Umoja wa Mataifa wajitosa sakata la Ben Saanane

Umoja wa Mataifa wajitosa sakata la Ben Saanane

Hivi ni kwanini mtu akianzisha thread humu JF siku hizi watu hawaulizi hata source(Chanzo)???,.. Mtu anatunga story zake na ka smartphone kake chumbani eti "UN yaingilia kati swala la Ben Saa9",.. hamjiulizi UN kitengo gani?,maana ina vitengo vingi,kupitia kwa wizara ipi ya TZ,habari imetolewa TV gani au mwandishi gani alikuwepo,na aliyeleta story hapa ameipata wapi?,matokeo yake watu wanakimbizana kubishana humu kumbe chanzo ni - THE CERTIFIED (Unverified user),au ndo yale yale ya unabisha nini wakati MANGE katwambia?
Kwa hiyo unataka chanzo ety?? kama huoni chanzo hukutakiwa kucomment ngoja nikitafte alafu utakuja
 
Usinifanye nikapewa ban kisa wewe mpuuzi mmoja tu nadhani hata wewe ungeandika story yako ukaweka chanzo unaishi kwa kukalili tu unafikili mimi kutokua verfied nitaweka upuuzi humu kama upuuzi wako?
 
Kwa hiyo unataka chanzo ety?? kama huoni chanzo hukutakiwa kucomment ngoja nikitafte alafu utakuja
Ndio mkuu naulizia chanzo cha hii habari,.,cha ajabu umeleta thread humu halafu ndo unaenda kutafuta chanzo.Tuwekee link na sisi tuone,weka hata link tu.Ben Saa8 anajulikana humu JF tu,hata mitaani watu hawana time ni nani,wamepotea watu kibao duniani tena muhimu,sana sana ni serikali zao ndo huwa zinahaha kuwatafuta,usiichukulie UN kimchezo mchezo ina majukumu mengi na kazi nyingi za ku deal nazo za ki dunia.
 
Waulize Mods kwanini jana wakati naweka uzi huu walitoa chanzo cha habari mimi nilifanya kama inavyopaswa kufanywa wala mimi sio mgeni wa jf najua kila kitu na sheria zake so hilo swali uliza Mods
 
Sakata la kupotea kwa mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa Chadema, Ben Saanane limechukua sura nyingine baada ya Umoja wa Mataifa (UN) kusema upo tayari kutuma watu nchini kwa ajili ya uchunguzi.

Saanane, ambaye pia ni msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alipotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba 18 mwaka jana na hadi sasa haijaeleweka kuwa alitekwa au kuuawa, ingawa CHADEMA imehusisha kutoweka kwake na taarifa ambayo Saanane aliitoa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utata wa elimu ya baadhi ya viongozi.

Siku chache baada ya kupotea kwa Saanane, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu aliitaka Serikali kueleza kama inamshikilia kada huyo au ifanye uchunguzi wa kina kuhusu kupotea kwake.

Sanjari na hilo, Lissu aliitaka Serikali kufuatilia ujumbe wa vitisho ambao Saanane aliwahi kutumiwa kwenye simu yake ya mkononi na mtu ambaye bado hajafahamika.

Akisisitiza msimamo wa chama chake, Lissu alizitaka mamlaka zote husika na usalama wa raia ziseme hali halisi inayozingira sintofahamu ya mahali alipo, ikiwa yuko ndani ya nchi au nje, au hata kama amefariki na kuzikwa kwa kutotambuliwa.

Wakati utata huo ukiendelea, ofisi ya kamishna mkuu wa haki za binadamu duniani ya UN yenye makao yake makuu jijini Geneva, Uswisi, imesema iko tayari kutuma timu wa uchunguzi.

Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano uliotishwa na ofisi hiyo, Kanda ya Afrika uliohusisha nchi za Sudan, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Ethiopia, Djibouti na Tanzania.

Akizungumza na gazeti hili jana, mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo- Bisimba alisema suala hilo liliibuka baada ya wajumbe wa mkutano huo kutaka kujua undani wa sakata hilo, lakini hakukuwa na taarifa za kina.

“Wajumbe walionyesha kuguswa na suala la mtu kupotea katika mazingira ya utata na kutaka tuelezee kwa undani ilivyokuwa. Hatukuwa na taarifa za kina hivyo wakasema wako tayari kulifanyia kazi endapo tutatuma urgent alert,” taarifa ya dharura.

“Taarifa tutakayotuma ndiyo itakayowawezesha wao kutuma timu ya uchunguzi ije hapa baada ya hapo watajua ni kitu gani waseme kwa Serikali.”
Dk Bisimba alieleza kuwa bado taarifa hiyo haijaandikwa kutokana na kuwasubiri ndugu wa Saanane ambao wanatakiwa kutoa maelezo kwa kina.

“Tuliwaambia ndugu zake waje tupate maelezo yatakayotuwezesha kuandika hiyo urgent alert, lakini bado hawajaja. Watakapofika tutaandika na kuituma ili uchunguzi ufanyike.”

Alipotafutwa kuhusu maendeleo ya uchunguzi wa suala hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI), Kamishna Robert Boaz alisema: “Nitafute Jumatatu kwa sasa nipo kwenye kikao.”
Jamani msitujazie server yetu JF. Suala LA Ben kwa yeyote anayetaka kulifufua basi aanzie kwa Mzee Focus Saanane ambaye ni Baba Mzazi wa Ben. Yeye alisema bila kumung'unya Maneno akimtaka Mbowe amlete mwanae akiwa hai. Sasa tumuulize amefikia wapi mbona kimya...
Au kaishwanong'onezwa mapema akae kimya baada ya kuujua Mchezo!?
Hata Huyo Bisimba kama kweli atawasiliana na familia anaweiza kuishia kupotezea tu kama familia ilivopotezea.
 
Lazima tuseme ukweli hata kama tutapotezwa wote but Tanzania is one and only one country tukiacha hii inchi ikavurugwa na mtu mmoja ni wapi tutakwenda!
 
Hapo ni wanapoteza muda tu kila nchi ina internal affairs zake...so , hao UN hata wakija watakuwa kama wapiga zumari tu wa ufipa.
Siku nyingine mengine soma tu inatosha sio kuandika ujinga kama huu
 
Jamani msitujazie server yetu JF. Suala LA Ben kwa yeyote anayetaka kulifufua basi aanzie kwa Mzee Focus Saanane ambaye ni Baba Mzazi wa Ben. Yeye alisema bila kumung'unya Maneno akimtaka Mbowe amlete mwanae akiwa hai. Sasa tumuulize amefikia wapi mbona kimya...
Au kaishwanong'onezwa mapema akae kimya baada ya kuujua Mchezo!?
Hata Huyo Bisimba kama kweli atawasiliana na familia anaweiza kuishia kupotezea tu kama familia ilivopotezea.
Yale Maji wanayofulia Chupi za kike ndio ulinyweshwa wewe
 
Mkuu Mshana hivi hatuwezi kuunganisha nguvu tukatumia zile rada za usiku za kiasili kujua nini kilitokea, je kwa sasa yupo wapi na je ni hai au mfu na kina nani walitekeleza hayo. Mimi nafikiri zinaweza kusoma tukapata pa kuanzia.
 
Inawezekana kabisa ila shughuli yake pevu
 
Back
Top Bottom