaka Manyerere Fafanua Zaidi ILA Sishangai Wewe Kuwa Kwa Team EL Na Umemuambukiza Hadi Mtani Wetu Mhaya Balile. EL Kakupa Tsh Ngapi?
 
Dah....eti hadi waziri mkuu wa sautso nae bila hata chembe ya aibu anatutamkia..... I'm so ashamed of my saut student org.
 
Back
Top Bottom