Umoja wa vyuo vikuu Mwanza watangaza kumuunga mkono Lowasa

Umoja wa vyuo vikuu Mwanza watangaza kumuunga mkono Lowasa

Wewe ndo mwendawazimu mwenye,utamuitaje mwendawazimu mtu mwenye akili zake?Nafili darasa lako halikuweza kukusaidia ktk maisha yako.
 
Badala ya kuhamasishana wasome kwa bidii ili kupunguza hizo lower class kwa GPA zao wao wanakazania hao wanasiasa..kiukweli hao wakiwa madarakani hawana jipya ndg zanguni watoto wa wakulima wenzangu.
Nyiw komaeni na desa zenu GPA ziitikie mwito.
 
Ni sifa gani kuubwa aliyo nayo EL hadi watu wampigia kifua cha uraisi?

Niliwahi kusikia wengine wakisema eti ana maamuzi magumu! Ptuuu! Mimi binafsi sikubaliani na hoja kama hii kumuingiza mtu Ikulu. Alishawahi kuwa kiongozi mbona hayo maamuzi magumu hatukuyaona yakilibadilisha taifa hili angalau kutoka nchi masikini sana na kuwa nchi inayoendelea? Ok, hata tukikubali kwa shingo upande kuwa ni kweli ana maamuzi magumu. Hivi ukiwa na maamuzi magumu halafu watendaji wako wooote wana maamuzi mepesi utaweza kufanya lolote?

Nikubaliane na mdau mmoja alieaandika kuwa ukiamka leo ukawaambia watanzania kuwa kazi ya kuandikisha wapiga kura imeshakamilika kwa asilimia 95 na tar 30 katiba itapigiwa kura watakubali na kupiga vigelegele.

Halafu kuna ujinga huu wanakweza eti yeye ndiye mwasisi wa shule za kata! Waongo wakubwa hawa labda vijijini kwao, binafsi kata yangu huko Mbeya Rungwe shule ya kata ninayotoka imeanzishwa mwaka 2004 ambapo Lowassa wala hakuwa waziri mkuu hali kadharika UDOM kimeanza kujengwa kipindi cha mkapa. Watanzania acheni kumwita jambazi kwa jina la msafi.
 
Hii imesukwa na antony diallo huyu ni mtandao wa lowasa kwa kanda ya ziwa. Wanachotakiwa kutambua ni kwamba rais wa nchi hapatikani kwa presha za kuwaaminisha watanzania kuwa lowassa ndio mtu anayekubalika nchi hii.ccm mtafanya kosa kubwa sana kumpa mtu uongozi alioununua kwa fedha zake mwenyewe mtatufanya tujute kuwa watanzania.
 
Kutoka kutoa zawadi ya pasaka mpaka kumtangaza lowassa kuwa chaguo sahihi la kuwa rais. Ha ha ha ha hii kawashikeni masikio wajinga.
 
Kimsingi wale wanaomshabikia Lowassa nafikiri watufute sera nyingine sio ya kusema kuwa Lowassa alianzisha shule za kata, ilhali hili swala lilianza toka Mkapa akiwa raisi kutokana na hitajiko hilo ndiyo walimu walijulikana kama voda vasta wakaanza kuajiriwa kukidhi hitaji la walimu katika mashule ? Na kama Lowassa ndiye mwanzilishi wa shule za Kata basi aliyestahili heshima Hizo ni waziri wa elimu wa wakati huo. Na kama Lowass anastahili heshima hiyo kwa vile alikuwa Waziri mkuu wa wizara zote basi anstahili lawama katika kufeli kwa wizara za afya ,maji,kilimo na ajira ambazo ndiyo kero tunazotaka aje kutokomboa
 
Acha UPOPOMA Mkuu! Ktk Umoja Wako Huo Wa Vyuo Vikuu Hebu Kitoe Na Nina Uhakika Chuo Kikuu Changu Pendwa SAUT Hakipo Na Hakithubutu.

ww ndo hujitambui na mjinga kwan daima mjinga hajitambui na kukarir kumekuathir na weng wenu mnao mchukia lowasa n mafund wa kukarr na co kuelewa pole xana
 
Hii imesukwa na antony diallo huyu ni mtandao wa lowasa kwa kanda ya ziwa. Wanachotakiwa kutambua ni kwamba rais wa nchi hapatikani kwa presha za kuwaaminisha watanzania kuwa lowassa ndio mtu anayekubalika nchi hii.ccm mtafanya kosa kubwa sana kumpa mtu uongozi alioununua kwa fedha zake mwenyewe mtatufanya tujute kuwa watanzania.

Thibitisha kauli yako kwamba ni kweli dialo ndo kawapeleka wanavyuo pale na ukishindwa kufanya hivyo nakusihi sana uache kutaja majina ya watu hovyo hovyo
 
Kuna maandishi kwenye daladala yanasema"usiyempenda kaja". Naona Mwaka huu huu msemo utahamia kwenye siasa.
 
Huo uamuzi wameufikia lini? Hatujapiga kura, hatujakaa tukaona wengi wanasemaje sasa umoja wa vyuo gani labda?
 
ww ndo hujitambui na mjinga kwan daima mjinga hajitambui na kukarir kumekuathir na weng wenu mnao mchukia lowasa n mafund wa kukarr na co kuelewa pole xana

xana ndio nini? Nafikiri wewe ndio hujielewi na nashawishika hujui hata huyo lowasa unamuunga mkono kwa sababu zipi bali unafuata mkumbo tu kama walivyo wengi humu na hao wanafunzi.poleni sana kama wafuasi wake ndio nyie.
 
Huo ni mwendelezo wa vimbwanga na kujikosha kwa wanachuo wa SAUT,CBE & BUGANDO
 
Mwanza vyuo vyote vibabeba div3 na div 4 kama UDOM, sasa hapo unategemea nini mkuu?




Nimeshagundua kuwa humu jamii forum kuna watu wenye mihemko tu sio great thinkers.

Division ya mtu inahusiana nini na ushabiki wa mtu.
Mbona hata mpira kuna wanaoishabikia manchester wengine Chelse ,wengine Arsenal n.k. Kila mtu na mapenzi yake huo ndio uhuru wa mawazo na demokrasia.
Leo hii mtoto wa mkulima anayesoma shule ya kata hawezi kufaulu sawa na mtoto wa tajiri anayesoma Tusiime hata kama uwezo wao wa kiakili upo sawa.

Kwa taarifa yako kama una mgombea wako anayefikiri kuwa atakubalika kwa kutumia watu wenye Division one ujue amepotea njia.Mageuzi na mapinduzi siku zote yanafanywa na watu wa kawaida waliochoka kunyanyaswa na wasomi wa ana yako na wenye dharau.
Ni wasomi wachache sana wanaowaza kulikomboa Taifa.Wasomi wwngi wanawaza maisha yao yawe mazuri tu hata kama wengine wanaumia.
Hata ikitokea vita wasome wako tayari kuhama nchi na sio kuipigania hata kama wangekua jeshini wakiambiwa wasonge mbele wanaufyata. Wanasubiri nchi iwe na amani ili wagombee madaraka.Wakipata madaraka wanachoangalia ni kugawana mishahara minono hawajali tena wanyonge.
 
Umoja wa wanachuo mkoani mwanza nao wamejitokeza kumuunga mkono lowasa ktk mbio za urais

Wanasema anaweza,anastahili na wapo pamoja nae,wakiongea wakiwa ktk shughuli ya kuchangia wasiojiweza wamedai kwamba lowasa alipambana ktk suala la elimu hivyo wanamuona ni mkombozi wao
Hivyo wanamtaka asisite kuchukua fomu muda utakapo fika

Source:chanel ten habari saa 1 usiku

My take: hawa ni wasomi wasiojitambua

Wanao jitambua ni wale tuu wanaosema Mbowe kichwa kizuri cha siasa, tundu lissu ni mwanasheria mzuri, mnyika amechafua hali ya hewa bungeni.
 
Back
Top Bottom