Umoja wa Mataifa wajitosa sakata la Ben Saanane

Umoja wa Mataifa wajitosa sakata la Ben Saanane

Hapo ni wanapoteza muda tu kila nchi ina internal affairs zake...so , hao UN hata wakija watakuwa kama wapiga zumari tu wa ufipa.
Internal affairs zipi zisizofuata human rights?.....

Shida ya CCM mnajisahau sana utadhani ninyi ndo mliumba Dunia.

Hakika ipo siku mtasema mna Mungu wenu huyu Mungu wa wote si wenu!
 
Internal affairs zipi zisizofuata human rights?.....

Shida ya CCM mnajisahau sana utadhani ninyi ndo mliumba Dunia.

Hakika ipo siku mtasema mna Mungu wenu huyu Mungu wa wote si wenu!

Kwahiyo mshabadilisha gia angani , maana niliona mkimuhimiza mwenyekit alete mtu wenu ila kawapa bakshishi na peremende kidogo mshaanza kujifanya mmemsahau Ben.

Swali la kizushi, hivi mwanao akipotea mwenye jukumu la kumtafuta ni Jirani yako au wewe Mzazi, maana alikuwa Salange wa mwenyekit wa ufipa na ndo ilibidi wambane mshua Wazo awaoneshe wana ufipa Ndugu yao Ben alipo, matokeo yake leo jirani (Lumumba) ndo kapewa kandarasi ya Lusaka mtoto wa familia nyingine , hivi ni sawa kweli Ku skepgoat na kuamua kumlalamikia Jirani yako kwa kupotea kwa mwanao. Tafakari chukua hatuna.
 
Sakata la kupotea kwa mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa Chadema, Ben Saanane limechukua sura nyingine baada ya Umoja wa Mataifa (UN) kusema upo tayari kutuma watu nchini kwa ajili ya uchunguzi.

Saanane, ambaye pia ni msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alipotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba 18 mwaka jana na hadi sasa haijaeleweka kuwa alitekwa au kuuawa, ingawa CHADEMA imehusisha kutoweka kwake na taarifa ambayo Saanane aliitoa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utata wa elimu ya baadhi ya viongozi.

Siku chache baada ya kupotea kwa Saanane, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu aliitaka Serikali kueleza kama inamshikilia kada huyo au ifanye uchunguzi wa kina kuhusu kupotea kwake.

Sanjari na hilo, Lissu aliitaka Serikali kufuatilia ujumbe wa vitisho ambao Saanane aliwahi kutumiwa kwenye simu yake ya mkononi na mtu ambaye bado hajafahamika.

Akisisitiza msimamo wa chama chake, Lissu alizitaka mamlaka zote husika na usalama wa raia ziseme hali halisi inayozingira sintofahamu ya mahali alipo, ikiwa yuko ndani ya nchi au nje, au hata kama amefariki na kuzikwa kwa kutotambuliwa.

Wakati utata huo ukiendelea, ofisi ya kamishna mkuu wa haki za binadamu duniani ya UN yenye makao yake makuu jijini Geneva, Uswisi, imesema iko tayari kutuma timu wa uchunguzi.

Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano uliotishwa na ofisi hiyo, Kanda ya Afrika uliohusisha nchi za Sudan, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Ethiopia, Djibouti na Tanzania.

Akizungumza na gazeti hili jana, mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo- Bisimba alisema suala hilo liliibuka baada ya wajumbe wa mkutano huo kutaka kujua undani wa sakata hilo, lakini hakukuwa na taarifa za kina.

“Wajumbe walionyesha kuguswa na suala la mtu kupotea katika mazingira ya utata na kutaka tuelezee kwa undani ilivyokuwa. Hatukuwa na taarifa za kina hivyo wakasema wako tayari kulifanyia kazi endapo tutatuma urgent alert,” taarifa ya dharura.

“Taarifa tutakayotuma ndiyo itakayowawezesha wao kutuma timu ya uchunguzi ije hapa baada ya hapo watajua ni kitu gani waseme kwa Serikali.”
Dk Bisimba alieleza kuwa bado taarifa hiyo haijaandikwa kutokana na kuwasubiri ndugu wa Saanane ambao wanatakiwa kutoa maelezo kwa kina.

“Tuliwaambia ndugu zake waje tupate maelezo yatakayotuwezesha kuandika hiyo urgent alert, lakini bado hawajaja. Watakapofika tutaandika na kuituma ili uchunguzi ufanyike.”

Alipotafutwa kuhusu maendeleo ya uchunguzi wa suala hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI), Kamishna Robert Boaz alisema: “Nitafute Jumatatu kwa sasa nipo kwenye kikao.”
Inogile
 
[HASHTAG]#freebensaanane[/HASHTAG]
 
Hakuna lolote, kuna nchi zingine watu maelfu wanapotea kila mwaka na hakuna cha UN wala nini.
 
Kwa nini hao ndugu zake hawajaenda kutoa hiyo taarifa kama walivyoombwa?
 
OK wasiliana na mamlaka husika zichukue hatua stahiki

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
Hivi kama mbowe ni suspect number moja tatizo nini asihojiwe,mbona kwenye drama za ngada walimkamataa?.

Kuna jamaa mmoja huko fb ambae aliku usalama wa taifa sasa yuko ugaibuni,nae kila siku anahangaika na mbowe kua ndo muhusika.kwa nini hadi leo police wako kimya?,hivi chadema/ mbowe ni mafia kiasi hiki kuvishinda vyombo vyote vya ulinzi na usalama tanzania?,kama jambo la ben tu lina washinda tukihoji weledi wao nao utaitwa uchochezi?.

Ingekua ni maandamano ya upinzani majeshi yote yangesha anza zile mbwembwe zao za kujigalagaza barabarani wakiwa na juice kwenye vi bags vyao.kazi kutuvizia tu humu jf.shame

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
CHADUMA Malalamiko yenu mengi sana, mara ben, mara kuibiwa kura, mara rais atangaze baa la njaa, hebu kuweni na hoja madhubuti ili wawaelewe, make inefikia kipindi hadi hawaon mwelekeo
Zote ni hoja zisizojibiwa kila day zinaongezeka tena ongeza na la vyeti hewa mkuu mbona haihitaji shule au wew team ngumbaro[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi ni kwanini mtu akianzisha thread humu JF siku hizi watu hawaulizi hata source(Chanzo)???,.. Mtu anatunga story zake na ka smartphone kake chumbani eti "UN yaingilia kati swala la Ben Saa9",.. hamjiulizi UN kitengo gani?,maana ina vitengo vingi,kupitia kwa wizara ipi ya TZ,habari imetolewa TV gani au mwandishi gani alikuwepo,na aliyeleta story hapa ameipata wapi?,matokeo yake watu wanakimbizana kubishana humu kumbe chanzo ni - THE CERTIFIED (Unverified user),au ndo yale yale ya unabisha nini wakati MANGE katwambia?
 
Back
Top Bottom