Umewahi kutembelea familia yenye toto lililodekezwa?!

Mkuu kama ulikuwepo....baada ya kifinyo katulia tuli kama sio yeye mpaka misa inaisha!

Ila yule mtoto wao kwa tabia zile sijui....
Mitoto ya kudekezwa hivo arrgh, inaboa mno, umekafunza adabu siku Nyingine kakifika kanisani katakua kanatulia coz katakua kanakumbuka last time maeneo haya nilichezea kifinyoo
 
Siku hizo kitambo sana bwana nikaenda kwa rafiki yangu hedemora ,Sweden anaitwa Anna Leena, nikambeba dogo mmoja hivi, akanikojolea makusudi ilikuwa mwaka 1992, nilimtandika kofi , hahaa familia nzima ilinichukia kwa kumcharaza dogo ila hawakuwa na jinsi, nikaamua kukausha, ila hawakuchukua hatua zaid maana ingekuwa hatari sana kwangu,

Cc luambo makiadi
 
Kuna siku nilienda mahali na yule mzee wa kukusanya rambi rambi za wasanii sasa kuna watoto wanasoma IS full ung’eng’e wakawa wanamzingua jamaa awachekeshe akawa anazuga nao anaenda nao sawa wazazi wao wakaingia ndani akamvuta mmoja akamkazia macho “oya ntakuzaba vibao mimi siyo babu yenu” afu akamvuta zaidi kama anataka kumuangusha akamrudisha tulicheka balaa madogo wakaenda kulala hatukuwasikia tenaaa
 
Juzijuzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi kama wale anaowaona kwenye Luninga, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea kama vile vitoto vya kwenye Luninga, mwenyewe anakaita junia sijui junia ndio hivyo hivyo, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja, basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala kukatazwa chochote.

Nilipata taarifa kuna siku kalimvua baba yake taulo alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, "No Junia no...! is bad!” Na kucheka cheka huku akisifu, "Tatizo la huyu mtoto ni ana akili za kikubwa” Ene wei siku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu, anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, "Junia no!", anapanda meza mara kabati, jamaa yangu na mke wake utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, "No Junia no" Mara mbili hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, 'Kwa ustaarabu wa nyumba ile na mie nikatoa ya kinafiki, 'No Junia no'.

Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Junia akaenda chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi...! "Leo umekuja kula kwetu?" "Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga chokoleti?" Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele toka jikoni, "Junia yu a veri bed". Sasa chenyewe si kikakosea kikanipanda kichwani na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii zereu.

Basi nilikishika mkono nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho kama kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichin... "We Junya ukinisogelea tena nakukata masikio kabisa".

Eeh bwana we kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza "Junia umefanya nini tena baba?" kimya "Junia what has happened?" kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha nyuma ya gauni la mamake, "Huyu kafanya nini?" Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa... "Wala sijui nimeona tu katimka hapa kaja huko".

Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na kumuuliza, "Junia a yu sik? Unaumwa?" Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa ananyamaza anajua kuna kukatwa masikio.

Wengine hatuangaliagi Luninga ohooo!!

WAZAZI WA ZAMA HIZI HII INATUHUSU ASILIMIA 100!

TUWE MAKINI NA ST FRANCIS SCHOOLS! ZINAFUNDISHA INGLISHI TU SO MALEZI!
SHAURI YETU!
Ahahahaahhahahahahaa

Yani nimecheka na wife hapa. Mkuu safi sana madekezo mengine kwa watoto ni ya kijinga sana kupita kiasi. You have made my Sunday kwa kweli
 
Mitoto ya kudekezwa hivo arrgh, inaboa mno, umekafunza adabu siku Nyingine kakifika kanisani katakua kanatulia coz katakua kanakumbuka last time maeneo haya nilichezea kifinyoo
eti kifinyoo...I wish wazazi wake wabadilike malezi ya yule mtoto!

Hivi ndani wanaishi vipi nae yule dogo???
 
Kuna siku nilivaa suruali kimodo na shart langu la bei mbaya nikaenda kwa baba Brian kumtembelea aisee yule mtoto sijui amefundishwa na nani? Alikuwa anadanda danda kwenye magoti huku anagusa kwenye kijiji lahaula dogo anakanasa goroli moja ya kende zangu then akauliza uncle hapa mbona pametuna kuna nini ,aisee niliona aibu mbele za wazazi wake nikaanza kulaumu kuvaa kimodo changu mpaka leo navaa mabuga.
RAI YANGU: MTOTO MWEUSI ALELEWE KIHIP HOP/KIKACHA YA AFRIKA UKIMLEA KAMA MZUNGU ITAKULA KWAKO.
 
Nilijua huu uzi ni wa mzee GuDume kumbe siyo lkn hata hivyo ni kisa kizur sana chenye mafunzo kwa jamii yetu...niliwahi kumtembelea Bro wangu mmoja mahali kwa bahati mbaya yeye sikumkuta alikuwa nje ya nchi so,ni liishi na watoto wake na mke wake kwa muda mrefu sana,kilichokuwa kinanikera ni watoto wake wadogo walikuwa na tabia mbaya kuliko za Junior...madogo wakimkuta mtu mzima sebuleni anaangalia mpira au taarifa ya habar wao wanabadilisha channel na kung'ang'ania remote control, sasa ikawa wakifanya hivyo inabidi niende kwenye bar ya jirani nikaangalie taarifa ya habar

Huu uzungu unaharibu sana watoto!
 
Kuna siku nilivaa suruali kimodo na shart langu la bei mbaya nikaenda kwa baba Brian kumtembelea aisee yule mtoto sijui amefundishwa na nani? Alikuwa anadanda danda kwenye magoti huku anagusa kwenye kijiji lahaula dogo anakanasa goroli moja ya kende zangu then akauliza uncle hapa mbona pametuna kuna nini ,aisee niliona aibu mbele za wazazi wake nikaanza kulaumu kuvaa kimodo changu mpaka leo navaa mabuga.
RAI YANGU: MTOTO MWEUSI ALELEWE KIHIP HOP/KIKACHA YA AFRIKA UKIMLEA KAMA MZUNGU ITAKULA KWAKO.
:D:D:D:D:D:D:D
 
bahati mbaya yeye sikumkuta alikuwa nje ya nchi so,ni liishi na watoto wake na mke wake kwa muda mrefu sana
Kwenye post yako hapa ndio ninishida napo mkuu. Huoni kama hao madogo walikua wanakufanyia kusudi ili ukereke uondoke maana yaelea uli over stay wakati baba mwenye nyumba mwenyewe hakuwepo ingawa sijajua uhusiano wenu upo vipi
 
Back
Top Bottom