Umewahi kutembelea familia yenye toto lililodekezwa?!

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Juzijuzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi kama wale anaowaona kwenye Luninga, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea kama vile vitoto vya kwenye Luninga, mwenyewe anakaita junia sijui junia ndio hivyo hivyo, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja, basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala kukatazwa chochote.

Nilipata taarifa kuna siku kalimvua baba yake taulo alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, "No Junia no...! is bad!” Na kucheka cheka huku akisifu, "Tatizo la huyu mtoto ni ana akili za kikubwa” Ene wei siku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu, anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, "Junia no!", anapanda meza mara kabati, jamaa yangu na mke wake utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, "No Junia no" Mara mbili hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, 'Kwa ustaarabu wa nyumba ile na mie nikatoa ya kinafiki, 'No Junia no'.

Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Junia akaenda chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi...! "Leo umekuja kula kwetu?" "Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga chokoleti?" Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele toka jikoni, "Junia yu a veri bed". Sasa chenyewe si kikakosea kikanipanda kichwani na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii zereu.

Basi nilikishika mkono nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho kama kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichin... "We Junya ukinisogelea tena nakukata masikio kabisa".

Eeh bwana we kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza "Junia umefanya nini tena baba?" kimya "Junia what has happened?" kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha nyuma ya gauni la mamake, "Huyu kafanya nini?" Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa... "Wala sijui nimeona tu katimka hapa kaja huko".

Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na kumuuliza, "Junia a yu sik? Unaumwa?" Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa ananyamaza anajua kuna kukatwa masikio.

Wengine hatuangaliagi Luninga ohooo!!

WAZAZI WA ZAMA HIZI HII INATUHUSU ASILIMIA 100!

TUWE MAKINI NA ST FRANCIS SCHOOLS! ZINAFUNDISHA INGLISHI TU SO MALEZI!
SHAURI YETU!
 
Malezi yamebadilika kwa kasi sana, wazazi wengi ukiwauliza wanakwambia hawezi kumchapa mtoto. Tabia chafu tulizokuwa tunaonywa sisi na wazazi wetu siku hizi zimekuwa tabia za ufahari mzazi kumuona mwanae akizifanya.

Tunafurahia mtoto wangu mtundu huyoo!! Matokeo yake ni tabia kama hizo za mtoto junia!!

Kwa muona mbali anaona kizazi kinachokuja miaka 100 ijayo jinsi kitakavyokuwa.
 
Juzijuzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi kama wale anaowaona kwenye Luninga, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea kama vile vitoto vya kwenye Luninga, mwenyewe anakaita junia sijui junia ndio hivyo hivyo, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja, basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala kukatazwa chochote.

Nilipata taarifa kuna siku kalimvua baba yake taulo alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, "No Junia no...! is bad!” Na kucheka cheka huku akisifu, "Tatizo la huyu mtoto ni ana akili za kikubwa” Ene wei siku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu, anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, "Junia no!", anapanda meza mara kabati, jamaa yangu na mke wake utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, "No Junia no" Mara mbili hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, 'Kwa ustaarabu wa nyumba ile na mie nikatoa ya kinafiki, 'No Junia no'.

Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Junia akaenda chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi...! "Leo umekuja kula kwetu?" "Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga chokoleti?" Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele toka jikoni, "Junia yu a veri bed". Sasa chenyewe si kikakosea kikanipanda kichwani na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii zereu.

Basi nilikishika mkono nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho kama kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichin... "We Junya ukinisogelea tena nakukata masikio kabisa".

Eeh bwana we kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza "Junia umefanya nini tena baba?" kimya "Junia what has happened?" kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha nyuma ya gauni la mamake, "Huyu kafanya nini?" Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa... "Wala sijui nimeona tu katimka hapa kaja huko".

Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na kumuuliza, "Junia a yu sik? Unaumwa?" Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa ananyamaza anajua kuna kukatwa masikio.

Wengine hatuangaliagi Luninga ohooo!!

WAZAZI WA ZAMA HIZI HII INATUHUSU ASILIMIA 100!

TUWE MAKINI NA ST FRANCIS SCHOOLS! ZINAFUNDISHA INGLISHI TU SO MALEZI!
SHAURI YETU!
Nimecheka sana hii story.
 
Hahaaaa usinikumbushe nilishawah mwagia mtoto wa jirani sufuria la unga kichwani na kpgo juu, kikanichoropoka kikakimbia huko nje na mayoe, kila mtu n kicheko mana kilikua kama msukule, Kilianza kua na heshma kuanzia hapo, kamefka kwao hakakusema, mama yake akawa anaulizia kwa vitsho nikamfuata mpk kwake nikamwambia ni mimi, Kumbe Mume alikua anamkanya sana mke wake asimdekeze mtoto, Yule mzee akaniambia hamna kesi kijana wangu we nenda kwa aman, nikawaacha wanagombana
 
Back
Top Bottom