Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,180
- 10,904
Umoja wa kundi la kiuchumi la BRICS lililoasisiwa na China na Urusi limeonekana kukua na kutishia uhai wa umoja wa mataifa na maslahi ya taifa la Marekani.
Hayo yameeleweka wakati umoja huo ukikaribia kufanya kikao chake mwezi Juni mwaka huu huko Afrika Kusini..
Balozi wa BRICS wa Afrika kusini Anil Sooklal amesema umoja huo umekuwa ukipokea maombi mapya kutoka nchi za Afrika na Mashariki ya kati. Kwa sasa wana maombi kutoka nchi 16
Umoja huo awali mwaka 2001 ulipoundwa ulizikushanya nchi za Brazil, Russia, India China kabla ya Afrika kusini kujiunga hapo mwaka 2010.Ifikapo mwaka 2050 inatarajiwa umoja huo utakuwa ukiongoza kwa nguvu za kiuchumi na ushawishi duniani.
Akizungumzia kuhusu tishio la umoja huo afisa kutoka wizara ya nchi ya Marekani amesema nchi yake ina mipango madhubuti kuhusiana na Afrika hasa kuhusu muundo wa kiuchumi na kiutawala.
Naye Blinken ameongeza kuwa muundo bora wa kiuchumi wa Marekani ni katika kukuza utwala wa kidemokrasia,kujali haki za binadamu na uwazi katika utendaji wake.