Ummy Mwalimu: Wataalamu wa afya punguzeni semina, wananchi wapate huduma vituoni

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,462
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka wataalamu wa afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa huo chini ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina”, amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha, Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa Serikali imejenga majengo ya hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la wataalamu wa Afya kutoa huduma bora patika vituo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kila kitu katika Sekta ya Afya ikiwemo majengo, vifaa tiba, kuajiri wataalamu na sasa ni jukumu letu wataalamu kutoa huduma bora kwa wananchi kwani ndio dhamira ya Serikali”, amesema Ummy Mwalimu.

Pia, Waziri Ummy Mwalimu ameutaka uongozi wa Mkoa wa Simiyu kuwasimamia madaktari ili wafanye kazi kwa weledi kwa kuangalia historia ya mgonjwa ili apate huduma sahihi na kwa wakati.

Ameongeza kuwa, lengo la Serikali ni kutoa huduma bora za Afya kwa Watanzania na kwa mara ya kwanza Serikali imetoa hela za dawa kwa asilimia 100, hivyo amevitaka vituo vyote vya Afya kuwa na Dawa zote muhimu ili kumsaidia mwananchi kupata huduma za matibabu kwa wakati.

Hata hivyo, Waziri Ummy ametoa rai kwa watoa huduma nchini kuzingatia utumiaji wa lugha nzuri, weledi na maadili na kuzingatia viapo vya wataalam wa afya wakati wa kuwahudumia wananchi.
 
Nchi ikishakuwa ya semina, warsha na makongamano usitarajie uwajibikaji kwa watumishi wa uma.
 
Mlishangilia posho za vikao na safari vilipoongezwa badala ya mishahra .
Kwa Sasa mwendo ni vikao na safari .
 
Sawa lakini hakuna sekta inayohitaji mafunzo ya mara kwa mara kama Afya.Labda kuwe na usisitizaje wa matumizi ya Tehema huku allowance zao zikibaki intact.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Kama mdau wa Afya katika upande wa kilimo Cha Dawa.

Ni surprise kuona mfumo wetu wa Afya ulivyo jaa siasa na si research na ugunduzi katika maswala ya dawa na Tiba nyingine.

China Ina zalisha dawa Herbs na nyinginezo na ni exporter namba moja duniani ,lakini sisi tunalima mbao kisha tuuze halafu tununue, insane!

Hakuna taasisi zinafanya mafunzo ya kilimo Cha madawa, mfano nani anajua kuhusu Yarrow, Comfrey, Raspberry, St. Johns wart, Lobelia, ginseng, borage na nyinginezo ambazo kima kila kijiji au familia zilitakiwa kuelimishwa na kupewa mbegu na wataalamu asi.

Dawa hizi zingetumika kutibu na ziada kuuzwa nnje. Kwa wale wa agribusiness hii ni nafasi kwao kuvuna faida mbili Kwa mara Moja ,upande wa Afya na biashara.

Mimi ni muhuburi wa Tiba Halisi si Tiba Asili
 
Back
Top Bottom