Uchaguzi 2020 Ummy aahidi kumuonesha Mwana FA vichochoro vya Serikali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambaye pia ni mgombea pekee wa Ubunge Jimbo la Tanga Mjini, Leo Septemba 2 ameshirikiana na mgombea wa Ubunge Jimbo la Muheza, Hamis Mwinjuma au Mwana F.A katika kampeni mkoani Tanga

Katika kampeni hiyo, Ummy ameahidi kushirikiana na Mwana FA kumuonesha kote kwa kupita, vichochoro vyote ndani ya Serikali na nje ya Serikali na kumuonesha wadau wote wa maendeleo ndani na nje ya nchi.

ccm hawataki tena wabunge wa kujenga hoja wanataka 2/3 itimie tu jiwe atawale milele. watanzania tusikubali upuuzi huu.
 
JPM hiyo ni sera au kula, tunataka kusikia sera na si vipasho vya kwenye vijora huko mitaanini mzee. Wewe unaonekana ni kiongozi dhaifu kuliko hata huyo uliyetaka kumpeleka kibra, na sasa yupo hai kabisa, Lissu alienda ulaya kupata matibabu na sio km unavyotoa sababu zako za kimbea, ingependeza tukisikia ukiomba msamaha kwa watanzania kwa kushindwa kuweka wazi mpaka sasa ni nani aliyehusika ktk tukio la kutaka kumuua Lissu, napia ulitakiwa kuomba radhi kwa kushindwa kuufanya mji wa dodoma kuwa salama kuliko mahali popote pale, maana tukio lilitokea dodoma, ambapo ni makao makuu ya nchi.
 
Umevuta bhangi za wapi wewe hahahaha... sasa hapa JPM ameingia je??
 
Rungwe ana kura yangu tayari...sera yake ya ubwabwa ndiyo bora kuliko sera za vyama vingine
 
Wakati wananchi wakimshangili mwana masumbwi anayetamba tanzania na kimataifa ndg nwakinyo, niliona mwakinyo akiinua vidole viwili kwa kificho akiwa kwenye uzindunzi wa kampeni za ccm kupitia mgombea wake ndg mwana FA je hii ilikuwa nipicha gani ishara hyo kuonyeshwa na mwakinyo??
Mwana FA ulimwalika mwakinyo? Unajua alichokifanya? Km hujui pitia picha mnato utaona.
Chanzo u-tube.
 
Vidole viwili "V" ni kifupi Cha "Victory" yaani ushindi.

Mwana-FA ana nia ya kushinda kwa hiyo sioni ubaya wa alama "V" kuonyeshwa na Mwakinyo ukizingatia pia kuwa Mwakinyo kaalikwa ili kuunga mkono juhudi za ushindi wa Mwana-FA.
 
Wakati wananchi wakimshangili mwana masumbwi anayetamba tanzania na kimataifa ndg nwakinyo, niliona mwakinyo akiinua vidole viwili kwa kificho akiwa kwenye uzindunzi wa kampeni za ccm kupitia mgombea wake ndg mwana FA je hii ilikuwa nipicha gani ishara hyo kuonyeshwa na mwakinyo??
Mwana FA ulimwalika mwakinyo? Unajua alichokifanya? Km hujui pitia picha mnato utaona.
Chanzo u-tube.
Hiyo maana yake ni victory acha umbumbumbu!
 
Hiyo maana yake ni victory acha umbumbumbu!

Yawezekana kweli mm mbumbumbu nazidi kuuliza ww mbulumbulu! Mbona kaitoa kwa kificho? Kwa woga? Nakwanini ccm hawaitumii km tafsiri yke ndo hiyo? Nakama alikuwa mualikwa yy mwakinyo kwani hakujua ishara za waliomwalika?
Ww mbulumbulu ( mchele wenye kiwango kibovu) kumbe ishara hii unaweza kuitumia hata kanisani kwa maana ya ushindi wa kumshinda shetani???😋😋

Kiujumla mwakinyo kaharibu km alivyohalibu ndg mbowe cku anawafukuza TBC live yy akijua hayupo live.

Nadhani niwakati wa mwakinyo kuomba msamaha km alivyoamliwa mbowe kuomba msamaha.
 
Back
Top Bottom